Kipimo cha UDINI na UKABILA ni nini? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kipimo cha UDINI na UKABILA ni nini?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwananchi Mtanzania, Jul 24, 2012.

 1. Mwananchi Mtanzania

  Mwananchi Mtanzania Member

  #1
  Jul 24, 2012
  Joined: Jul 3, 2012
  Messages: 92
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sisi kama Watanzania inabidi tufanye kazi kwa ajili ya hatma ya taifa moja, lenye nguvu na umoja. Hivi ile hali ya zamani imekwenda wapi kwa watu wa dini zote kupendana na kushirikiana?
  Mimi kama mtanzania ningependa kama Bwana Juma akitoka msikitini, kama ni usiku na njia ina vibaka, awe huru kugonga hodi kwa Yosefu amsindikize. Na kama Yosefu siku ametoka kanisani na akapata kiu, basi awe huru kuomba maji hata chakula ka bwana juma. Nina wasi wasi shutma nyingi watu wanazotoleana humu si za kweli.
  Ifike kipindi tuwe na aibu. Siwezi leo nikamtukana Mkristo au Muislam, Mhaya, Mchaga, Nnyakyusa, Mhehe, Mkinga, Mbena… nk katika Jamii Forum, ati tu kwa sababu identity yangu haijulikani, wakati katika hali halisi, nina marafiki wa imani na makabila husika. Hivi unajisikiaje unavyomshutumu mtu wa imani fulani, halafu huko mabara barani unapata huduma kutoka kwake? Ni nani ambaye akienda dukani, akienda ofisini, akienda polisi, akipanda dala dala, e.t.c hua anauliza imani au kabila la mtu ambaye ana msaidia? Sasa hii tabia ya leo ya kuanza kubandikana majina: Fulani Mkabila, Fulani mdini inaanzia wapi? Ni kweli wana hizi tabia, au mengine ni matatizo yetu wenyewe?
  Labda niulize tu: Kipimo cha UDINI na UKABILA ni nini? Ni idadi kubwa ya marafiki na maswahiba wa imani husika? Sidhani. Kila mtu amezaliwa, kukulia, kusoma na kuishi katika maeneo Fulani. Kwa hali hiyo basi, historia yako ya maisha ina mchango mkubwa wa aina ya marafiki zako. Kama mtu umekua katika meneo ya mchanganyiko, ni lazima utakua una mchanganyiko wa marafiki na jamaa tofauti, ukilinganisha na mtu ambaye sehemu kubwa ya maisha yake imekua ni katika aneo moja, au lenye kabila au imani Fulani ambayo hapo ndio dominant. Hivyo basi, sidhani kama kuna mtu hua anachagua azaliwe au aishi katika eneo Fulani. Hivyo basi, pahala mtu alipozaliwa, shule aliyosomea, mambo kama kama mafundisho, madrass, nature ya familia husika (mchanganyiko kiasi gani) e.t.c. hua vinachangia sana katika aina ya mchanganyiko wa marafiki.
