Kipigo ndani ya kambi ya jeshi chadaiwa kusababisha kifo cha konda wa daladala

kabon14

JF-Expert Member
Jun 14, 2016
1,233
867
index.jpeg

Salim Kassim enzi za uhai wake
Kondakta wa daladala linalofanya safari zake kati ya Nguvumali hadi Raskozone, Salim Kassim amefariki dunia baada ya kudaiwa kushambuliwa ndani ya kambi ya jeshi jijini hapa.

Kwa mujibu wa habari zilizopatikana na kuthibitishwa na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tanga, Benedict Wakulyamba, kondakta huyo alikufa wakati akipelekwa katika Hospitali ya Mkoa ya Bombo na chanzo cha kifo bado kinachunguzwa.

Mwananchi ilielezwa kuwa tukio hilo lilitokea juzi usiku, ambapo mashuhuda walidai kuona kondakta huyo akichukuliwa na wanajeshi na kuingizwa kambini na baadaye alitolewa akiwa hajitambui

Akizungumzia tukio hilo, Khalid Juma mkazi wa Nguvumali jijini hapa alisema askari hao wamekuwa na desturi ya kuwapiga wananchi bila kuchukuliwa hatua zozote za kisheria.

“Tumekuwa tukipata vipigo kila wakati, licha ya viongozi kupata taarifa za matukio hayo wamekaa kimya na hili tukio ni la tatu kutokea hapa,” alidai Khalid.

Diwani wa Kata ya Nguvumali ambaye pia ni Meya wa Jiji la Tanga, Alhaji Mustapha Selebosi alisema sababu za kipigo hicho ni mwanafunzi wa shule moja jijini Tanga ambaye ni mtoto wa ofisa wa JWTZ kuzozana na kondakta.

Chanzo: Mwananchi
 
Duu yaani sababu ni mwanae kuzozana na kondakta ,sasa huyo kulikuwa na sababu gani ya kumpiga ? Mngempa adhabu tu ya kuogea miche mitatu ya sabuni ya mbuni na maji yasiyozidi kikombe kimoja mbona angenyooka

Anyway R.I.P
Siku hizi watoto hawa hawajui in adhabu gani za kumpa raia asikusahau,matokeo yake wanaingiza na mihemko huko, yanawatokea puani.

Umeishawahi kushuhudia mtu anamwagilia miti ya miembe mpaka ialike maua???
 
We nawe unatumia nyayo kufikiria. Huyo mwanafunzi inasemekana aligoma kulipa nauli, konda akazuia begi lake la shule. Dogo akaenda kushtaki kwao. Gari wakati inarudi ikasimamishwa na jamaa watatu waliovaa kiraia wakiwa na yule dogo, gari iliposimama wale jamaa wakamwambia dereva tunashida na konda wako. Konda akamkambidhi hela dereva na kuondoka na wale jamaa.

Dereva akapeleka abiria na kuwasiliana na tajiri wa gari. Tajiri akaripoti polisi, polisi wakaenda kambini, kufika, wanaambiwa mtu kapelekwa hospitali, kufika hospitali wanaambiwa mtu wenu ameshakufa.

MyTake: Jenerali Mwamunyange wasaidie ndugu wa marehemu huyu kuhakikisha afisa aliyetoa amri ya kuteswa kwa konda huyo sheria za kijeshi zinamtia hatiani, ili iwe fundisho kwa wengine.
 
Wakati mwingine watoto hawa sio wazuri sana..hasa wakishajua nafasi za baba zao!

Sasa huyu mwanajeshi kama alitaka mtoto asisumbuliwe si angemnunulia kagari..au alitaka apande bure yeye na pia familia yake ipande bure?

Ni jambo la kijinga sana kuchukua maelezo ya hawa watoto wetu wa kileo na kwenda kumpotezea mtu uhai wake!
 
Duh!!!,Sasa nimeamini ule Usemi usemao "Mjinga mpe cheo/madaraka",Yaani sijui ni ujinga wa namna gani Kumpotezea Uhai mwenzako eti kisa umesikiliza malalamiko ya Mwanao.Hivi km watoto wa hao Wanajeshi ni Wanafunzi hao Walimu si wana Kibarua kigumu kweli???!!!,Lkn kwa huu Uonezi Mungu mwenyewe atawalipa tu.Ndio maana haya majamaa hata yakistaafu pamoja na kulipwa Mkwanja mrefu lkn Maisha yao huwa yanakuwa ovyo sababu ni Manung'uniko ya watu.
 
Siku hizi watoto hawa hawajui in adhabu gani za kumpa raia asikusahau,matokeo yake wanaingiza na mihemko huko, yanawatokea puani.

Umeishawahi kushuhudia mtu anamwagilia miti ya miembe mpaka ialike maua???
Saa ngapi watajulikana kwamba wao ni wanajeshi?Wajue tu si kwamba raia hawawezi kuwapiga na wao,ukizingatia wengi wao wanaishi uraiani,ni tunaheshimu utawala wa sheria.Mwanajeshi mwenye maadili mema ya kijeshi hawazi kupiga raia.
 
Duh!!!,Sasa nimeamini ule Usemi usemao "Mjinga mpe cheo/madaraka",Yaani sijui ni ujinga wa namna gani Kumpotezea Uhai mwenzako eti kisa umesikiliza malalamiko ya Mwanao.Hivi km watoto wa hao Wanajeshi ni Wanafunzi hao Walimu si wana Kibarua kigumu kweli???!!!,Lkn kwa huu Uonezi Mungu mwenyewe atawalipa tu.Ndio maana haya majamaa hata yakistaafu pamoja na kulipwa Mkwanja mrefu lkn Maisha yao huwa yanakuwa ovyo sababu ni Manung'uniko ya watu.
Kweli kabisa aisee..
 
Back
Top Bottom