Kingwendu na Steve Nyerere: Tumieni "Vipaji" mnaposoma magazeti E-Fm Radio

nyumbamungu

JF-Expert Member
Mar 3, 2017
997
828
Kwanza natoa pongezi kwa Uongozi wa E-Fm Radio kwa kuwa kumbuka na kuwaamini Wasanii hususani wa Maigizo maarufu kama Bongo Movie kwa kuwa sehemu ya Watangazaji wake, baadhi niliowasikia wakitangaza ni pamoja na Bi Hindu, Swebe, Mpoki hao wanasikika kwenye vipindi kama Watangazaji.

Hawajaishia hapo takribani miezi miwili au mitatu wamewaongeze wengine wawili Steve Nyerere na Kingwendu Ngwendulile, katika kipindi cha Joto la Asubuhi katika kipengele cha Kusoma magazeti, Rai yangu kwao watumie Vipaji vyao vya sanaa katika kusoma na kuchambua habari wanazosoma bila kuzidisha utani utakaoudhi na wenye madhara au mbwembwe zitakazoharibu uchambuzi wao na ikaharibu hiyo habari nzima.

Napenda kuwakumbusha nadhani wanamkumbuka Msanii mwenzao Idd Ligongo waliokuwanae katika fani akatumia fursa vizuri na leo tunavyoongea yupo Sauti ya Amerika (VoA) kama Mtangazaji. Mwisho "Wamkumbatie" sana Nguli na Muanzilishi wa kuhoji habari za kwenye magazeti akiwa hewani Komredi Gerald Hando, enzi zile akiwa na Fina Mango pamoja na Jimmy Kabwe. Bila kumsahau Mussa Kipanya na Babby Mama.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom