Roger Sterling
JF-Expert Member
- May 10, 2015
- 13,010
- 23,653
Jamaa ana mtoto wa kike, umri kama miaka mi-4 sasa. Hajaoa, wala hana mawasiliano na mama wa mtoto(Tuyaachie hapo tafadhali). Mtoto anaishi na wazazi wa jamaa. Jamaa anamuona mwanae mara kwa mara, na anajitahidi kuwa baba bora.
Ana kaka yake wa damu anayeishi na kufanya kazi America, ni marafiki wazuri pia. Anapofanyia kazi kaka yake, wanatoa benefits mbali mbali kama za matibabu, elimu, n.k. kwa wafanyakazi pamoja na familia zao. Kaka hajaoa, wala hana mtoto, anaishi na mpenzi. Katika maongezi, Kaka amependekeza jamaa ampeleke mwanae ili akafaidike na hizo benefits pamoja na mambo mengine. Jamaa kamuambia kaka yake ampe muda kidogo ili afikirie.
Jamaa ana uwezo wa kumtunza mwanae(fedha sio tatizo), na angependa pia wawe karibu ili kutengeneza bond baina yao. Ila pia, elimu na exposure atakayopata America ni tofauti sana, isipokuwa jamaa atakuwa na muda/uwezo wa kuwa na binti yake angalau mara 3 kwa mwaka.
Vaa viatu vya jamaa, unadhani kipi ni bora kwa huyu mtoto? Karibu.