Kingunge ndani ya mkate wa Edward N. Lowassa

Kingunge ndani ya mkate wa Edward N. Lowassa

chakii

JF-Expert Member
Joined
Sep 15, 2013
Posts
21,369
Reaction score
27,785
Katika kumbukumbu za mwaka 1995 wakati wa mchakato wa kupata wagombea wa kushika nafasiya urais, Kingunge Ngombale Mwiru alikuwa mjumbe wa kamati kuu CCM.

Kama kawaida mchakato wa vikao vikuu CCM uliwadia, lakini kabla ya kuanza kwa vikao hivyo, Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, alikuwa amekutana mahali fulani na Kingunge jijini Dar es salaam na kunong'onezana kuhusu uadilifu wa Lowassa, mwanasiasa kijana tu wakati huo ambaye alikuwa ameamua kutaka kuongoza Taifa hili.

Mwalimu alikuwa anamwamini sana Kingunge, ama pengine kutokana na uelewa wake au kutokana na utiifu wake wa " ndiyo mzee". Kamati Kuu ilipoanza kikao chake na jina la Lowassa kuwasilishwa mbele ya wajumbe wa kikao hicho ili waweze kulijadili, mtu wa kwanza kusimama ndani ya kikao kwa lengo la kueleza sifa za Lowassa alikuwa ni Kingunge.

Huyu huyu tunayemjua kuwa ni miongoni mwa wanasiasa wakongwe hapa nchini, ambao sisi wengine tuliwafahamu na kuwaamini kwamba siasa zao na itikadi zao zinaongozwa na ujamaa au ukomunisti. Moja ya itikadi ambayo Baba wa Taifa, aliikubali nakuiamini kwamba inaweza kuwaondoa Watanzania kwenye unyonge wa kifikra katika kukabiliana na umaskini, ujinga na maradhi.

Ni kingunge aliyewaeleza wajumbe wa Kamati Kuu jinsi Lowassa asivyofaa hata kujadiliwa na kikao hicho kutokana na utajiri mkubwa alionao wa fedha na mali nyingi, yakiwemo majumba ya kifahali wakati umri wake na muda wake wa utumishi wa umma, havifanani na utajiri wake huo.

Zipo pia taarifa kuwa ni Kingunge aliyewakumbushawajumbe kuwa CCM ni chama cha wakulima na wafanyakazi wanyonge, hivyo hakiwezi kuongozwa na Kada wake mwenye utajiri usiokuwa na maelezo ni wapi ameupata mali hizo na kwa njia gani!

Baada ya maelezo hayo ndipo Mwalimu Nyerere akapigilia msumari kuwa Lowassa hana sifa za kuliongoza Taifa hili. Kuna wakati marafiki zake Lowassa walipopata taarifa hizi walimjulisha Lowassa kuwa aliyepigilia msumari jina lake kukatwa alikuwa Kingunge Ngombale Mwiru.

Lowassa baada ya kupata taarifa hizo alimtolea uvivu Mzee Kingunge na kumwendea, kabla ya kumtamkia kuwa "wewe mzee ni mtu mbaya sana siwezi kuongea na wewe tena katika maisha yangu." Lakini baadaye Nyerere aliwapatanisha baada ya Kingunge kulalamika na kushitaki kwake.

Cha kushangaza sasa katika Hotuba yake Kingunge aliyoitoa kwa niaba ya wazee wa CCM katika safari ya Matumaini hiyo ya Lowassa siku ile ya Jumamosi ya Mei 30, mwaka huu, katika Uwanja wa Sheikh Amani Abeid, imewashangaza wengi na kumuonyesha kuwa Kingunge hana nia nzuri kwa chama chake cha CCM na Tanzania kwa ujumla wake.

Kifupi kabisa niseme mapema hapa; kwamba kama Kingunge alidhani hotuba yake ile imemjenga mtu wake Lowassa, atakuwa amejidanganya mwenyewe. Kwa maoni yangu, hotuba ile imerahisisha sana jukumu la vyama vya siasa nchini vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) kuing'oa CCM katika Uchanguzi Mkuu wa Oktoba 25 Mwaka huu!

Tuendelee kuona mengi na kuyafahamu.
 
Kama enzi za 1995, Lowassa alikuwa na guts za kufuata Kingunge na kumpa vipande vyake, kwa kipindi hiki Lowassa anaweza kumzaba vibao huyu mzee na labda ndicho Kingunge kahofia hilo lisimpate imebidi ajikombe. Sababu nyingine kwa sasa Kingunge anajihusisha na ufisadi wa kiaina fulani, kwahiyo anajaribu kufuta kabisa mambo ya 1995 ili asije kusutwa.
 
