Stroke
JF-Expert Member
- Feb 17, 2012
- 40,225
- 51,471
Matokeo ya hivi karibuni ya kidato cha nne kimezua maswali mengi moja wapo likiwa hili kama kichwa cha habari kinavyoonesha.
Elimu bure ilikua sera ya vyama vyote vilivyoomba ridhaa ya kushika dola 2015.
Sote tumeona namna gani serikali ya awamu ya tano jinsi ilivyojitahidi kutimiza ahadi hiyo kwa haraka kwa kuanza kutoa elimu bure.
Jambo la kushangaza ni baadhi ya wadau wa elimu kuanza kuponda sera ya elimu bure kua ni chanzo cha kushuka ufaulu.
Mshangao huo unazidi pale ninapovuta kumbukumbu kua ni watu wale wale ambao walikua wakiikosoa serikali kua pamoja na kua na rasilimali za kutosha bado imeshindwa kutoa elimu ya bure, ndio hao hao leo wanaoiponga tena sera hiyo.
Sioni uhisoano wa moja kwa moja wa sera ya elimu bure na matokeo ya hivi punde ya kidato cha nne. matokeo ni yale ambayo yamekuja kabla ya sera kuanza. hivyo sio sahihi kuipinga sera hiyo kwa kipimo cha matokeo hayo.
Vile vile sio sahihi kusema kwamba kwakua shule flani wanalipa ada kubwa na kwakua huduma zote zipo ukilinganisha na shule nyingine hivyo ufaulu utakua mkubwa hoja hiyo haina mashiko kwani hata katika matokeo haya tumeona ni kwa namna gani baadhi ya wanafunzo wamefanya vyema tu hatakama wametoka kwenye mazingira magumu.
Mimi nashauri tuipime hii sera kwa kuangalia matokeo yajayo kuliko kuipima sasa wakati ni hivi majuzi tu imeanza kutekelezeka.
Swali langu ni hili;
Je, ni kweli kwamba sera ya elimu bure haifai na inadidimiza elimu?
Je, ni kweli kwamba kuchangia elimu kunapelekea kupatikana kwa elimu bora hivyo kuongeza ufaulu?
Nategemea kusikia mengi toka kwenu wanajamvi.