KIPANGA SHERIA,SHERIA,SHERIA

security guard

JF-Expert Member
Sep 27, 2011
799
603

SHERIA, SHERIA, SHARIA

(Dr. Muhammed Seif Khatib)

Labda tukubaliane kuwa kila jambo huwa na utaratibu wake ili likamilike. Mfano mzuri ni wa taratibu za mchezo wa kabumbu au wengine huiita kandanda, mchezo unaongozwa kwa kupendwa duniani. Una muda wake wa kucheza. Dakika tisini. Una idadi yake ya wachezaji, ishirini na mbili. Wengine husema hata refaa naye ni mchezaji. Unao mwamuzi na wasaidizi wake wawili. Unao muda wa kupumzika. Lakini pia unao sheria zake za kuongoza mchezo huo. Ingawa unaitwa mpira wa miguu, lakini golikipa yeye anaruhusiwa kutumia mikono yake! Ingawa unaitwa mpira wa miguu, lakini mchezaji akitumia kichwa kufunga goli siyo kosa. Lakini lenye uzito zaidi ni kuwa mwamuzi ndiye mwenye kauli ya mwisho akiwa uwanjani. Kwa hali hii, wale wote wanaocheza mchezo huo hutakiwa wafate sheria, kanuni na maamuzi ya mwamuzi. Na kwamba maamuzi yake hayawezi kutenguliwa.

Hayo ndiyo yaliyojiri huko Zanzibar mwaka 2015 mwezi wa Oktoba. Ulikuwepo Uchaguzi Mkuu ambao ulishirikisha vyama vya siasa ambavyo vina usajili wa kudumu. Zipo taratibu za kuendesha uchaguzi unaohusika. Vyama vya siasa na viongozi wake wote waliweka saini kukubali kushiriki katika uchaguzi. Wote walikubaliana kuwa chombo kinachosimamia ni Tume na siyo mtu aitwaye Jecha. Na kwa bahati mbaya ndani ya Tume wamo pia wawakilishi wa vyama vikuu vya siasa vya Zanzibar. Nao wote walikubaliana kuwa Tume ndiyo mwamuzi halali na kwamba uamuzi wake wowote hauwezi kuhojiwa na mtu yeyote au mahakama yeyote. Aidha Tume haitakiwi kuingiliwa na mtu yeyote. Si Sheikh si Askofi. Si Jaji si Rais. Ni Tume huru Tume baada ya kutanabahi kuwa uchaguzi umefanyiwa hujuma, takwimu za kura zimechezewa, wapiga kura hasa Pemba wamenyimwa haki yao ya kupiga kura, ikaamua uchaguzi ufutwe. Baya na kubwa kuliko yote ni kule kwa mgombea wa Rais mmoja kunyakua mamlaka ya Tume ya kujitangazia matokeo yake ya ushindi wa urais. Hili ni kosa kubwa la kijinai ambalo lingeweza kuzua maafa makubwa na kusababisha umwagaji wa damu. Huyu aliyetenda kitendo hiki hapaswi kuacha bila mkono wa sheria kuchukua mkondo wake. Zanzibar hakuna mgogoro na wala hakuna kosa kwa mtu aitwaye Jecha. Uchaguzi umefutwa na chombo halali. Uchaguzi umefutwa na Tume kwa kufata taratibu, kanuni na sheria. Uchaguzi haukufika hatima yake hivyo hakuna mshindi wa Uraia wala hakuna wawakilishi au madiwani. Utaratibu wa kutangaza mshindi wa urais wa Zanzibar unajulikana. Mwenyekiti wa Tume anaweza kwa Jecha au Mazurui, muhimu ni mamlaka siyo jina, nasaba au dini ya mtu. Mwenyekiti hakukamilisha kazi ya kukusanya matokeo halali na kuyatangaza yote. Hivyo hakupata jumla ya kura halali za wagombea wote. Ili mgombea wa urais wa Zanzibar ashinde kihalali yafuatayo yafanyike. Kura halali za wagombea wa urais zikusanywe zijumlishwe, zihakikiwe na baada ya kuridhika, zitamkwe rasmi na Mwenyekiti wa Tume. Atamkwe rasmi nani ameshinda kwa kura ngapi. Hilo bado halikufanyika. Pia aliyetajwa kama ameshinda apewe cheti cha uthibitisho ya ushindi wake. Hakuna aliyetajwa wala aliyepewa cheti cha uthibitisho wa ushindi. Hatua nyingine ingafata kwa aliyeshindwa ni kuwekwa siku maalum ya kuapishwa huyu Rais mteule. Siku hiyo haikuwekwa kwa sababu Jaji hajapewa jina la mgombea aliyeshinda. Hatua ya mwisho ingekuwa Rais Mteule wa Zanzibar kuapishwa hadharani na Jaji Mkuu wa Zanzibar. Nalo hilo halikufanyika kwa vile hakuna mgombea urais aliyetangazwa na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar. Hivi basi kwa kufata taratibu na utawala wa sheria uchaguzi wa Zanzibar haukufika mwisho. Kurejewa siyo kosa, dhambi wala kuvunjwa kifungo chochote cha sheria au Katiba. Urais ni kazi ya heshima. Ikulu ni pahapa patakatifu. Huwezi kukabidhi vitu hivi kwa mtu mmoja kinyume na sheria. Utawala bora ni kufata sheria na taratibu ambazo watu wenyewe wamejiwekea. Watu waungwana na wastaarabu hufata sheria. Rudini Wazanzibar katika uchaguzi ili muwapate viongozi halali akiwemo Rais. Sheria, sheria, sheria!
 
