Kipindi kigumu kama hiki JK aliwatumia sana Steven Wassira na Lukuvi, sasa Baraza la Mawaziri kimya!

iparamasa

JF-Expert Member
Nov 14, 2013
13,437
14,924
Si vibaya kukumbuka awamu ya nne NA mambo yake!

Mkwere alipoona mambo yamekwama saana, aliwatumia mawaziri wake kufanya mijadala na kutafuta muafaka wa mambo na wadau mbalimbali.

Ni pale tu alipoona mambo yametatizika,si mara moja aliwatumia lukuvi na wasira kuongea na vyombo vya habari kutuliza hali,
Kwa sasa sijaona kama kuna wa kutumwa,Baraza zima la mawaziri liko kimya kabisa kama hawapo!!
 
Mzee lukuvi,ardhi kama imekubana rudi ofisi ya waziri Mkuu,sera uratibu na bunge,

Lukuvi anajua the rules of the game and the rules of engagement
 
No team work.
Kila MTU ana hofu ya kutumbuliwa.
Mtumbuzi amegeuka kuwa msemaji wa mamlaka ya hali ya hewa.
Mtumbuzi kisha sema hamna ukame na wala hamna njaa.
Mifugo inayokufa, imeamua yenyewe kugoma kula.
Na ng'ombe watatu wabadilishwe kwa debe MOJA LA mahindi.
 
Baraza zima limewekwa mfukoni mwa suruali ya mtu yule ingawa sijui ni mfuko wa kushoto au wa kulia wa suruali yake.
Suleiman jaffo anasikika....japo muda unavyosogea,naona sauti yake inasikika kwa mbaaaaali,kama anatokomea porini,ila sauti yake inasikika,japo sasa ni kama yuko mbali,nadhani anachanja mbuga au pumzi zinaleta shida
 
Hawataki kumuudhiiii.....mfalme maana wengine ambao wengi wao hakuwataka!!
 
Katika serikali ya mzee wa bashasha, Tyson alikuwa kiungo mkabaji ( Mkata umeme), alikuwa mahiri kweli yule jamaa, Nakumbuka alivyokuwa akienda kwenye mijadala mbalimbali kama vyuoni kutetea positions za mukulu.

Katika awamu hii sijaona mtu akicheza kama midfield wote kimyaaa, sijui kwa nini!.
 
Katika serikali ya mzee wa bashasha, Tyson alikuwa kiungo mkabaji ( Mkata umeme), alikuwa mahiri kweli yule jamaa, Nakumbuka alivyokuwa akienda kwenye mijadala mbalimbali kama vyuoni kutetea positions za mukulu.

Katika awamu hii sijaona mtu akicheza kama midfield wote kimyaaa, sijui kwa nini!.
Kweli kabisa,hata kwenye bunge la katiba alimuokoa mkulu,
 
Back
Top Bottom