Kipi kinachotushaua kushereheka na mwaka mpya ?

Judgement

JF-Expert Member
Nov 13, 2011
10,327
4,779
JF membars ! Hembu fungukeni mlione hili, kwamba kila NUKTA
SEKUNDE
DAKIKA
ROBO SAA
NUSU SAA
SIKU
WIKI
MWEZI
MWAKA
MUONGO (DECADE).
Zinavyosogea mbele au kupita viumbe vyote vilivyo katika uso wa dunia huongezeka umri. Na hakuna ubishi kila kiumbe kina muda mahsusi wa kuwepo duniani.
Iwe Binadamu, Ndege, Samaki, Miti, wadudu e.t.c Ndiyo kusema kila Nukta ipitayo inamsogeza binadamu katika kumuweka kua MAITI au MAREHEMU MTARAJIWA !
Mwaka wa jana ulikua na miaka 20, mwaka ujao 21, mwaka utakaofata 22! Ni kwenda mbele tu hiyo ndiyo KANUNI.
Miaka haitoki 80 kurudi nyuma!, kuna binadamu atakaeishi miaka 200 ?.
Hapa ndipo kwenye KUSUDIO langu la kimsingi, hivi inakuajekuaje tusheherekee MAPITIO YA KWENDEA KUFA ? nisengekua na hoja kama ingekua tunazaliwa na umri mkubwa then umri unarudi nyuma kisha tunarejea matumboni na kisha tunazaliwa upya!
Mafataki, Fashifashi, Shampeni, Choma matairi, Mapati makubwamakubwa yanahusu katika hili ?.
Nini mantiki na faida ya Kushereheka ukirejea kwa niliyoyaainisha hapo juu ? Fungukeni mnipe maoni yenu nini mitazamo yenu mkizingatia nyinyi ni GRETI SINKA.
 
Kwahiyo kila siku inaposogea tuwetunaomboleza? Yaani bado sijapata lengo la maelezo yako.
 
kwa kweli hilo ni neno mkuu judgement! hata mi mwenyewe nakuwaga na mawazo kama hayo, hasa hivi sasa niwakumbukapo marehemu ambao hawakubahatika kuuona mwaka huu mpya wa 2012 tunaousheherekea, japo tulisheherekea pamoja kuukaribisha mwaka uliopita wa 2011 ....,
 
Kwahiyo kila siku inaposogea tuwetunaomboleza? Yaani bado sijapata lengo la maelezo yako.

Mh. Devine ! Sina maana hiyooo! Maana yangu ni instead of KUSHEHEREKEA ni vema tukaifanya sikukuu hii iwe ya binadamu kujifanyia TAFAKARI (counter check) kwamba umefanya yapi na yepi katika uliokua umeyakusudia ndani ya mwaka unaoumaliza, wapi ulikwama na nini ukifanye usikwame tena! Pale ulipofanikiwa uongeze ufanisi.
Kwa wale wenye imani na dini zao WATAFAKARI ni kipi walichokifanya kibaya kisichokubalika na imani zao kisha watubu kuyajutia hayo SALA na MAOMBI vikachukua nafasi nafsini mwao.
 
mnh hapo umeniweka sawa sasa.
 
watu hawasheherekei kuingia mwaka mpya
watu wanasherehekea kumaliza mwaka salama....
 
watu hawasheherekei kuingia mwaka mpya
watu wanasherehekea kumaliza mwaka salama....

Sherehekea kumaliza mwaka salama! Mwaka jana age 25 ! Mwaka huu 26 then 27- 40- 50- 70- 90 - ( 100 shughuli kufika huku) naheshimu maneno yako, but mimi nitaendele kusheherekea kwa kutafakari, si kwa kurusha fataki.
 
Back
Top Bottom