Kiongozi wa chama cha siasa kufanya vitu nje ya ilani na kutotimiza ilani ni utovu wa nidhamu

Man Wid

Member
Aug 13, 2015
44
7
Dr. Magufuli ktk hafla fulani alitoa sifa nyingi sana kwa Boss wake, nakuu "umefanya mengi sana tena mengine yapo nje ya ilani".

Kiongozi mkubwa kabisa wa chama ndio msimamizi mkuu wa ilani za chama ktk utekelezaji wake.. Sasa ukikuta kiongozi huyo nasifiwa tena na anayetegemea kuwa mrithi wake kuwa alifanya vitu nje ya ilani wakati huo ilani haijakamilika na sitegemei kwa muda uliobaki kuwa itakamilika. Sasa najiuliza:-

1. Ni dharau kwa chama chake au kuna dalili za udikteta katika kutawala wake
2.Ilani ilitengenezwa kimakosa na kama kweli kwanini isifanyiwe marekebishi na kila mwanachama ajue
3.Serikali imepewa dhamana na wananchi kutekeleza ilani sasa nje ya hapo hiyo dhamana imetoka wapi
4.Kama Magufuli akipewa dhamana na utaratibu huu anausifia si ataendelea kukiuka dhamana aliyopewa
5.Ebu wekeni na mengine mengi wanajamii maana kukosea tunaanza kidogo mpaka inakuwa mazoea
 
Moja ya viongozi waliobaki kwenye historia ya nchi hii kwa kufanya kazi yake vizuri sana ni Nyerere, ulishawahi kujiuliza kuwa alikuwa anatumia ilani ya chama gani alipokuwa anatekeleza majukumu yake?
 
CCM NI CHAMA CHA FAMILIA YAKE,anaweza kusema na kufanya atakavyo na hakuna wa kumuuliza. Ukihoji tu basi utakatwa,we huoni anachoambulia Mzee Warioba na Kingunge hivi sasa? KURA YETU NI KWA LOWASSA WA CHADEMA,UKAWA.
 
Ukimuuliza huyo mwenyekiti ilani ipo wapi au ilikuwa inasemaje hatakupa majibu.
 
Back
Top Bottom