Sasa naelewa kwa nini safari hii hujachaguliwa kwenye wadhifa wowote
Mtu mzima unandika makala ndefu uongo mtupu kuhalalisha ufedhuli WA Jecha
mfano umasema uchaguzi umefutws na tume na siyo Jecha,uongo wa wazi
Mahaba yako kwa Tanganyika yana kupofusha akili
 
Hapa naona huyu Daktari leo kaamua Kusaka Tonge kwa nguvu zote!

Mtunzi wa makala hii anajaribu kufananisha zoezi la uchaguzi Mkuu wa Zanzibar kwamba ni sawa na mpira wa miguu! Kwangu mimi sidhani kama yuko sahihi kufananisha hivyo kwani ni vitu viwili tofauti kabisa. Lakini tuchukulie ya kwamba haya inawezekana kufananisha mpira wa miguu na uchaguzi mkuu. Kinachoshangaza kwa muandishi na inavyoonesha ni kwamba hata huo mchezo wenyewe wa mpira wa miguu (ambao kaufananisha na Uchaguzi Mkuu) basi hauelewi vyema! Katika kuthibitisha hilo ninalolisema basi angalia hapo nilipo highlight katika paragraph yake ya mwanzo ya hii makala yake. Asichoelewa yeye ni kwamba Katika mchezo wa mpira wa miguu wahusika wote (wachezaji pamoja na waamuzi ) basi wanatakiwa wafuate sheria za mpira wa miguu zinavyosema na sio wachezaji pekee hapa! Nitatoa mfano katika hili. Katika sheria za mpira wa mguu basi kama wewe ni mchezaji basi huwezi kuukamata mpira kwa mkono na ukafunga goli! sheria haikuruhusu kufanya hilo. Pia kama wewe ni muamuzi wa mchezo huu basi sheria haikuruhusu wewe kutoa adhabu ya Penalti kwa kosa la corner ball .

Kwa ufupi ni kwamba kwenye mpira wa miguu kila kosa lina maamuzi na adhabu yake inayostahiki! Mchezaji akifanya kosa basi huadhibiwa pale pale uwanjani. Lakini na hata mwamuzi naye akifanya kosa basi kuna vyombo vinavyohusika na waamuzi humuadhibu panaposatahiki! Ni mara nyingi tu tumeshuhudia waamuzi wa mpira wa miguu kufungiwa, na chama cha waamuzi wa mpira, kuchezesha mpira kwa makosa mbali mbali. Huo ndio mpira wa miguu na sheria zake ulivyo. Lakini pia katika sehemu nyengine ambazo nidhamu inapokosekana pia tumeona watazamaji wanapowaadhibu waamuzi wa mpira wa miguu pale pale uwanjani mara tu wanapohisi haki haikutendeka!

Klichotokea katika Uchaguzi wa zanzibar wa Oktoba 2015, ambacho ni kibaya zaidi , ni kwamba kuna wawakilishi tayari wamepewa vyeti vya ushindi kama ni washindi halali wa uchguzi huo kwenye majimbo yao. Kama ukifananisha na mpira wa miguu basi ni kusema tayari Mwamuzi umekubali magoli yaliyofungwa na score board linaonesha 27:27 halafu leo uamue kufuta bao tu bila ya sababu za msingi! Kwa kweli ni hatari .

Daktari huyu anataka kuufananisha mpira wa miguu na Uchaguzi wa Zanzibar wa 2015 . kwa kweli ni hatari iloje katika jamii yetu hii kuwa na Phd holders wanaojaribu kutetea kila kitu! Badala ya kuwa Madaktari wa Falsafa munakuwa hamuna tofauti yoyote na yule Daktari wa muimbaji Khadija Kopa!
 
Hi

hicho kizee naona kinazeeka vibaya hivi hakujui kusoma alama za nyakati nini? Hakujui kuwa Watanzania wa sasa hawadanganyiki? Zanzibar ni koloni la Tanganyika na sasa Jeshi lipo kule huyo Shein anatawala kijeshi na atakuwa dikiteta kuanzia tarehe 20 baada ya uchaguzi haramu ambao utampachika ikulu kwa njia za Wizi baada ya hapo akiapishwa ataanza kamata kamata watu wengi watafungwa, kupigwa kuwa vilema wa kudumu, kubambikiwa kesi nk, Dikiteta mpya yupo njiani kuanza kazi kuanzia siku akiapishwa.
 
Ka
Sasa naelewa kwa nini safari hii hujachaguliwa kwenye wadhifa wowote
Mtu mzima unandika makala ndefu uongo mtupu kuhalalisha ufedhuli WA Jecha
mfano umasema uchaguzi umefutws na tume na siyo Jecha,uongo wa wazi
Mahaba yako kwa Tanganyika yana kupofusha akili
hako kazee kana njaa wamekapa vicent kakaamua kuandika makala pasipo kutafakari kwanza, kanazeeka vibaya kapo busy kuharalisha Udikiteta Zanzibar, siku kikinuka lazima katakuwa ka kwanza kupelekwa The Hague uholanzi kujibu mashitaka kwa uchochezi huu aliouanza sasa.
 
Mahakama ya uhalifu wa kimataifa ifunge kamera zake Zanzibar maana tarehe 20 baada ya uchaguzi haramu na feki kutaanza kamata kamata ya hovyo hovyo, wengi watabambikiwa kesi,Udikiteta utashika kasi ni bora Mahakama ya The Hague wasogee mapema kabsa ikibidi watume mashushu wao mapema waingie Zanzibar kushuhudia kinachoendelea.
 
SHERIA, SHERIA, SHARIA

(Dr. Muhammed Seif Khatib)

Labda tukubaliane kuwa kila jambo huwa na utaratibu wake ili likamilike. Mfano mzuri ni wa taratibu za mchezo wa kabumbu au wengine huiita kandanda, mchezo unaongozwa kwa kupendwa duniani. Una muda wake wa kucheza. Dakika tisini. Una idadi yake ya wachezaji, ishirini na mbili. Wengine husema hata refaa naye ni mchezaji. Unao mwamuzi na wasaidizi wake wawili. Unao muda wa kupumzika. Lakini pia unao sheria zake za kuongoza mchezo huo. Ingawa unaitwa mpira wa miguu, lakini golikipa yeye anaruhusiwa kutumia mikono yake! Ingawa unaitwa mpira wa miguu, lakini mchezaji akitumia kichwa kufunga goli siyo kosa. Lakini lenye uzito zaidi ni kuwa mwamuzi ndiye mwenye kauli ya mwisho akiwa uwanjani. Kwa hali hii, wale wote wanaocheza mchezo huo hutakiwa wafate sheria, kanuni na maamuzi ya mwamuzi. Na kwamba maamuzi yake hayawezi kutenguliwa.

