Heart Wood.
JF-Expert Member
- Nov 16, 2014
- 972
- 1,150
Bila shaka Mungu anaendelea kuyahudumia maisha yako, anaendelea kujihusisha na Maisha yako na Familia yako, pamoja na ndugu na Rafiki zako, kwa sababu ndiye aliyetuumba. Kama ndiye aliyetuumba, hakika ni katika yeye ndipo tunafahamu kusudio la Maisha yetu hapa Duniani. Kama hutambui kuwa Mungu ni sababu ya Maisha yako mpaka sasa, basi Maisha yako hayatakuwa na maana yoyote, kwa maana, yote huanza na YEYE kwa sababu ndiye aliye Asili ya mambo yote.
Bila shaka umeweka Mipango mingi tunapouanza Mwaka huu mpya, 2017. Bila shaka umeweka mikakati mbalimbali ili kufikia mafanikio ya mipango yako. Pamoja na hayo, imenipasa kukushirikisha mambo machache ninayodhani yanaweza kukusaidia katika siku zako za Uhai zilizobaki hapa Duniani.
Kwanza kabisa, imetupasa kutambua kuwa, Maisha ya hapa Duniani ni mafupi ukilinganisha na yale tutakayoyaishi baada ya kifo cha Mwili, naam, ni pale roho itakapotengana na miili hii tuliyonayo, ambapo huitwa “kufariki”. Biblia inasema maisha ya hapa Duniani yapata miaka Sabini na ikiwa tuna nguvu ni miaka Themanini (Zab 90: 10), Lakini, maisha ya Mbinguni kwa wafanyao mapenzi ya Mungu imeahidiwa maisha ya umiilele( 1Yoh 2: 17), Lakini, pamoja na hayo,cha kushangaza ni kwamba, tumeyapenda zaidi maisha ya Dunia hii kuliko yale ya Mbinguni bila shaka hii ni kutokana na ufahamu wetu kutiwa upofu (2Wakor 4:4), Laiti kama fahamu zetu zisingekuwa zimetiwa upofu, katika hali ya kawaida tu, ukiambiwa uchague maisha ya milele na maisha ya miaka 80, bila kusita utachagua maisha ya umilele kuliko haya ya miaka 80 yaliyo mafupi sana. Biblia iansema “Msiipende Dunia wala mambo yaliyomo katika dunia. Mtu akiipenda Dunia, kumpenda Baba hakumo ndani yake. Maana kila kilichomo duniani, yaani, tamaa ya mwili, na tamaa ya macho, na kiburi cha uzima, havitokani na Baba, bali vyatokana na dunia, Na dunia inapita, pamoja na tamaa zake….”( 1Yoh 2: 15 - 17)
Ili kujihakikishia maisha ya Mbinguni, tiketi na kipimo chake kinapatina hapa Duniani, jinsi tunavyoishi, jinsi tunavohusiana na Mungu pamoja na wanadamu.
MWAKA 2017 UWE WA KUENENDA SAWASAWA NA NENO LA MUNGU
Kuishi sawasawa na Neno la Mungu ni tiketi namba moja ya kuyafikia maisha ya milele, Neno la Mungu ndiyo ushindi wa maisha yetu (Mathayo 4: 4).