  Sasa swali la kujiuliza, ni wangapi kati yetu, wanaosema Fulani "Mdini" (iwe Mkristo or Muislamu) au ni Mkabila, wamewahi kubaguliwa kidini au kikabila na mtu husika? Hua tunatumia vigezo gani? Hisia, minong'ono, kutokuaminiana, idadi ya marafiki zake, au ni namna gani anavyopenda imani yake? Nitashangaa kama mtu akihukumiwa kwa kupenda imani yake, kwa sababu after all hiyo ni haki yake. Sidhani kama mtu ameamua kua thabiti katika Uislam au Ukristo, leo akabandikwa jina la "Mdini", kwa sababu otherwise utataka huyo Muislam au Mkristo afanye mambo kinyume na imani yake – hapo, tutatafutana lawama bure!
  Imefikia wakati sisi watanzania tunapoteza hata uwezo wa kufikiri katika mambo fulani. Kwa nyakati tofauti, kwa mfano, nimesoma Mz Ruksa, na Mh Samwel Sitta, wote wakishutumiwa kua wadini, kisa tu walisema "Kiongozi bora ni Mcha Mungu"! Hivi leo msemo huu wa kiswahili wa kawaida umegeuka kua UDINI? Wote walihukumiwa "wadini" kutokana na kauli inayofanana. Kilicho wahukumu, nafikiri, ni imani zao. Ni lazima tutafakari mara mbili kabla ya kutoa kauli zetu.
  Kimtazamo wangu, ukimshutumu Fulani kua ni mdini au mkabila, eti tu kwa sababu ana marafiki wengi wa imani au kabila fulani, na hilo linakukera, basi wewe ndiye mdini au mkabila. Na ni lazima uanze kua na mazoea ya kukubali hali ambayo si kila sehemu utakuta watu wenye kabila au imani yako.. wanaweza wawe wachache, au wasiwemo kabisa. Cha muhimu ni kuangalia unapata haki yako? Anayefanya kazi hiyo ana maadili na taaluma husika? Na mambo haya, si ya kuyatolea maamuzi kihisia au ki minong'ono.
  Iwapo ukaangalia chama cha siasa, na ukakihukumu tu kina udini au ukabila kwa sababu ya viongozi wake, yawezekana pia una tatizo la udini au ukabila, kwani siasa za nchi hazihusiani na ibada au matambiko (kwa msemo wa Mwalimu), na hivyo basi, sioni sababu kwa nini ukereke eti ni kwa sababu gani viongozi wa chama Fulani si wa imani au kabila inayo fanana nay a kwako.
  Mtu akiteua viongozi, ukaangalia tu ukaona ambao hawafanani na imani yako ni wachache, halafu ukaamua kumshutumu mfanya uteuzi ni mdini au mkabila, basi wewe ndiye una matatizo, kwa kua tunajua wazi kwamba katika teuzi za kitawala, iwe ngazi ya kijiji au hata uwaziri, kwa msemo wa Mwl Nyerere, sio nafasi za matambiko au Ibada... Hivyo basi, suala la wangapi ni kabila gani au wangapi ni dini gani, kama linakukera, basi wewe ndiye unatatizo (haijalishi unaitwa Gabriel au Hussein), na ni lazima ufanye kazi kuliondoa moyoni mwako.
  Nina wasi wasi, wengi tunaotoa shutuma za UDINI au UKABILA, sisi ndio tuna matatizo, na si hao tunao watuhumu.
  Mungu ibariki tanzania
   
