Kingunge? Waseme wengine

singidadodoma

JF-Expert Member
Nov 11, 2013
4,394
1,531
UAMUZI wa kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kingunge Ngombale Mwiru kujiondoa kwenye chama hicho umekosolewa na Katibu Mkuu wa chama hicho, Abdulrahaman Kinana, pamoja na aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba.

Kwa mujibu wa Kinana, tatizo kubwa la Kingunge ni mgombea aliyekuwa akimuunga mkono hadharani kushindwa kupitishwa na vikao vya CCM, lakini kwa mujibu wa Jaji Warioba, Kingunge hawezi kujitenga na udhaifu au uimara unaohusishwa na CCM katika masuala ya uongozi.

Kinana akizungumza na Raia Mwema wiki hii kihusu hatua hiyo ya mzee Kingunge alisisitiza kwamba, kanuni na taratibu kuhusu uteuzi wa mgombea urais CCM zilizingatiwa, na Lowassa, anayepigiwa debe na Kingunge, alishiriki kupiga kura kwa mujibu wa Katiba ya CCM, ndani ya Halmashauri Kuu (NEC) kuchagua majina matatu kati ya matano kutoka Kamati Kuu ili kwenda Mkutano Mkuu, lakini vile vile alishiriki kupiga kura ndani ya Mkutano Mkuu, kuchagua jina moja kati ya matatu yaliyoletwa kutoka NEC.

Kinana anasema Lowassa alishiriki kupiga kura kuchagua majina matano ambayo ni January Makamba, Balozi Amina Salumu, Dk. Asha Rose Migiro, Bernard Membe na Dk. John Magufuli.

Kauli ya Kinana
Kwanza nianze kwa kusema kwamba namheshimu sana mzee Ngombale, amekitumikia Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa muda mrefu sana na vile vile ameitumikia nchi kwa muda mrefu pia. Anastahili heshima na kwa kweli mimi namheshimu sana.

Lakini jambo jingine analozungumza ni kuhusu malalamiko dhidi ya CCM kwamba, chama hakikutenda haki katika mchakato wa uteuzi wa mgombea urais.

Napenda kusisitiza kwamba mchakato wa uteuzi ndani ya CCM umezingatia Katiba ya chama chetu na vikao vyote vilivyofanyika vimezingatia matakwa ya Katiba ya chama.

Katiba ya CCM ukurasa wa 168 kifungu B cha ibara 109, kinaeleza kazi za Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu wakati wa uchaguzi, kwamba ni pamoja na "..kufikiria na kutoa mapendekezo yake kwa Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa juu ya majina ya wanachama wasiozidi watano wanaoomba kugombea kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Katika vikao vya uteuzi, kulikuwa na mjadala mrefu na taratibu zote zilizingatiwa.

Tatizo lililopo kwa mzee Ngombale ni moja tu, ni kwamba alikuwa na mgombea wake aliyemchagua kabla hata ya vikao vya chama. Badala ya yeye kusubiri taratibu na vikao vya chama tayari alikuwa ameshiriki kutengeneza na kutangaza mgombea wake, akaamua mgombea wake ndiye awe huyo huyo bila kujali uamuzi wowote wa vikao. Wagombea wote 38 walitendewa haki kwa kuzingatia katiba na taratibu za CCM.

Tangu mchakato wa uteuzi wa mgombea urais uanze, mzee Ngombale alikuwa na mgombea wake ambaye ilikuwa dhahiri kama hakuteuliwa huyo basi Katiba na taratibu zimekiukwa.

Maelekezo ya kikatiba yapo na yamefuatwa, ukisoma ibara ya 107 kifungu 13(B) inaweka bayana kwamba majukumu ya Kamati Kuu ni kutoa majina matano kwenda NEC ambako yanapigiwa kura na kupatikana majina matatu yanayokwenda kwenye Mkutano Mkuu kwa ajili ya kupigiwa kura na kupata jina moja. Kamati Kuu ilifanya kazi yake, majina yalipelekwa NEC kote mijadala ilifanyika na hatimaye NEC ilipiga kura na kisha Mkutano Mkuu ulipiga kura.

