Hahaha. Chill bro. Nimemaanisha hawajavuka nje ya Bongo. Kigamboni si nje pia?
Ndio maskani nini?
nikweli kabisa,sio drugs tu atarudi akiwa hana upendo na babaake yeye ni marafiki zake tu wa states tena kama Huyo ndugu atakua amepigika ndio atamzarau kabisa,mtoto mlee ktk njia impasayo akiw MTU mzmima umpeleke sasa states mana pia hujui atapa uangalizi gani huko kama anauwezo wa kimtunza mwanae amtunze asije akampoteza akiwa bado haiwatu tunadhani marekani ndo kila kitu. Ataporudi hapa ana abuse drugs ndo mtaelewa, america is the worst place to rase a black child
Hahaha. Sio kwamba Bongo ni pabaya, jamaa ana uwezo wa kumnunulia mwamvuli na ice cream kupunguza makali pia.
Mi Mkojani, ukitaja Kigamboni unanigusa kabisaa!
Inshort, Nitamlea Mwanangu Tuu MkuuJamaa ana mtoto wa kike, umri kama miaka mi-4 sasa. Hajaoa, wala hana mawasiliano na mama wa mtoto(Tuyaachie hapo tafadhali). Mtoto anaishi na wazazi wa jamaa. Jamaa anamuona mwanae mara kwa mara, na anajitahidi kuwa baba bora.
Ana kaka yake wa damu anayeishi na kufanya kazi America, ni marafiki wazuri pia. Anapofanyia kazi kaka yake, wanatoa benefits mbali mbali kama za matibabu, elimu, n.k. kwa wafanyakazi pamoja na familia zao. Kaka hajaoa, wala hana mtoto, anaishi na mpenzi. Katika maongezi, Kaka amependekeza jamaa ampeleke mwanae ili akafaidike na hizo benefits pamoja na mambo mengine. Jamaa kamuambia kaka yake ampe muda kidogo ili afikirie.
Jamaa ana uwezo wa kumtunza mwanae(fedha sio tatizo), na angependa pia wawe karibu ili kutengeneza bond baina yao. Ila pia, elimu na exposure atakayopata America ni tofauti sana, isipokuwa jamaa atakuwa na muda/uwezo wa kuwa na binti yake angalau mara 3 kwa mwaka.
Vaa viatu vya jamaa, unadhani kipi ni bora kwa huyu mtoto? Karibu.
aah hata ice cream za bongo plus mwamvuli bado banah... btw mtoto anaishi kwa grands wake, means malezi ya baba bado hayapati hata akiwa hapa so its beta akaenda huko tu!!! jus saying
I think He better let the kid go,I know he wants to be a good father but the child need that exposure atakua kiakili na kutopenda kuwa tegemezi jamii zetu nyingi za Afrika watoto wanakua na akili tegemezi kweli knowing dad is there,grandmom or grandpops na ndugu wengine lakini kuwa nje ya nchi kunabadilisha sana najifananishia mimi mwenyewe before na after. Ni mtazamo wangu.
Na hapa ndiko kwenye point yote!!!!
Amwache mtoto aende mamtoni bana...exposure ni kitu ingine ati!!!
Ningelikuwa mimi, mwanangu namlea mimi mwenyewe haijalishi maisha yangu yakoje. Mtoto anahitaji malezi ya mzazi mwenyewe angalau kwa miaka kumi ya mwanzo. Pamoja na kwamba huyo ni kaka yake, anauhakika gani na malezi atakayopewa mtoto.....!? Dunia ya leo imeota meno, anaweza kuwa ndugu yako wa damu lakini bado akamnyanyasa mwanao.