Kipindupindu chaibuka Dodoma kwa kasi

RUCCI

JF-Expert Member
Oct 6, 2011
1,701
1,714
Kaimu Mganga mkuu wa mkoa wa Dodoma, Dk, Nassoro Mzee amesema tangu kuzuka kwa ugonjwa huo wilaya ya Kondoa pekee imegundulika kuwa na jumla ya wagonjwa 27.

Amesema tangu kuzuka kwa ugonjwa huo Agost mwaka jana Wilaya ya Kondoa ilikuwa haijawahi kuripotiwa kwa mgonjwa wa kipindupindu lakini ugonjwa huo umezuka na mmoja kati ya hao ameripotiwa kufariki dunia.

Amesema kutokana na hali hiyo juhudi mbalimbali zimekuwa zikichukuliwa ikiwemo kutoa elimu juu ya kuudhibiti ugonjwa huo, kubaini chanzo cha kutokea kwa milipuko hiyo ambapo kwa kushirikiana na wizara ya maji wamekuwa wakiyapima maji yanayotumiwa na wananchi na kubaini kama baadhi ya visima vinavyotumiwa na wananchi vina vimelea vya ugomnjwa huo.

Amebainisha kuwa mpaka jana wagonjwa walioripotiwa kuwa na kipindupindu ni 25 ambapo wilaya ya Mpwapwa ikiwa na wagonjwa wane, Manispaa kumi na Kondoa wagonjwa 11.

Daktari huyo amesisitiza kuwa kipindupindu katika mkoa wa Dodoma bado kipo na kutoa wito kwa wananchi kuzingatia kanuni za afya kwa kuzingatia suala la kuchemsha maji kabla ya kunywa, kunawa mikono kabla na baada ya kula, kunawa mikono watokapo chooni, kutojisaidia vichakani na kuzingatia matumizi ya vyoo bora na kusimamia sheria ndogo ndogo zilizopo.
 
Na hivi hakuna safari za nje, utasikia Wizara imetuma wataalamu kutoka makao makuu kama hamsini kwenda kupiga Kambi huko kwa wiki nne ili kusaidia kupambana na ugonjwa huo, wakifika huko wanakaa tu na kuchukua data baada ya wiki wanageuza wakati wamevuta mshiko wa mwezi, nchi hii bana we acha tu.
 
Na hivi hakuna safari za nje, utasikia Wizara imetuma wataalamu kutoka makao makuu kama hamsini kwenda kupiga Kambi huko kwa wiki nne ili kusaidia kupambana na ugonjwa huo, wakifika huko wanakaa tu na kuchukua data baada ya wiki wanageuza wakati wamevuta mshiko wa mwezi, nchi hii bana we acha tu.


Mbinu za kuiibia serikali zinazidi kubuniwa kila kukicha, tena hawakai muda wote huo, wanakaa wiki moja tu wanasepa lakini wanakuwa wamesaini posho ya mwezi mzima
 
CCM ndio wamekipeleka huko
kwani hawa wateule wa JPM wenye ma PhD wanafanya nini....kipindupindu kila kona utadhani nchi hii ya mataahira wasiojitambua kwa lolote..ni aibu kuwa na wataalamu wabobezi (madaktari, maprofesa) ambao wanafanya kazi za utawala badala ya kutumia utaalamu wao kutafuta ufumbuzi wa matatizo sugu kama kipindupindu.....shame on you doctors & professors of Tanzania
 
Back
Top Bottom