Na kwa taarifa yenu na wengine ni kwamba, Lowassa ambaye ndiye mgombea wa mzee Ngombale alipiga kura ndani ya NEC kwa ajili ya kupata majina matatu lakini vile vile, katika Mkutano Mkuu Lowassa huyo huyo mgombea wa mzee Ngombale alipiga kura.

Kwa hiyo, Lowassa alishiriki kutafuta wagombea watatu kati ya watano kutoka Kamati Kuu na pia alishiriki katika mchakato wa kupata mgombea mmoja kati ya watatu ndani ya Mkutano Mkuu.

Mgombea ambaye mzee Ngombale alimbeba alishiriki kikamilifu vikao vya NEC na Mkutano Mkuu baada ya mchakato wa awali kukamilika kwa mujibu wa Katiba ya Chama na taratibu zake.

Kuhusu uamuzi wake wa kujivua uanachama wa CCM, niseme tu kwamba alijiunga na CCM kwa hiari yake na kwa kweli amejiondoa kwa hiari yake, sisi tunamtakia kila la kheri katika maisha yake ya kustaafu.

Lakini hili la upatikanaji wa mgombea mfumo uliotumika mwaka huu ndiyo ule ule uliotumika mwaka 1995, mwaka 2005 na katika michakato hiyo, mzee Ngombale alishiriki na kukubaliana na uamuzi wote wa vikao husika.

Mwaka 1995 kulikuwa na wagombea 17, mchakato ukafanyika wakapitishwa watano kwenye Kamati Kuu na baadaye watatu kutoka Halmashauri Kuu kwenda Mkutano Mkuu ambao ni mzee Cleopa Msuya, Benjamin Mkapa na Jakaya Kikwete na hatimaye mzee Mkapa akashinda.

Mwaka 2005 mfumo huo huo ulitumika, walikuwa jumla ya wagombea 11, katika Kamati Kuu wakapitishwa watano kwenda NEC na kwenye NEC wakapitishwa watatu kwenda Mkutano Mkuu ambao ni Dk. Salim Ahmed Salim, Jakaya Kikwete na Profesa Mark Mwandosya.

Kwa hiyo, Mzee Ngombale hakitendei haki chama chetu kutokana na tuhuma zake hizo. Na tena niwakumbushe tu kwamba, mwaka 1995 Lowassa alikatwa jina na mzee Ngombale alikuwamo kwenye vikao na aliunga mkono, akakubaliana na uamuzi wa vikao.

Sababu zilizotumika kumwondoa Lowassa mwaka 1995 ndizo zile zile, kwa hiyo utaona mzee Ngombale mwenye mitazamo miwili inayotofautiana. Anazo kauli mbili, ile ya mwaka 1995 ya kukubaliana na sababu za kuenguliwa kwa Lowassa na mwaka huu 2015, sababu zile zile ambazo hakubaliani nazo.

Mzee Ngombale alikuwapo kwenye vikao vya Kamati Kuu na Halmashauri Kuu, na tena mwaka 1995 kwenye NEC atakumbuka kwamba baada ya Lowassa kutuhumiwa, kuna mjumbe mmoja wa NEC alipendekeza aitwe kikaoni ili atoe maelezo juu ya tuhuma dhidi yake.

Lowassa alishindwa kutoa sababu zilizojitosheleza katika kujitetea dhidi ya tuhuma zilizoelekezwa kwake na kikao
kikaondoa jina lake. Lakini pia mzee Ngombale anakumbuka namna John Malecela alivyoondolewa na aliridhika na uamuzi wa vikao. Malecela rufaa yake ilikataliwa na wajumbe wa NEC. Hapa ukweli ni kwamba, chama hakiwezi kuwa na misimamo miwili tofauti kwa jambo moja linalofanana.

Kwa hiyo, uamuzi uliofanyika katika mchakato wa uteuzi wa mgombea urais ulikuwa wa haki na nafikiri mgombea wa mzee Ngombale angepita asingeweza kuzungumza maneno haya..

