Peter Mwaihola
JF-Expert Member
- Jun 23, 2022
- 289
- 489
Umewahi kujiuliza ni kwanini baba husifiwa kuwa shujaa na kichwa cha familia?
Tena kichwa chenye sifa ya kiuongozi ndani yake ambacho ni tegemeo la wote katika familia na jamii.
Kisha ukapata jibu kuwa baba huitwa kichwa cha familia kwa sababu gani hasa?
Bila shaka jibu lako la kwanza lilikupa mwanga kuwa baba ni jina lenye sifa ya kiuongozi ndani yake ndio maana huitwa kichwa cha familia.
Kwa maana hiyo baba aliebora hakosi sifa za Uongozi bora na umuhimu wake hujidhihirisha wakati wote.
Hata upande wa pili wa shilingi jibu bado kiongozi bora anafanana na baba aliebora.
Kiongozi bora hakosi ujasiri katika mambo mbalimbali yaliyo mbele ya jamii yake kama ilivyo kwa baba bora anapoamua jambo ndani ya familia yake.
Sio jambo geni kusikia baba amesimamia jambo fulani katika familia lilokuwa linaonekana haliwezekani lakini likawezekana, hiyo ndio sifa ya baba kama kiongozi bora.
Kiongozi bora anashaurika, huwapa mwanya wanaomzunguka kumpa mawazo mbalimbali juu ya mambo ya jamii husika.
Hata baba aliebora ni rafiki wa familia yake husikiliza na kuchukua mawazo mbalimbali ya mke wake, watoto wake Kisha huyafanyia kazi.
Kiongozi bora ni mfariji wa jamii yake mithili ya baba kwenye familia, kwani linapotokea Jambo la kutia wasiwasi kiongozi ndie hutafuta namna ya kuwatuliza watu wake wasiogope na wawe na matumaini ya kuwa salama.
kama baba inapotokea hatari kwenye familia yeye ndie huwa kipaumbele kushika silaha, kuchukua tahadhari na kuilinda familia isiingie katika mabaya.
Kiongozi aliebora hufanya maamuzi yenye busara yasiyo umiza watu wake mithili ya baba asiye na upendeleo wala umimi katika maslahi ya familia yake.
Ni wazi kuwa kiongozi aliebora ni kimbilio la watu wake na ni baba wa suluhisho la matatizo ya jamii yake.
Hatuna budi kukubali kuwa kuna ugumu kutenganisha ubora wa kiongozi na mfano wa baba aliebora kwenye familia.