Kipanya sio balaa bali viongozi wengi wanafanyakazi kwa kumuogopa asiwatumbue. Kuna kesi ilipelekwa mahakamani na PPF dhidi ya ATCL kuhusu mafao ya wastaafu kutokana na kampuni kutopeleka makato ya michango yao walipokuwa kazini. Mahakama iliamuru mali za ATCL zikamatwe na kuuzwa ili kuwalipa wazee wastaafu. Wizara ya U. U.Mawasiliano, na Wizara ya fedha waliahidi kulipa ili mali za ATCL zisikamatwe. Hadi sasa hawajalipa kwa kumuogopa raisi eti alikataza malipo ya aina hiyo siku alipofungua jengo la PPF pale Arusha. Ni kweli mawaziri na viongozi wanamuogopa sana mkuu. Wanakiuka maagizo ya mahakama kwa kumuogopa mkuu
Nao PPF wajipendekeza kujenga viwanda huku wakikataa kulipa mafao kama sheria za mifuko ya jamii na SSRA zinavyoelekeza. Viongozi wengi sio weledi wa kazi zao kwa kutetea matumbo yao