Alipoulizwa kama yuko tayari kuunda timu ya wazee kwa ajili ya kuzungumza na mzee Ngombale ili asitishe uamuzi wake, Kinana alisema; "Angekuwa ametangaza kwamba anatafakari kujiondoa CCM hapo tungeweza kufanya hivyo lakini yeye amekwishakutangaza kujiondoa CCM, tunamtakia kila la kheri."

Vile vile alipoulizwa kwamba haoni mzee Kingunge anaweza kuwa na athari katika kampeni za sasa za CCM kuisaka Ikulu, alisema; "Sidhani kama kutakuwa na athari yoyote. Takriban asilimia 75 ya maisha ya mzee Ngombale yamekuwa ndani ya CCM na serikali yake. Ameshiriki kikamilifu kuandaa na hata kusimamia sera na programu mbalimbali za CCM katika nyadhifa za juu zaidi kwenye chama na serikali. Kwa hiyo, leo Watanzania hawatamwamini na kwa kweli watamshangaa sana kama yeye ndiye kinara na msemaji wa mabadiliko hayo yanayozungumzwa."

"Ni miujiza kwa Watanzania kumwamini mzee Ngombale kwamba ndiye wakala wa mabadiliko nje ya CCM. Lakini katika tuhuma zake mzee Ngombale na Lowassa wanasema demokrasia na haki haikufuatwa kwenye mchakato wa uteuzi CCM, jambo ambalo si kweli kama nilivyofafanua, lakini na mimi nataka niwaulize huo mchakato wa kumteua Lowassa kuwa mgombea wa Chadema na kisha Ukawa, umefuata utaratibu?

"Je, kilichofanyika Chadema ni haki na demokrasia? Ninavyojua, Chadema wanayo katiba yao na taratibu zao za namna ya kumpata mgombea urais kwa kushindanisha wanachama wao, lakini vile vile, Ukawa walikuwa na kanuni zao walizokubaliana juu ya namna ya kumpata mgombea urais kwa pamoja.

"Haya yote hayakuzingatiwa, Lowassa alitoa masharti kwa Chadema, kwanza, hakutaka apambanishwe na mwanachama mwingine yeyote kwenye chama hicho katika uteuzi wa mgombea urais – awe mgombea pekee, hakutaka kuwapo kwa mchakato wa urais wa wazi.

"Lakini si tu ndani ya Chadema, hata ndani ya Ukawa, aliweka masharti hayo hayo, awe mgombea pekee ambaye hatashindanishwa na wenzake. Yaani siku ya kwanza alijiunga Chadema, siku ya pili, akateuliwa kuwa mgombea urais na siku ya tatu akateuliwa na Ukawa kuwa mgombea wao pekee.

Namuuliza Ngombale, kwenye CCM tumeweka bayana haki na demokrasia ilifuatwa; je, huku Chadema na Ukawa haki imetendeka? Je, wanachama wa Chadema walipata fursa ya kutimiza haki yao ya kuomba kugombea urais? Vipi kuhusu Ukawa, wagombea wengine walishindanishwa na Lowassa kama matakwa ya kanuni zao yalivyoelekeza?

"Watanzania hawawezi kuwaamini watu wa namna hii na kwa kweli, inashangaza kwamba, alama ya mabadiliko yanayozungumzwa taswira yake ni mzee Ngombale na Lowassa. Watu ambao hawana umadhubuti mioyoni wa kuzungumzia demokrasia ambayo imevunjwa huko huko wanakonadi kile wanachoita mabadiliko.

"Mimi nasema kama ni mabadiliko kwa mantiki ya mabadiliko wanayozungumzia kwa nini hawakuyaleta ndani ya CCM na serikalini ambako walikuwa wametumikia kwa miaka mingi? Hawa wanahadaa Watanzania kama vile ambavyo wanahadaa hata nafsi zao.

Hakuna jambo ambalo limeamuliwa na kutekelezwa kwa ushawishi wa CCM bila Kingunge kwa miaka mingi, kwa hiyo kama CCM inahitaji pongezi zinamhusu Kingunge na kama inahusika kulaumiwa basi hizo lawama zinamhusu," alisema Kinana na kusisitiza kuwa Kingunge hawezi kuwa alama ya mabadiliko.

