KINNAPA kumaliza migogoro ya ardhi Kiteto

KINNAPA kumaliza migogoro ya ardhi Kiteto

JAMHURI

JF-Expert Member
Joined
Dec 15, 2010
Posts
449
Reaction score
60
Wafugaji na wakulima ni makundi ndani ya jamii ambayo yanategemeana kwa shughuli za kiuchumi ili kuendesha maisha yao.

Kawaida wafugaji wanatumia ardhi wa shughuli za ufugaji pamoja na kilimo, huku wakulima nao wakiitumia kwa Kilimo.

Shughuli hizi huendesha maisha ya makundi hayo pamoja na kwamba kwa miaka ya hivi karibuni kumeibuka uhasama baina yao.

Shirika la KINNAPA lililopo Kiteto kwa kushirikiana na Serikali pamoja na wadau wengine wa maendeleo kama Irish, wamewezesha jamii ya Kifugaji kuanzisha nyanda za malisho ya mifugo katika maeneo yao.

Vijiji vinne Lengatei, Orkitikiti, Ngapapa na Engongoengare vilijengewa uwezo na kuunda nyanda za malisho ya pamoja yaitwayo (OLENGAPA).

Katika kuunga mkono mpango huo pia vijiji vingine vinne navyo vimeweka mkataba wa pamoja kuwa na nyanda za malisho ya pamoja ili kuondoa tatizo la migogoro ya wakulima na wafugaji.

Vijiji hivyo ni Loolera, Amei, Lembapuli na Losoit ambao baada ya kuathiriwa na migogoro hiyo kwa muda mrefu kwa pamoja wameamua kutenga eneo la pamoja kwaajili ya malisho.

Mratibu wa Shirika la KINNAPA, Abraham Akilimali akizungumza na wananchi hao alisema mpango huo umekuwa na manufaa makubwa kwani nchi mbalimbali Afrika zimefika kujifunza.

"Tumepata wageni toka nchi nane Afrika kuja kujifunza mpango huu.. kama vijiji hivi vitaamua kuutekeleza vyema na kwa umakini migogoro itakuwa ndoto?

Kwa upande wake Bw. Nkini Seba kaimu afisa misitu Wilaya alisema suluhisho la migogoro ya ardhi Kiteto pamoja na mipango ya matumizi bora ya ardhi pia ni kuwa na nyanda za malisho ya pamoja kwaajili ya mifugo.

Kwa upande wa wenyeviti hao walipongeza Shirika la KINNAPA kwa kusaidia wakulima hao kuanzisha na kubuni mpango huo wakisema utakuwa mwarubaini wa migogoro.

Nao wananchi walisema pamoja na kuridhia mpango huo Serikali wanapaswa kuhakikisha wanakuwa karibu hasa katika wakati huu ambao wako katika hatua za awali.

Mwisho
 

Attachments

  • IMG_20180908_160721.jpg
    IMG_20180908_160721.jpg
    104.8 KB · Views: 32
Back
Top Bottom