 2. Malaria Sugu

  Malaria Sugu JF-Expert Member

  #2
  Jul 24, 2012
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 2,653
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mwananchi Mtanzania Christianity and Islam are the predominant religions of Tanzania. About 40-45% of the population practice Christianity, about 35-40% practice Islam. The rest of the population adhere to traditional beliefs, most of which centre around ancestor worship and nature-based animism. Most Christians live on the mainland, where missionary stations and schools reach deep into the continent. Islam is the major religion of the coastal areas but is also practiced further inland along the old caravan routes.
  Religion plays a large part in the daily life of Tanzanians. In Christian areas, families attend church together dressed in their Sunday best. Church services always involve singing and the hymns often sung in complex harmonies spill out to the streets outside. Easter and Christmas are major events in Tanzania, with services and celebrations often extending far into the day and night. The lunar month of Ramadan is an important time for Muslims around the country, who fast from food and drink from sunrise to sunset. After Ramadan comes the Eid, a time of feasting and festivity for the whole community. Tanzania’s Asian religious minority includes Hindus, Sikhs, and Ismailis.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 3. Mwananchi Mtanzania

  Mwananchi Mtanzania Member

  #3
  Jul 24, 2012
  Joined: Jul 3, 2012
  Messages: 92
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Poor The reason I posted that, is because nowadays, people are easily accusing politicians and political parties of UDINI or UKABILA, and of course, nono of those giving the said accusation can actually prove that he/she was ever marginalised by persons or political parties to which he/she throw accusations. I have a feeling that some of us find it easy just to raise such issues, for political reasons or for reasons known to ourselves, without carefully thinking of the dangers of doing so. Teke the following examples: If a minister appoints some officials, some will quicly want to compare the tribal or religious affiliations of the appointees and the Minister. I think we witnessed this when Hon. Mwakyembe appointed the new board of ATCL. Or, think of accusations thrown to CHADEMA and CUF; or, when a president appoints people to hold certain positions, if majority are Christians, some will say that the system is "pro-Christians" (because now the president is a muslim), and if it happens that the majority are Muslims, some will say that the president is "pro-Muslims". So, in all these circumstances, people are moved by "feelings" instead of "facts", and we want to legitimise a fact that "each religion and each tribe, must, at every particular moment, have a representation in political related activities". I think this is wrong. This worries me a lot.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 4. Kiranja Mkuu

  Kiranja Mkuu JF-Expert Member

  #4
  Jul 24, 2012
  Joined: Feb 18, 2010
  Messages: 2,100
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Kikwete na wenzake wanapindisha mafundisho ya baba wetu wa Taifa.
  Hali mbaya ya taifa letu imesababishwa na rais wetu
   
 5. Hayajamani

  Hayajamani JF-Expert Member

  #5
  Jul 24, 2012
  Joined: Jul 2, 2012
  Messages: 883
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Ninavyo fahamu ni:
  1: Kila kiongozi akichaguliwa kuangalia ni wa dini gani, dini yetu wapo wangapi
  2: Kutaka kujua dini fulani tupo wangapi, badala ya kushughulikia matatizo chungu nzima ya kifamilia/jamii zetu yanayotukabili kama vile ukosefu wa elimu, kazi, maadili mabovu, magonjwa n.k.
  3: Kutaka kuanzisha taasisi mbalimbali kwa ajili ya kututenga na wengine kama vile mahakama, please expand more ...
  4: Kung'ang'ania maitikadi ya kigeni na kuyatumia kama silaha kubagua wengine, kuwa, kuchoma n.k.
  5: Kukataza waabudu wake wasishiriki kazi za maendeleo kama vile sensa n.k.
  6; ......
  7: .......
   
 6. K

  KISIMASA Member

  #6
  Jul 24, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 39
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  He who praises the rain, has seen it. Do not under-estimate any accusation until there is a proof beyond reasonable doubt. Again yes there must be affiliation. You heard from the parliament recently " will the president choose an advisor who he is not affiliated with"???? What other evidence do you need?
   
 7. Shinto

  Shinto JF-Expert Member

  #7
  Jul 24, 2012
  Joined: Dec 6, 2010
  Messages: 1,781
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Tizama CHADEMA utauona huo UKABILA, UDINI na UKANDA!
   
 8. C

  Careboy wamuntere Senior Member

  #8
  Jul 24, 2012
  Joined: Jul 9, 2012
  Messages: 163
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hizo takwimu umezipata wapi ndg, na ni sensa ya mwaka gani iliyoonyesha kipengele cha dini, unajua masuala kama haya ndo yanayoleta hisia kwamba watu wanainterest binafsi ktk hizi takwimu za kitaifa, leo unaongelea waislam kadhaa, wakristo kadhaa. uliwahesabia wapi>? hebu tuwe makini na hizo comment zenu, zinaweza kuzua hisia mbaya miongoni mwa jamii zetu.
   