Kuhusu madai ya Kingunge kwamba, katika Awamu ya Nne, Rais Jakaya Kikwete hakuna jambo la maana alilofanya, Kinana alisema; "Rais Kikwete amefanya kazi kubwa sana kwa kipindi chake cha miaka 10 katika nyanja zote, Ngombale anajua na mgombea wake (Lowassa) anajua na mara kadhaa wamemsifu Rais Kikwete hadharani.

Anaweza kuwa na tofauti zake na Rais Kikwete lakini kusema kwamba hakuna jambo la maana alilofanya, si sahihi. Si jambo linalotarajiwa kutoka kwake."

Kauli ya Warioba
Kwa upande wake, aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba naye ameelezea kushtushwa na uamuzi wa Kingunge Ngombale Mwiru, akipinga sababu zilizotumiwa na kada huyo mkongwe kujiondoa CCM lakini vile vile, akikumbuka enzi za ujana wao namna walivyokuwa wakiandaa propramu za chama chao kupitia kundi lao maalumu, maarufu kwa jina la TANU Study Group.

"Nimeshtushwa kusikia Ngombale anatoka CCM, amekuwapo TANU na CCM kwa miaka 61. Tulikuwa naye TANU tukifanya kazi ya ubunifu wa maandishi na uchambuzi katika kusaidia chama, tulikuwa naye pamoja na akina Patrick Qoro, Gisler Mapunda na wengine. Ngombale anahusika na mafanikio karibu yote ya chama. Hana historia nje ya TANU na CCM. Chochote alichofanya na kufanikiwa msingi wake ni chama. Nadhani ingekuwa sahihi kwake kuendelea na kubaki katika historia hiyo, akaendelea kuitetea.

"Angebaki kutetea itikadi anayoitambua, lakini kitendo chake cha kujiondoa ni udhaifu. Na kwa kweli, amethibitisha kwamba yeye na baadhi ya wenzake ndiyo waliokuwa wakikwamisha mabadiliko ndani ya CCM, mabadiliko ya kukataa uongozi kununuliwa, mabadiliko ya kukataa siasa za mitandao. Haya ndiyo mabadiliko tuliyokuwa tukiyapigania mimi na baadhi ya wenzangu, huko wao wakishiriki kuyapinga.

"Sisi tulikuwa tunataka mabadiliko ndani ya CCM, tulipingwa, tulisema hakuna umoja tunahitaji umoja zaidi, tulisema uadilifu umetetereka mno katika chama kiasi cha fedha kuwa ndiyo kila kitu. Walitupinga na kwa kweli, katika hili, Kingunge na wenzake walikuwa wakipinga mabadiliko na kushabikia siasa za mitandao na makundi. Sisi tulitaka maamuzi magumu yafanyike CCM ili kukirejesha chama kwenye mstari.

Sasa leo hii, dalili za mabadiliko tuliyokuwa tukiyataka zimekuwa dhahiri, tumepata mgombea ambaye hakutumia fedha kushinda uteuzi, tumekuwa na mgombea ambaye hakuwa na makundi, huu ni mwanzo mzuri wa kufanya mabadiliko ya kiuongozi ndani ya chama na serikalini.

"Ni vigumu kukubaliana na sababu anazozitoa Ngombale, yeye badala ya kufanya uamuzi kwa kuzingatia matakwa ya misingi ya chama chetu, anafanya uamuzi kwa kumfuata mtu. Mtu hawezi kuwa ndiye mustakabali wa chama hata kidogo. Mimi nitaendelea kumheshimu lakini kwa hili (la kumfuata Lowassa badala ya kusimamia misingi ya kiitikadi) sikubaliani naye," alisema Jaji Warioba

Jaji Warioba aliongeza kusema: "Mwaka 2005 tulizungumza masuala haya ya kupinga makundi na mitandao, alivumilia na kutetea hali hiyo. Mimi nadhani kinachomsumbua yeye na watu wengine ni kuangalia matokeo ya mchakato na si taratibu za mchakato.

Awali, mimi niliposikia kwamba kuna vijana wa CCM wanakusudia kushinikiza Ngombale afukuzwe, nilisema wakifanya hivyo watakuwa wamefanya makosa makubwa, lakini sasa amejiondoa mwenyewe kwa sababu ambazo hazina uzito. Kama ni suala la udhaifu wa CCM basi Ngombale hawezi kukwepa udhaifu huo, yeye ni sehemu ya udhaifu huo. Amefanya makosa kujiondoa CCM."

Kingunge: Kwa nini nimeondoka
Akizungumza na waandishi wa habari nyumbani kwake Kijitonyama, jijini Dar es Salaam Jumapili iliyopita, Kingunge alisema anaondoka CCM kwa kuwa hakuridhishwa na mchakato wa uteuzi wa mgombea urais wa CCM, akisema wagombea wote, takriban 38 hawakutendewa haki na Kamati Kuu, na wengi wao majina yao yalichujwa na Kamati ya Maadili ya chama hicho, akisema kamati hiyo haikuwa na uhalali wa kufanya hivyo.

Vile vile Kingunge alidai kwamba Rais Jakaya Kikwete hakufanya jambo la maana katika kuendesha nchi katika kipindi chake cha uongozi wa miaka 10, lakini vile vile, CCM kimepoteza uhalali wa kuongoza nchi, akidai kimeishiwa kile alichokiita pumzi

Chanzo Raia Mwema
 
hakika comrade kinana na jaji warioba wamesema kweli.mzee ngombale amekitumikia ccm zaid ya miaka 60 ikiwa ccm imefanya vyema basi hatuwezi kuzitenga pongezi hizi na ngombale lakin kama ccm imefanya mabaya basi nayo hayawezi kuyatenga na ngombale.
mzee ngombale ameshindwa kusimamia itikadi na misingi aliyo iamini na kuishia kumfuata mtu.
hakika mzee wangu ngombale kwa hili umetupa mipaka na u ndani ya upotovu ulio mkuu
 
Mzee Kingunge Ngombale Mwiru kuwadi wa Ufisadi "The fight for justice against corruption is never easy. It never has been and never will be. It exacts a toll on our self, our families, our friends, and especially our children. In the end, I believe, as in our case, the price we pay is well worth holding on to our dignity". Frank Serpico Hayo maneno hapo juu yamenifanya nifikirie sana tamko la Mzee Kingunge Ngombale Mwiru(KNM), kama alivyokaririwa na gazeti la mwananchi la Jumapili(Makala hii).Na kunikumbusha ukubwa wa tunachokipigania. Anachokifanya Mzee Kingunge, si kigeni ana cheza na kumbukumbu yetu. Anata kutuaminisha Kingunge wa leo ni yule yule Kingunge wa kipindi cha mwalimu Nyerere. Lakini tuki re-load kidogo tu, ukurasa wetu wa kumbukumbu unakuja na majibu mazuri ambayo, yanatupunguzia wasiwasi wa anacho kifanya Mzee (KNM) Kingunge wa leo ni nani , Je anafananaje na Mgombea anayempigia debe? 1. Jibu ni ndio. Kama Lowassa alivyopoteza Uwaziri Mkuu kwa UFISADI wa Richmond,Kingunge naye mda mchache tu baada ya Lowassa kutoka kwenye uwaziri mkuu, alipoteza Mrija wake mkuu wa kipato ( Kwenye Parking systems za Dar es salaam). Andiko hili litajikita kwenye mrija wake mmoja tu, uliokatika pale Ubungo Bus terminal. Taarifa ya Mkugazuzi wa Hesabu za serekali- ya mwaka wa fedha ulioishia, 30th June, 2009, ilikuwa na haya ya kusema kuhusu kampuni iliyomilikiwa na familia ya Mzee Kingunge. "A Special Audit conducted at Dar es Salaam City Council was carried out at Ubungo Bus Terminal (UBT) owned by City Council Management. The Audit particularly covered revenue collections generated from the UBT. The brief outcomes are as follows: • The Dar es Salaam City Council entered into a contract with an Agent M/s Smart Holding Company Limited of DSM to collect revenues on behalf of Dar es Salaam City Council. According to Contract Agreement, the Agent was contracted to pay to the Council Shs.1,500,000 per day as revenue accruing from motor vehicles using the terminal, i.e security provided to Passenger Buses kept over night, parking and entrance fees. • We carried out the study on the same sources of revenue and the outcome of the study indicated that the average revenue for the described sources was Shs.4,618,629 per day compared to Shs.1,500,000 the Council was getting from the Agent which is far apart. • We noted existence of unauthorized leasing of the business premises without owner's consent. For example, the lessee paid Shs.130,000 per month as rent to the lessor (the owner) while the lessee received Shs.600,000 per month from unauthorized subleases. • Total revenue collection for the period from June, 2006 to April, 2008 amounting to Shs.146,692,226 collected by revenue collectors but the same were not banked. • The Dar es Salaam City Council entered into contract with 100 small vendors to carry out business at Ubungo Bus Terminal Kwa maneno mengine, Kwenye makusanyo tu, Mzee kingunge alikuwa anapata faida ya Milion 3 kwa siku (3,118,629) au Kipato cha mzee kwa mwezi kilikuwa milioni 90+. Sasa baada ya huu mrija na mingine inayohusu parking system Kuzibwa Kwanini asiungane na mafisadi wenzie kupinga maamuzi ya chama yenye masilahi mapana ya nchi. Huku akijua akifanikiwa atakula pipi tamu zaidi. Na hiyo ndio bei ya utu wa Mzee Kingunge, tusishangae. Na si kuwadi tu wa UFISADI nay eye ni FISADI. Kusoma kwa nini Lowassa ni Fisadi na Ushahidi--- bofya hapa Kusoma Ripoti ya Mkaguzi wa Serekali kuhusu UFISADI wa Familia ya Kingunge ( Page 198-200), Bofya hapa From JF
 
