Kipima joto cha ndoa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kipima joto cha ndoa

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Kimbweka, Aug 7, 2012.

 1. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #1
  Aug 7, 2012
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  [​IMG]


  Kuna mahali wanandoa waliulizwa swali hili:
  Je, mke uliyenaye au mume uliyenaye sasa kama ingetokea sasa hivi iwe ni ule wakati unachumbiana naye kuwa mke au mume ungemchagua kuoana naye?
  Zaidi ya asilimia 70 walisema wasingekuwa tayari kuoana nao kwani wamegundua kuna tofauti kubwa sana ya mtu aliyenaye sasa na yule alikuwa kabla ya kuoana.
  Je, wewe ungeliulizwa swali hili leo ungekuwa na jibu gani?
  ... Ukweli jibu unalo wewe ndani ya moyo wako na ni siri yako.
  Ukitaka kujua ndoa yako ina joto kiasi gani unaweza kujibu maswali yafuatayo kwa usahihi na uaminifu kabisa kwa kuchagua jibu sahihi kwako.

  1. Tunaweza kumaliza mgogoro au tofauti ya mgongano wa kimawazo chini ya dakika 15.
  A. Hata siku moja.
  B. Mara chache sana
  C. Mara kwa mara
  D. Mara zote

  2. Huwa tuna tabia ya kumaliza matatizo yetu kabla ya kulala
  A. Hata siku moja
  B. Mara chache sana
  C. Mara kwa mara
  D. Mara zote
  3. Huwa nawaza kuhusu talaka
  A. Hata siku moja
  B. Mara chache sana
  C. Mara kwa mara
  D. Mara zote

  4. Namkumbatia na kumpa busu mpenzi wangu kwa mahaba
  A. Hata siku moja
  B. Mara chache sana
  C. Mara kwa mara
  D. Mara zote
  5. Mapenzi katika ndoa yetu yanaridhisha sana
  A. Hata siku moja
  B. Mara chache sana
  C. Mara kwa mara
  D. Mara zote
  Hadi hapo naamini umepata picha kamili ya wapi unaelekea na mpenzi wako.
  Je, yafuatayo nayo ni wimbo wa kila siku katika ndoa yako?
  Kama ni kweli basi unahitaji msaada haraka iwezekanavyo.
  Mawasiliano ovyo
  Hakuna tendo la ndoa na kama lipo basi ni bora wajibu hakuna ladha halisi
  Kupungua kwa hamu ya tendo la ndoa
  Hakuna mahaba
  Hakuna kutiana moyo wala kupeana asante
  Migogoro isiyoisha
  Kuumizana kihisia
  Kukosa uaminifu kati ya mwanandoa
  Migogoro ya matumizi ya fedha
  Tabia ya kukefyakefya

  AMEN....................!!!!!
   
 2. Nambe

  Nambe JF-Expert Member

  #2
  Aug 7, 2012
  Joined: Jan 18, 2011
  Messages: 1,455
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  mh.................bitter truth..lol
   
 3. N

  Neylu JF-Expert Member

  #3
  Aug 7, 2012
  Joined: May 28, 2012
  Messages: 2,650
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Ngoja waliopo kwenye ndoa waje..
   
 4. K

  KipimaPembe JF-Expert Member

  #4
  Aug 7, 2012
  Joined: Aug 5, 2007
  Messages: 1,287
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Majibu yako kwenye red. Msaada uko wapi?? Uweke hapa wote wanufaike!!
   
 5. Hayajamani

  Hayajamani JF-Expert Member

  #5
  Aug 7, 2012
  Joined: Jul 2, 2012
  Messages: 883
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Kadiri mlivyo jaaliwa, hata mara moja au mara nyingi tuu, bila kujali ni wapi ilimradi kuwe na faragha mtu asiwa chabo, hata jikoni, hata sebuleni, hata bafuni kama anafua na wewe mfue tu.
   
 6. Roulette

  Roulette JF-Expert Member

  #6
  Aug 7, 2012
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 5,618
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Msaada wangu:tekeleza Mawazo yako ya talaka!
   
 7. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #7
  Aug 7, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,963
  Likes Received: 1,852
  Trophy Points: 280
  mmh! aisee sijui wenzangu ila kwangu mimi huwa hii ni institution isiyohitaj umri wala phd bali maturity ya akili na busara zaid.
   
 8. Asulo

  Asulo JF-Expert Member

  #8
  Aug 7, 2012
  Joined: Jun 25, 2012
  Messages: 733
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Kipimajoto kizuri sana mkuu kwa wanandoa.
  Hapa kila mtu anaweka majibu yake na kutafakari mwenyewe moyoni kama anamapungufu gani.
  Ila ni vyema kwa kudumisha ndoa zetu.
   
 9. K

  KipimaPembe JF-Expert Member

  #9
  Aug 8, 2012
  Joined: Aug 5, 2007
  Messages: 1,287
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Thanks Roulette
   
Loading...