 9. Mwananchi Mtanzania

  Mwananchi Mtanzania Member

  #9
  Jul 24, 2012
  Joined: Jul 3, 2012
  Messages: 92
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nina wasi wasi na hoja ya kushutumu Marais wa Tanzania kwa Udini au Ukabila. Almost wote wamebandikwa tuhuma hizi. Sikubaliani na hoja hii:
  Tatizo la hoja hii ni kwamba, hakuna Rais ambaye hajawahi kubandikwa tuhuma hizi.. inategemea tu ni dini gani. Mkapa na Baba wa Taifa walisemwa vibaya pia. Rais Mwinyi naye alisemwa vibaya. Sasa does it mean miaka yote tumekua tukichagua wadini? I do not think so. Miongoni mwetu, tuna matatizo.
  I got you:
  It is wrong from the beginning, katika masuala purely ya ki serikali, eti kusema una balance kabila or itikadi za kiimani. Hizi zipo nyingi, na cha muhimu ni uwezo wa mtu na kutenda haki. Bhati mbaya, miongoni mwetu watanzania, wapo tunaokerwa tu, eti kwa sababu Fulani katika shughuli Fulani, hafanani na mimi kiimani, au marafiki zake wengi ni wa imani au kabila Fulani. Pia tuna tatizo la kufikiria kwamba chochote kinachosemwa na viongozi wa dini ni sawa, bila kudhani kwamba na hawa ni binadamu, sio malaika, and for that matter, hua wana makosa. Viongozi wetu wa kiimani, wawe wanaitwa wachungaji, au ma ustaadh, ma mufti, au maaskofu, wengi wamejikuta at times wanavamia hoja za kisiasa or za kisheria, wakati wao si wanasiasa wala si wanasheria. Wanasema wanafanya mambo kwa maslahi ya waumini wao, lakini wamechangia kwa kiasi kikubwa kutugawa wananchi. Hili suala la sense.. likiwemo, au lisipo kuwemo, mimi sioni tofauti yoyote. So, I do not see any reason kwa nini watu washikie bango kwamba lazima liwepo, au lazima lisiwepo…
  Bwana
  Hili la CHADEMA, au tuseme hata CUF, si vizuri la kuliangalia juu juu. Wakati mwingine nahisi hivi vyama vinaandamwa kwa sababu ya kisiasa, na kama kuna viongozi wa dini wameshawishika, basi wameingizwa "mkumbo"! Nitatoa mifano ya vyama kadhaa:
  Ikumbukwe kwamba Mwaka 1992, ulipoanza mfumo wa vyama vingi, kwa mfano, Waanzilishi wa CUF walikua ni James Mapalala na Dr. Chemponda. Wafuasi wengi kutoka Pemba walijiunga baada ya Maalim seif kujiunga na CUF, na hili lina historia ya mbali sana (upemba vs uunguja). Sasa coincidentaly, wapemba wengi walikua coast, na huko ndiko cuf ikapata ufuasi. Sidhani kama ni sahihi, kulaumu CUF kwa kuwa na Waislam Wengi.
  Kuhusu CHADEMA, waliambiwa kwamba ni wa "Ukanda". Lakini tukumbuke kwamba hii tuhuma alipewa Lyatonga Mrema mwaka 1995 wakati yuko NCCR, na sasa hapewi tena wakati yuko TLP! John Cheyo, na chama chake cha UDP wala hatusikii akiandamwa. Na kile chama cha Peter Kuga Mzirai chenye wafuasi Upareni pekee, wala hakiandamwi. Nafikiri hapa, inabidi tuwe waangalifu. Tuangalie ukweli wa mambo kiundani. CCM bahati yao wamekaa muda mrefu, kwa hiyo wamekua wana matawi kote kote, lakini katika hali halisi, kila chama cha siasa hua kina "political base", ambayo historia yake inatokana na mambo mengi, ikiwemo waanzilishi. Of course kwa hili, nitawalaumu viongozi wa makundi ya kidini kwa kukaa "kimya" bila kuwakumbusha waumini wao kwamba wana uwezo wa ku support au kupinga chama chochote kile… naona wamekua kimya kidogo, na hapa ndipo ninaposema, hawa ni binadamu, lazima wakosolewe. Si kila wanachokifanya ni sahihi.
  , well said. Zamani kidogo, miaka kama miwili hivi imepita, Niliwahi kukutana na mabwana Fulani kwenye basi walikua wako bize wanachanganua hoja hiyo. Sikuwaelewa, kwa sababu nao walikua wanatoa takwimu ambazo sijui hata zimetoka wapi. Kwa kweli sikuweza kujua kama walikua wanaitwa kina Robert au kina Juma, kwa sababu kwenye mazungumzo yao yote (mimi nilikua kiti cha nyuma yao), si kuweza kujua haswa walikua wanadhamiria nini. Any way, niliachana nao. I was not interested.
   
Loading...