Habofyi MTU hapo. MTU unaonekana kabisa umeandika kwa ushabiki tubofye ili kiwe nn? Tunachokijua sisi wananchi wa kawaida ni kuwa vita iliopo ccm ni vita ya kimaslahi kwa makundi yanayohasimiana. Ikikatwa mirija kwenye kundi A basi inafunguliwa kundi B. Chama kimeshaondoka kwa wakulima na wafanyakazi kimekuwa cha wafanyabiashara na wapiga michongo. Sisi wananchi tunaamini kama mirija imekatwa kwa akina Kingunge na imefunguliwa kwa kina Lizone basi jambo LA mhimu ni kuipiga chini ccm tujipange upya maana ccm haina maslahi kwa wananchi. Tulitaka mirija ikatwe kwa makundi hasim ndani ya ccm kisha ifunguliwe kwa wananchi. Na tunaamini akina Warioba na wenzao wanaoitetea ccm kwa nguvu zote haram na halali wanajilinda ili wasije hukumiwa kwa makosa waliyoyatenda ktk michongo yao. Pia tunaamini mtu yeyote anayehama ccm ni msafi wa kiwango cha juu sana. Mtu anayejiunga na ccm ni mwenye tamaa na aliyepigika balaa. By mwananchi kutoka Makete na Tunduma.
 
nilifurahishwa sana na yule muandishi aliyemuuliza swali kuwa kingunge anasema huu ni muda wa mabadiliko, je lowassa angepitishwa na ccm angeyasema haya? je angehama chama? kingunge alibaki kujiuma uma tu. wala hakuwa na jibu la maana.
 
dr Slaa mnamsifu kujitoa chadema, Kingunge mnamshutumu kujitoa ccm,mbona wote sababu ni moja kugombea urais. lazima mkubali kwanza ccm imechokwa na watanzania walio wengi hata kama mgombea wake angekuwa Lowasa
 
nilifurahishwa sana na yule muandishi aliyemuuliza swali kuwa kingunge anasema huu ni muda wa mabadiliko, je lowassa angepitishwa na ccm angeyasema haya? je angehama chama? kingunge alibaki kujiuma uma tu. wala hakuwa na jibu la maana.
jibu la maana hapo ni kwamba watanzania wengi wamechoshwa na ccm kwa kila mwenye kutaka kuwa ndani ya uongozi wa nchi kialali lazima ajitoe ccm
 
Back
Top Bottom