Kipi kimekupita

moreen baby

Senior Member
Joined
Feb 20, 2014
Posts
127
Reaction score
23
Haya Mambo Huwezi Kuwa Umepitia kama Umezaliwa Baada ya Mwaka 90's...

1. Kupakwa GV kwenye kidonda
2. Kung'olewa jino kwa uzi
3. Ubwabwa kupikwa j2 tu
4. Kidonda kuwekwa unga wa 'rangi mbili' a.k.a tetesakrin
5. Kupamba kadi na pamba sebuleni
6. Ukumbi wa sherehe kupambwa kwa toilet paper
7. Kunyolewa na mkasi
8. Kufunga pesa kwenye leso au pindo la kanga
9. Wavulana Kuvaa Nguo ya ndani aina moja nchi nzima VIP, usiombe ikakatika ukakuta imebana Kifua.
10. Ku rewind kanda kwa peni
11. Nchi nzima Kuangalia Movie ya Commando John, Double Impact, Rambo na Bluce Lee..
12. Watoto Wa Mtaa Mzima Kufahamiana sababu ya kucheza Wote Jioni Kombolela na Kibaba..
13. Kuunguzana na tunda ya Ubuyu baada ya kuisugua chini
14. Kukata ndala, ati ni kifutio
15. Kunyolewa msalaba shuleni kisa nywele ndefu
16. Kuweka Vibox box kwenye Shati la shule Mgongoni..
17. Kuweka Shati la Shule "Blue" eti liwe zuri.
18. Ubitoz Ulikuwa ni Kusimamisha Kora Ya Shati.
19. Ukiandika Barua kwa Umpendae lazima uchore moyo na Mkuki na lazima upulizie Pafyumu ya "YU".
20. Hata kama Mlikuwa mmegombana January lakini Mtu anakuambia "Utaipata Siku Ya Kufunga Shule".

Je wewe unakumbuka nini??
 
Ha ha ha.... Ila hiyo y 3 kwetu hy haikuwepo, zmenikumbusha mbali sana.
 
Kula wali then unaacha kipunje shavuni unauliza watoto wenzio leo tumekula nn?
 
Daaah nmekumbuka vingi ila kitu cha kombolela ni noumeer
 
 
Marufuku kumuonesha mwenzio kaburi/makaburi kwa kunyoosha kidole, et utakufa nawe.
daaah!
 

#17 . Imenikumbusha kuweka blue kwenye socks siku ya kwenda kupiga passport shuleni
 
Naomba 7 imenikumbusha mbaaali sana
 
Kuvaa soks za punda milia alafu unapandisha mpk magotini
 
Mkuu umesahau kupoteza soksi moja afu iliyobaki unakata vipande viwili siku zinasonga aaaaaaaaa

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 
Nimecheka sana aseee duhhhh ilikuwaga rahaa kwel.
 
Duh, nakumbuka mengi sana. Beringi, mchezo wa ringi, kusukuma matairi, kuwinda kware...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…