Kipi muhimu: Madawati na vitabu au vitambulisho

Nani wanakaa chini bila madawati??jibu watoo wa walalahoi....wao waoo wao wanasoma Kimombo Medium Schools na wengine nje ya Nchi.TUITION fee zinatoka hapo hapo kwenye vitambulisha
 
Ahh, na nyie mnaoleta hizi thread za kulalamikia dalili badala ya ugonjwa wenyewe, nanyi pia tumewachoka. Mfumo wa utawala wa nchi yetu umejengwa ktk misingi ya kukidhi haja za genge la watawala. Pindi tutakapoikomboa nchi kutoka kwa genge la watawala ndipo tutakapoeza kweli kutatua matatizo yetu objectively.
 
kipi kipewe umuhimu au kipaumbele cha kwanza inategemea wewe ni nani, unaamini nini na unasimamia nini bila kusahau wakati ulionao.

wewe ni mwananchi.....
kwa maana halisi ya neno mwananchi yaani mzalendo....kipaumbele kinaweza kuwa elimu na mengine baadae...maana unaamini kuwa elimu ni msingi wa mafanikio ya kila taifa...taifa lenye utapiamlo wa elimu hata kama kila mzawa atapewa kitambulisho cha utaifa ni bure kabisa...

wewe ni mlanchi....
mfano wa wala nchi ni wanasiasa....kipaumbele kitakuwa ni lile lenye maslahi ya kisiasa...kama ni mwaka 2010, mwaka wa uchaguzi, lile litakalorahisisha mchakato wa wewe kurudi kwenye utukufu ili uendelee kula nchi...hilo ndilo litakuwa na umuhimu wa kwanza....kwa mantiki hiyo inawezekana kwa kuzingatia wakati, vitambulisho ni muhimu zaidi....si kwa sababu wananchi wanavihitaji sana laa....uchaguzi unakuja na pesa zitahitajika ili watawala waweze kurudi madarakani...wafanyeje....pitisha dili la vitambulisho...kamata chako...ingiza kwenye uchaguzi...ukirudi madrakani utajipanga jinsi ya kurudisha kila senti uliyoitumia si kwenye hazina laa...mfukoni mwako...

inakatisha tamaa lakini mtandao umeshai-shape political landscape ya nchi....nasikitika sioni mwangaza mbele labda baada ya 2025 Lowasa atakapokuwa anamaliza muda wake wa uraisi....

amesema kweli aliyesema...Tanzania ni zaidi ya uijuavyo.......
 
Vyote ni muhimu. Umuhimu wa kimoja sio sababu ya kuzuia kingine kisipatikane. Huwezi kusema tuache kupata Vitamini kwa sababu Protini ni muhimu kuliko Vitamini. Ili tujenge taifa la kisasa lazima kila mtu atambulike - alipe kodi, asiwe mzururaji na awe na shughuli rasmi!
 
Ahh, na nyie mnaoleta hizi thread za kulalamikia dalili badala ya ugonjwa wenyewe, nanyi pia tumewachoka. Mfumo wa utawala wa nchi yetu umejengwa ktk misingi ya kukidhi haja za genge la watawala. Pindi tutakapoikomboa nchi kutoka kwa genge la watawala ndipo tutakapoeza kweli kutatua matatizo yetu objectively.

Baada ya kuwatoa watawala waliopo (genge) mtachagua genge lingine ..hivyo tutakuwa na na kazi moja tu kutoa genge moja baada ya lingine..mhh!
 
Back
Top Bottom