Kiongozi makini hawezi kuja na propaganda za ufisadi

Kiongozi makini hawezi kuja na propaganda za ufisadi

milimo

Member
Joined
Nov 29, 2012
Posts
61
Reaction score
32
Ninavyo amini hakuna mtu mmoja pekee ambaye anaweza akawa na ufisadi unaoweza kusababisha kusinyaa kwa uchumi wa nchi na pia kudumaza huduma za jamii. Pia hakuna mtu mmoja pekee ambaye anaweza kutokomeza ufisadi. Wale wanaokuja na gia za kutokomeza ufisadi kwenye utendaji wa umma watuambie wazi mbinu watazotumia ili tuzipime na tutoe ushauri wa kuziboresha. Na kama walikuwemo serikalini watuambie kwa nini serikali (ambayo wao ni miongoni) imeshindwa kupunguza/kuondoa ufisadi na wana mbinu gani mpya za kuondoa hilo tatizo na hizo mbinu waziweke wazi. Kwa wale ambao hawakuwepo kwenye serikali inayolalamikiwa kwa ufisadi basi nao watuambia namna gani wenzeo wameshindwa kuondoa hiyo hali na wao watatumia mbinu gani kuondoa hilo tatizo. Kusema tu fulani ni fisadi msimchague hizo ni siasa za enzi za ujima. Kama kweli kuna mtu mmoja pekee ambaye ndiye aliyesababisha matatizo ya ufisadi wa nchi hii basi huyo nampa kongole na ni kichwa, kwa maana hiyo tunaweza kumtumia huyohuyo kwa uwezo huo huo kusaidia kuondoa huo ufisadi (kama Mwenyezi Mungu alivyo mgeuza Sauli/Paulo kutoka kuwa muuaji na kuwa mtume wa Mungu). Na pia kama kuna mtu pekee anaweza kuondoa tatizo la ufisadi tulilonalo basi huyo nguvu yake itakua inakaribiana na Mola.

Kuna baadhi ya vyama wanamtuhumu mtu mmoja kuwa ni fisadi (cha kuchekesha walikua naye kwa zaidi ya miongo minne), kama kweli chama kizima kilishindwa kumdhibiti mtu mmoja, basi huyo atakua lulu kumtumia kwa upande mwingine wa kudhibiti ufisadi kwa kumpa majukumu mapya ya upande mwingine (udhibiti). Najiuliza hivi huyo mtu ndiye mtu pekee aliyesimamia kusaini/kukwapua au alikuwa kiongozi wa watu waliosaini mikataba yote ya dhuruma kwa nchi na ambayo bado inaendelea kulitesa Taifa hadi sasa; nazungumzia uzwaji wa NBC, Uzwaji wa ATC kwa shirika la SAA, mikataba ya madini, ununuzi wa rada, ununuzi wa ndege ya raisi, Esrow, Richmond, EPA n.k. Tatizo la rushwa/ufisadi kwa nchi hii ni kubwa sana na kumtwisha mtu mmoja ni propaganda tu ambazo hazileti tija yoyote. Kusema ukweli kwa wale wacha Mungu na wanaofanya kazi za udhibiti kama PCCB, Polisi, Usalama nk hawako na furaha na kazi zao ila wanafanya kazi kwa sababu ya mshahara tu. Kazi zao mara nyingi ni kuumiza watu na hilo sio tatizo, ila tatizo linakuja pale ambapo usawa katika kurekebisha maovu haupo, utakuwaje na furaha na kazi yako wakati aliyeiba mabilioni waziwazi (kama ya escrow) huwezi kumgusa ila aliyegawiwa kamgao kidogo ndio unamkomalia, utakuwaje na furaha unapolazimika kumpeleka mahakamani mtu aliye saini mkataba mbovu wa milioni mbili halafu huwezi kumgusa mtu aliye saini mkataba mbuvu wa mabilion ya fedha, utakuwaje na furaha wakati unalazimika kumfungulia mashitaka mtu aliyeiba kuku halafu huwezi kumgusa mtu aliyekwapua magunia ya fedha, utakuwaje na furaha kumpeleka mahakamani mtu aliyekwepa kodi ya milioni kumi halafu huwezi kumgusa mtu anayekwepa kulipa kodi kwa sababu yuko karibu na watawala au familia za watawala. Hawa watu wanaofanya kazi kwenye tasisi hizo tuwahurumie sana kwa sababu wanafanya kazi kwenye mazingira magumu sana na kwa wale wenye hulka ya huruma na wacha Mungu hawana furaha na kazi zao maisha yote ya utumishi wao ila wanafanya kazi ili wapate mahitaji ya familia zao tu.


Hivyo tatizo la rushwa ni la kimfumo wala sio la mtu mmoja. Ingekuwa wakati ule wa Yesu Kristu ambapo aliwambia wale Wayahudi waliotaka kumpiga mawe yule Mama aliyefumaniwa (sijui hilo tendo alifanya bila mwanaume kama tunavyomnyoshea kidole mtu mmoja) kama kuna mtu hajawahi kuzini na ampige mawe yule mwanamke, nadhani kila mtu anajua kilichotokea na kama hujui muulize jirani yako atakufahamisha. Kwa mfano huo huo, hao wanaomtuhumi mwenzao kwamba ni fisadi waliuzwe swali hilo hilo mbele ya Mwenyezi Mungu kama kuna mmoja wao alifanya kazi ya umma na hajawahi kupokea rushwa, kutoa rushwa au kufanya ufisadi basi huyo amnyoshee kidole huyo anayeitwa fisadi, sidhani kama kutakuwa na kidole hata kimoja kitainuliwa. Hivyo Ufisadi/rushwa vitaondolewa au kupunguzwa kwa kutengeneza mifumo ya uwazi katika shughuli zote za umma na hizo huduma zipatikane kwa wahitaji (umaskini na rushwa ni mapacha). La muhimu ni kuimarisha uchumi wetu na wale wanaosimamia mifumo ya uchumi wawe kweli tayari kuwa waminifu na wasimamiwa vizuri na mifumio iliyowekwa. Mifumo haitengenezwi na mtu mmoja ila kundi la watu wenye mtazamo mmoja.

Mwenyezi Mungu Ibariki Tanzania hasa wakati huu tunapoelekea kwenye uchaguzi mkuu, ili uchaguzi uwe wa Amani na haki ikatendeke maana Amani ya kudumu ni tunda la haki.
 
Hahaa, haiepukiki, JIZI LOWASSA lazima lipigwe tu kwenye kampeni.
 
Bandiko lako lote hilo ndio kutetea kwamba ufisadi si hoja ya msingi?
 
mtoa mada na wachangiaji wote wa kwanza hadi wa 4 wote mpokitengo cha propaganda lumumba mkiwa na ID tofauti humu JF, lizabon=jingalo, taarifa zenu tunazo nahatuna wasiwasi na nyie. Baada ya lizabon kupuunzwa na watu humu kaamua kutumia akaunt yake nyingine.
 
Back
Top Bottom