Hayo ndiyo yaliyojiri huko Zanzibar mwaka 2015 mwezi wa Oktoba. Ulikuwepo Uchaguzi Mkuu ambao ulishirikisha vyama vya siasa ambavyo vina usajili wa kudumu. Zipo taratibu za kuendesha uchaguzi unaohusika. Vyama vya siasa na viongozi wake wote waliweka saini kukubali kushiriki katika uchaguzi. Wote walikubaliana kuwa chombo kinachosimamia ni Tume na siyo mtu aitwaye Jecha. Na kwa bahati mbaya ndani ya Tume wamo pia wawakilishi wa vyama vikuu vya siasa vya Zanzibar. Nao wote walikubaliana kuwa Tume ndiyo mwamuzi halali na kwamba uamuzi wake wowote hauwezi kuhojiwa na mtu yeyote au mahakama yeyote. Aidha Tume haitakiwi kuingiliwa na mtu yeyote. Si Sheikh si Askofi. Si Jaji si Rais. Ni Tume huru Tume baada ya kutanabahi kuwa uchaguzi umefanyiwa hujuma, takwimu za kura zimechezewa, wapiga kura hasa Pemba wamenyimwa haki yao ya kupiga kura, ikaamua uchaguzi ufutwe. Baya na kubwa kuliko yote ni kule kwa mgombea wa Rais mmoja kunyakua mamlaka ya Tume ya kujitangazia matokeo yake ya ushindi wa urais. Hili ni kosa kubwa la kijinai ambalo lingeweza kuzua maafa makubwa na kusababisha umwagaji wa damu. Huyu aliyetenda kitendo hiki hapaswi kuacha bila mkono wa sheria kuchukua mkondo wake. Zanzibar hakuna mgogoro na wala hakuna kosa kwa mtu aitwaye Jecha. Uchaguzi umefutwa na chombo halali. Uchaguzi umefutwa na Tume kwa kufata taratibu, kanuni na sheria. Uchaguzi haukufika hatima yake hivyo hakuna mshindi wa Uraia wala hakuna wawakilishi au madiwani. Utaratibu wa kutangaza mshindi wa urais wa Zanzibar unajulikana. Mwenyekiti wa Tume anaweza kwa Jecha au Mazurui, muhimu ni mamlaka siyo jina, nasaba au dini ya mtu. Mwenyekiti hakukamilisha kazi ya kukusanya matokeo halali na kuyatangaza yote. Hivyo hakupata jumla ya kura halali za wagombea wote. Ili mgombea wa urais wa Zanzibar ashinde kihalali yafuatayo yafanyike. Kura halali za wagombea wa urais zikusanywe zijumlishwe, zihakikiwe na baada ya kuridhika, zitamkwe rasmi na Mwenyekiti wa Tume. Atamkwe rasmi nani ameshinda kwa kura ngapi. Hilo bado halikufanyika. Pia aliyetajwa kama ameshinda apewe cheti cha uthibitisho ya ushindi wake. Hakuna aliyetajwa wala aliyepewa cheti cha uthibitisho wa ushindi. Hatua nyingine ingafata kwa aliyeshindwa ni kuwekwa siku maalum ya kuapishwa huyu Rais mteule. Siku hiyo haikuwekwa kwa sababu Jaji hajapewa jina la mgombea aliyeshinda. Hatua ya mwisho ingekuwa Rais Mteule wa Zanzibar kuapishwa hadharani na Jaji Mkuu wa Zanzibar. Nalo hilo halikufanyika kwa vile hakuna mgombea urais aliyetangazwa na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar. Hivi basi kwa kufata taratibu na utawala wa sheria uchaguzi wa Zanzibar haukufika mwisho. Kurejewa siyo kosa, dhambi wala kuvunjwa kifungo chochote cha sheria au Katiba. Urais ni kazi ya heshima. Ikulu ni pahapa patakatifu. Huwezi kukabidhi vitu hivi kwa mtu mmoja kinyume na sheria. Utawala bora ni kufata sheria na taratibu ambazo watu wenyewe wamejiwekea. Watu waungwana na wastaarabu hufata sheria. Rudini Wazanzibar katika uchaguzi ili muwapate viongozi halali akiwemo Rais. Sheria, sheria, sheria!
Kwakutumia mfano wako wa Mpira wa miguu. Mchezaji mmoja akikosewa timu zima inaandhibiwa au mchezaji mwenyewe? Kama kulikuwa na tatizo Pemba kwanini Unguja warudie? Jingine kama tume ni huru na ina mamlaka, kwanini Kikwete na watu wake wanne na Maalim chini ya Mwenyekiti Shein walikuwa wanatafuta suluhu ya huo uchaguzi? Huon walikuwa wanaingilia mamlaka ya tume? Walikuwa wanaenda Ikulu kwa Magufuli kutoa taarifa gani? Hivi mheshimiwa na kusoma kwako kote umeshindwa kujiuliza maswali haya madogo ya chekechea?
 
Back
Top Bottom