Kipi bora?naomba ushauri?

malifimbo

Senior Member
Joined
Apr 2, 2013
Posts
129
Reaction score
32
Habari wana jf.mm mwezi huu wiki iliyo pita niliomba nafasi ya kufundisha secondary shule flani yombo-buza ilikuwa siku ya jmosi nikafanya interview nikapita na nikapewa barua ya kazi ya mshahara 300000 kwa mwez kama probation time for months then nipate mkataba wa 2year.
Na mimi ninakaa tabata segerea nauli kwenda na kurudi kwa siku ni 2000 na 60000 kwa mwezi bila chakula.
na kwa sasa sina nauli hiyo ya kwendea huko kutokana na uwezo wangu sina.
huku nasubiri nianze kazi trh 14.1.2014 kuna sehemu nikapeleka CV yangu college flani ya walimu hapa kariakoo.nikaongea na mkuu wa chuo kasema nifundishe computer na kaniambia itanilipa 10000 perday na 50000 kwa siku tano perweek na 200000 per month.Nauli ni 1000 kwa siku na 20000 kwa mwez chakula nakula hapohapo.SASA JE WANAJAMII NIENDE WAPI NA NIACHE WAPI
ASANTENI
 
Ni bora uwende utakapo pewa mkataba kuliko kufanya kazi kama kibarua.
 
Fanya kazi ya Mkataba,
Kibarua unaweza kuanza wiki hii kisha akaja ndugu yake yupo chuo akakutoa.
 
Usiende kote,endelea kulala tu mtoto mzuri.
 
Nenda kwenye mkataba kaka usiangalie pesa za kila week cha msingi kopa kwa mtu pesa ya nauli kwa wiki hasa au ongea na huyo mkuu upewe hata pesa ya kutanguliza ya msaada kaka
 
Fanya cost benefits analysis, nenda kariakoo.

Jitume kufanya kazi na ushinikize upewe mkataba.

wanakupoteza tu hao
 
fuata mkataba na mda utakavyoenda waweza pata hata chumba maeneo ya karibu, hivyo cost ya nauli itapungua
 
Habari. Riziki anapanga Mungu, uamuzi na uchaguzi unao mwenyewe. Ushauri wangu fanya kazi unayoipenda, kama ni computa au ni kushika chaki. unapofanya kazi unayoipenda, faida zake ni kua hutaichoka kazi na utafanya kwa moyo na kwa juhudi, hii itampelekea mwajiri wako kukupenda na kukupa mshahara mzuri. Ushauri wangu mwingine ni muwa, fanya kazi kwa lengo ya kumfurahisha mwajiri wako na sio kwa kutaka mshahara, unapofanya kazi vizuri, mshahara mzuri utakuja tu mwenyewe. Mungu akujaze uvumilivu. ASANTE
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…