Kiongozi wa Kijeshi wa Sudan awatimua mabalozi waliopinga mapinduzi

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,500
9,279
Kiongozi wa Kijeshi wa Sudan Abdel-Fattah al-Burhan amewafuta kazi mabalozi karibu sita waliokosoa mapinduzi ya kijeshi. Mabalozi wa Sudan nchini Marekani, Umoja wa Ulaya na Ufaransa walitangaza wiki hii kuunga mkono serikali iliyopinduliwa ya Waziri Mkuu Abdalla Hamdok na kulaani mapinduzi.

Wengine waliotimuliwa ni mabalozi katika nchi za Qatar, China na Umoja wa Mataifa mjini Geneva. Wakati huohuo wanadiplomasia wa kigeni wamekutana na waziri mkuu aliyepinduliwa Abdalla Hamdok mjini Khartoum.

Katika taarifa ya pamoja walioitoa kupitia Twitter, wanadiplomasia hao wamesema kuwa kiongozi huyo yuko katika afya njema na kwamba wanaendelea kutoa wito wa kurejeshewa uhuru wake. Taarifa kutoka nchini humo zinasema kuwa waandamanaji saba wameuawa tangu jeshi lilipofanya mapinduzi siku nne zilizopita.

Mapinduzi ya kijeshi yametishia kusimamisha mchakato wa kipindi cha mpito cha Sudan kuelekea demokrasia ambao ulianza baada ya kuondolewa kwa Omar al Bashir mwaka 2019.
 
Huyo jamaa Al Burhan anadanganywa sana na Russia lakini ajue hawataweza kumsaidia dhidi ya kuporomoka kwa uchumi wa nchi yake.

Hata walipofanya hayo mapinduzi Russia hawakuyalaani. Huyo inatakiwa apigwe ban mara moja kwa sababu ana tamaa tu ya kutaka kutawala kibabe kinyume na matakwa ya wananchi wa Sudan.
 
Back
Top Bottom