Makusudically
JF-Expert Member
- Feb 3, 2014
- 2,203
- 1,235
Mimi huwa mpenzi na mfuatiliaji wa kipindi hiki kwa karibu sana. Kipindi cha leo nikiwa na Wenzangu wapatao 12 tulishanga sana mwandaaji wa kipindi hiki Mwasalanga, hatukuelewa ama alifanya makusudi au ilitokea bahati mbaya, Mgeni aliye mualika kuja kwenye kipindi alijitambulisha kwa jina la Seleman Msuya kama sikosei, na kuwa ni msomi na mwandishi mkongwe, wakati tunamsikiliza, kwa hakika tulishindwa kumwelewa, je aliaalikwa ili kuja kuishambulia Serikali?
Mara nyingi alisikika akisema Maamzi aliyotoa Dr.H.Mwakyembe ni kukurupuka, nakwamba Kiongozi wa juu hana mawasiliano ya karibu nawaziri wake. Na kwa ufupi serikali hii siyo makini. Msuya hapa hapa hatumuelewi, anadhani nchi ni kama familia kwamba kila asubuhi unaweza kuwaamsha wote ukawaambia nataka leo muende shambani.
Urais ni taasisi, kitendo cha Rais kutengua kauli ya waziri wake siyo cha ajabu hadi Mwasalanga akiandalie kipindi maalumu na kuizodoa Serikali kwa kumtumia Msuya ambaye dhahiri alijionesha ni "partson". Mara aongelee Bashite sijui alikuwa analenga nini, kama anachuki na Serikali si angeweka wazi tu kuliko kupitishia chuki zake kwenye kipindi ambacho sisi ni wapenzi wake?
Ikumbukwe kuwa ndugu yangu Mwasalanga kitendo cha Rais kutengua kauli ya waziri ni chakawaida na siyo kimeanza leo nasiyo Tanzania peke yake, Mfano mwaka 1974/75 Nwl Nyerere alitengua kauli ya Waziri mkuu wake Mh.Rashid Kawawa kuhusu kufunga maduka ya watu binafsi na kuyapa nafasi maduka ya vijiji vya ujamaa.
Nyerere alisimama na kufuta amri iliyotolewa na Waziri mkuu nakurekebisha kuwa maduka hayo yatajifunga menyewe. Sasa mbona haikuonekana ajabu, Pia Rais wa Zimbabwe naye aliwahi kufanya hivyo hivyo kwa Waziri wake wa Aridh wakati wa Land Reform, Peter Both hivyo hivyo kwa Waziri wake wa mambo ya ndani wakati wa ubaguzi, Donard Regan wa USA alifanya hivyo hivyo kwa balozi wake Ubelgiji, San Abacha wa Nigeria alifanya hivyo hivyo kwa Waziri wake wa Nishati.
Sasa Leo wewe Mwasalanga na huyo Msuya kwa Makusudi mazima mnaamua kuizodoa na kuifedheshesha nchi yenu wenyewe, kana kwamba kauli hiyo ni mbaya nakwamba Serikali siyo makini. Jamani kuweni wazalendo.