Kipande system imehamia Tanzania?

mjanja wa kijiji

JF-Expert Member
Joined
Oct 2, 2018
Posts
1,907
Reaction score
5,069
Kipande System ni mfumo uliokuwepo Kenya kipindi cha ukoloni, ambapo kila mtu mwenye umri wa kuanzia miaka 18 alilazimika kulipa kodi na kuwa na kitambulisho cha kazi ambapo ilikuwa ni lazima utembee nacho popote uendako.

Sasa kwa hapa Tanzania tangu itangazwe kuwa machinga wote wawe na kitambulisho kumekuwepo na tabia ya watendaji wa Kata/ kijiji kulazimisha watu kununua vitambulisho na kuvivaa shingoni hata kama umeajiliwa kwa mama lishe na unalipwa 1000 kwa siku lazima uwe na kitambulisho.

Kwa hiyo nauliza tumerudi kwa mkoloni?
 
Hao watendaji wa chini wasikuaminishe kwamba tumerudi huko,kwa kuwa umeliweka hapa taarifa imefika litafanyiwa kazi na wakubwa wao kwani wanachofanya sio sahihi kabisa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…