Kipi bora kati ya Mbio za Mwenge na Muungano?

makoye2009

JF-Expert Member
Jun 12, 2009
2,638
1,218
Nategemea Rais wangu JPM atasoma thread hii maana najua ni mtu anayejishughulisha na mitandao ya kijamii na media zinazogusa maisha ya Mtanzania kama tulivoshuhudia hivi karibuni Rais alipopiga simu kituo kimoja cha redio.

Kwanza nimpongeze kwa juhudi za kubana matumizi na sera ya utumbuaji majipu.Hoja yangu ni huu utaratibu wa kubana matumizi kwenye vitu vya msingi na hiyo fedha kupelekwa kwenye vitu visivyo muhimu. Sherehe za Kitaifa kama siku ya Uhuru(9/12) na siku ya Muungano(26/4) zote zimeainishwa kwenye Katiba na sheria lakini kwenye A5 zinaonekana hazina maana!

Tangu mheshimiwa JPM aingie madarakani tumeona akifuta sherehe za Uhuru 9/12/2015 na kuamru watu wafanye usafi na fedha iliyo okolewa ikipelekwa kwenye kujenga barabara za lami.

Kama hiyo haitoshi keshokutwa tena hatutakuwa na sherehe za Muungano 26/4/2016 na badala yake watu watapumzika majumbani na fedha hiyo itaelekezwa kwenye matumizi mengine ya lazima!

Sikukuu hizi ni muhimu na zinatukumbusha matukio muhimu za kitaifa kama siku ya kupata Uhuru na kujitawala toka kwa mkolone! Sherehe za Muungano ni kuonyesha umuhimu wa kuunganika kwa Tanganyika na Zanzibar kuwa nchi moja ya Tanzania!

Kufuta sherehe hizi muhimu ni kutowatendea haki Watanzania wa pande zote mbili kwa maana ya Bara na Visiwani.Lakini pia ni kutowatendea haki waasisi wa taifa letu Nyerere na Karume. Sidhani na siamini kama Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere na Amani Karume kama wangekuwa hai wangekubaliana na kile anachofanya JPM!

Juzi tumeshuhudia Uzinduzi wa mbio za Mwenge kule Morogoro kwa mbwembwe na bashasha nyingi. Najua hapa kuna mamilioni ya Fedha yameteketea na yataendelea kuteketea mpaka siku ya kuzima hilo li mwenge ambalo kwa hakika huwa sioni tija yake kwa Watanzania.

Kama swala ni kubana matumizi kwa kufuta vitu visivyo na faida kuna haja gani ya kuendelea na mbio za Mwenge kwa hii A5? Mwenge unaingiza kiasi gani cha fedha iwe ni kodi au michango?

Sifa ya mwenge sana ninayoijua ni kueneza ufusika, ngono na uasherati na mwisho wake UKIMWI! Watu wamekuwa wakishuhudia ndoo na ndoo za mipira ya kiume na ya kike(condoms) zikikusanywa pale Mwenge unapokesha/kulala!

Hii siyo sifa wala picha nzuri ya Mwenge. Ni bora kusitisha mbio za Mwenge na kuruhusu watu wakasherehekea siku za kupata Uhuru au siku ya Muungano kwani muhimu kuliko Mwenge.

Nawasilisha.
 
Nilitarajia kabisa mbio za mwenge ama zingedutwa kabisa au zingefanyika kimkoa. Ni upotezaji muda na rasilimali. Mafuta ya magari pamoja na posho na manunuzi yasiyofuta taratibu za manunuzi
 
Back
Top Bottom