GE2025 Kiongozi wa Rastafarians: Tuilinde amani ya Tanzania, vita ikitokea hatuna nchi ya kukimbilia, Tunamuunga mkono Rais Samia

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
1,446
Reaction score
2,093
Hapa ni njaa ndo imezidi na hili joto la Daslam, nilikuwa nawaheshimu sana hawa jamaa nimeamini njaa ni mbaya sana

-----------------
Umoja wa Rastafarians Tanzanian wamefanya matembezi ya amani ndani ya jiji la Mwanza kama njia ya kuenzi na kuhimiza mila, desturi, amani na upendo vigezo ambavyo wamevitaja kuwa urithi mkuu wa Taifa la Tanzania.

Matembezi hayo yalivuta hisia za wakazi wengi wa Mwanza, huku washiriki wakibeba mabango yenye ujumbe wa amani, mshikamano na kutokomeza chuki miongoni mwa Watanzania

Akizungumza na Manara TV, Kuhani Mkuu wa Imani ya Rastafarians Tanzania, Valerian Bagaile Magena, alisisitiza kuwa Tanzania imejengwa juu ya misingi ya amani na upendo misingi ambayo, kwa mujibu wake, haitakiwi kuchezewa wala kuingiliwa na vitendo vya uchochezi

Rastafarians hao wameahidi kuendelea kuwa mabalozi wa amani na maadili mema katika jamii, wakiamini kuwa ni jukumu la kila Mtanzania kulinda na kutunza amani ya nchi kama sehemu ya urithi wa vizazi vya sasa na vijavyo


Your browser is not able to display this video.
 
Mtaendelea kutowaheshimu wengi tu hususani wenye njaa..
Lakini nyie mlioshiba achaneni nao wenye njaa
 
Hawa wapumbavu wenu mkae nao huko huko
 
Rasta wa kwanza mpumbavu,Marasta huwa ni watetezi wa haki,
Huyo ni mvuta bangi
 
Rasta wa kwanza mpumbavu,Marasta huwa ni watetezi wa haki,
Huyo ni mvuta bangi
Ila angesimama akaponda jambo fulani kwa muondoko wa Captain Tesha kesho ungesikia Rasta ametekwa amepotea mazima na Butika angeinuka kesema sio Rasta huyo ni mvuta bange amethibetishwa na DCEA kuna mahali hua analima bange
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…