Imetupasa kutambua kuwa, Kujifunza Neno la Mungu, Kumwabudu Mungu, na kuishi sawasawa na Neno lake si jambo la hiari, na kuwekwa kama jambo la ziada baada ya kukamilisha ratiba zetu za Kila siku, bali ni kiini cha maisha yetu. Imetupasa kulitafakari neno la Mungu kila wakati,usiku na mchana, tuwapo safarini, tuwapo Ofisini, tuwapo shambani, tukutanapo na rafiki na ndugu zetu nyakati za mapumziko, tuwapo katika kusanyiko la Watu wengi n.k,
MWAKA 2017 UWE WA KUKUA KIROHO
Ili ukue Kiroho, lazima ukubali kuwa tofauti na mambo ya Ulimwengu huu, lazima ukubali mabadiliko katika ratiba za Maisha yako, mtindo wa kuishi na namna nyingine za Dunia hii, lazima ukubali kupoteza baadhi ya mambo unayofikiri ni muhimu katika hii Dunia na mengine mengi ya mtindo wa Dunia hii, hauwezi kutaka kufikia viwango wa juu kiroho bila kuruhusu mabadiliko katika mfumo mzima wa maisha yako, ukisema unakua kiroho, huku hakuna mabadiliko kati ya mfumo wa maisha yako ya zamani na ya sasa, huko si kukua, ni kuendelea kudumaa. Kwa muda mwingi, yawezekana kabisa kuwa tangia kuzaliwa kwako, umeujaza ufahamu wako kwa mambo yasiyo ya msingi, mambo yasiyofaa na yenye kusababisha Matengano kati yako na Mungu, kukua Kiroho ni pamoja na kukubali kuondoa ufahamu danganyifu wa Kidunia na kuujaza ufahamu wako kwa kweli ya Mungu kupitia Neno lake. Lazima ufanye mabadiliko ya kile unachokisikiliza na kukitazama, lazima ukubali kuchagua maneno ya kuzungumza, lazima ukubali kubadilisha maeneo ya kutembelea na watu wa kukutana nao, n.k
MWAKA 2017 UWE WA KUJIHUSISHA NA NENO LA MUNGU KWA KIASI KIKUBWA ZAIDI
Imetupasa kufanya bidii zaidi kuutafuta Ufalme wa Mungu kuliko mambo mengine, tukiupata Ufalme wa Mungu, Mahitaji yetu mengine kama Wanadamu hapa Duniani, Mungu atayafanikisha(Mathayo 6: 33), kwa sababu Biblia inasema “Ayang’ang’aniaye maisha yake atayapoteza, lakini yeye atakayeyatoa maisha yake kwa ajili yangu atayaona.” (Mathayo 10:39) Neno linaendelea kusema; “.Kwa maana itamfaidia nini mtu kuupata ulimwengu wote, lakini akayapoteza maisha yake?(Mathayo 16: 26). Itakufaa nini kuwa tajiri mkubwa mwenye magari na majumba lakini uukose Ufalme wa Mungu.? ( ieleweke kuwa hapa simaanishi kuupinga utajiri ule wa haki, bali ule usio wa haki).
Kama umepanga kuweka bidii zaidi za mafanikio yako kiuchumi kwa Mwaka 2017, basi bidii yako ya kufanikiwa katika maisha ya kiroho iwe mara kumi zaidi ya nguvu na mikakati uliyopanga kufanikiwa kiuchumi, kumuomba Mungu isiwe sehemu ya ratiba ya maisha yako, bali iwe uhalisia, utamaduni, mtindo na tabia ya maisha yako ya kila siku. Neno la Mungu linasema, (Mathayo 22:37 - 38).Yesu akamjibu, “‘Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote na kwa roho yako yote na kwa akili zako zote.’” Hii ndio amri iliyo kuu, tena ni ya kwanza
Huwezi kumpenda Mungu kwa moyo wako wote kama hupati muda wa kuzungumza naye kupitia SALA mara kwa mara, huwezi kumpenda Mungu kwa moyo wako wote kama hupati muda wa kusoma na kujifunza neno lake. Kama umepanga kusoma vitabu vya jinsi ya kufanikiwa kiuchumi, kisiasa, mahusiano au vinginevyo katika maisha yako kwa mwaka 2017 mara mbili kwa siku, basi kusoma Neno la Mungu iwe mara kumi zaidi. Huo ndio msingi wa kufanikiwa, hatumtumii Mungu ili kufanikisha mipango ya maisha yetu pekee, bali kumruhusu Mungu atutumie kwa mujibu wa kusudio la kuumbwa kwetu, maana yeye alitujua tangu tukiwa tumboni mwa mama zetu, hivyo anatufahamu zaidi kuliko tunavyomfahamu yeye, kama yupo anayetufahamu zaidi na yeye ndiye chanzo cha Maisha yetu, kwa nini kusumbuka kwa fahamu na akili zetu wenyewe na kukataa kumuhusisha yeye atujuaye kwa kila kitu?
Heri na Fanaka za Mwaka 2017 ziwe za kudumu katika Maisha yako, Mungu akubariki na kukushindia katika yote.