Siasa mchezo mchafu, anachoangalia sasa yule ni akifa azikwe kifahari, ndio maana anakaa karibu ya waridi ili anukie.
 
cyber law jaman mtu unakula maharage unaota unakuja leta hekaya jf

no research no right to speak. kati yako na yeye nani amekula maharage sijui ya wapi?

watanzania wengi hawatafuti taarifa wala hawataki kusoma halafu mnakimbia kimbia na kutoa maneno machafu kwa watu wanaotafuta taarifa kwa udi nauvumba.

WEWE IANWEZEKANA UKIWEKEWA TV INAYOONYESHA TAARIFA YA HABARI NA NYINGINE BONGO FRAVOR UNAONEKANA UATAANGALIA BONGO FLAVOUR BADALA YA TAARIFA.

HII HABARI ILIYOWEKWA NA NA MLETA UZI AMEITOA KWENYE GAZETI LA RAIA MWEMA TOLEO LA JANA. Na stori hii inakumbusha jinsi KINGUNGE alivyofanikisha zoezi la kumtosa LOWASA kwenye uteuzi wa mgombea urais 1995. kingunge alikuwa mstari wambele kuwashawishi wajumbe wasimpitishe lowasa kwa sababu alikuwa ni tajiri wa muda mfupi na haikujulukana aliutoa wapi huo utajili. kwa hiyo KINGUNGE na NYERERE WAKAFANIKIWA KUWASHAWISHI WAJUMBE WASIMPITISHE LOWASA NA IKAWA HIVYO. LAKINI SASA HIVI KINGUNGE NDIYE AMEKUWA MPAMBE MKUBWA WA KUMTETEA LOWASA ALIYEMKATAA 1995.

Information is power
 
Naona Lowassa alimwajiri babu akamsafishe la sivyo pangechimbika,na mzee akaitikia pasipo kuelewa Nyerere aliwahi kukataa kumsafisha Lowassa.
 
  • Thanks
Reactions: DSN
Da hii maneno ngumu kumesa na kama ni kweli basi CCM ilikotoka mpaka ilipofika hapa inaitaji mtu mwenye ubongo wa kweli kweli si ubongo wa kinafiki katika kuishape iendane na nyakati mpya.
 
nasikitika kusema kwamba mengi uliyoongea umeyatunga na umemwingizia maneno mdomoni hayati mwalimu na pia hujui kilichotokea siku hiyo.....acha kuandika vitu usivyovijua
 
Mwaka 1995 na 2015 ni tofauti ya miaka 20.

CCM imebadilika sana na sio chama cha wakulima na maskini tena. Wanasiasa karibu wote sasa ni matajiri.

Utajiri wa Lowassa sio issue tena. Hata mtoto wa mkulima sio maskini tena.
 
Naona Lowassa alimwajiri babu akamsafishe la sivyo pangechimbika,na mzee akaitikia pasipo kuelewa Nyerere aliwahi kukataa kumsafisha Lowassa.
hakumwajiri ila ametumia gharama zake kwenda na kurudi, kula na kulala Arusha, kwa sababu aliambiwa aende akasafisha uchafu wake aliosambaza mwaka 1995, bila ya hivyo pangechimbika na Nyerere ambaye angemsaidia hayupo. Babu ikabidi achukue makusanyo ya kodi pale ubungo terminal na aende AR.
 
katika kumbukumbu za mwaka 1995 wakati wa mchakato wa kupata wagombea wa kushika nafasiya urais, kingunge ngombale mwiru alikuwa mjumbe wa kamati kuu ccm.

Kama kawaida mchakato wa vikao vikuu ccm uliwadia, lakini kabla ya kuanza kwa vikao hivyo, baba wa taifa, mwalimu julius nyerere, alikuwa amekutana mahali fulani na kingunge jijini dar es salaam na kunong'onezana kuhusu uadilifu wa lowassa, mwanasiasa kijana tu wakati huo ambaye alikuwa ameamua kutaka kuongoza taifa hili.

Mwalimu alikuwa anamwamini sana kingunge, ama pengine kutokana na uelewa wake au kutokana na utiifu wake wa " ndiyo mzee". Kamati kuu ilipoanza kikao chake na jina la lowassa kuwasilishwa mbele ya wajumbe wa kikao hicho ili waweze kulijadili, mtu wa kwanza kusimama ndani ya kikao kwa lengo la kueleza sifa za lowassa alikuwa ni kingunge.

Huyu huyu tunayemjua kuwa ni miongoni mwa wanasiasa wakongwe hapa nchini, ambao sisi wengine tuliwafahamu na kuwaamini kwamba siasa zao na itikadi zao zinaongozwa na ujamaa au ukomunisti. Moja ya itikadi ambayo baba wa taifa, aliikubali nakuiamini kwamba inaweza kuwaondoa watanzania kwenye unyonge wa kifikra katika kukabiliana na umaskini, ujinga na maradhi.

Ni kingunge aliyewaeleza wajumbe wa kamati kuu jinsi lowassa asivyofaa hata kujadiliwa na kikao hicho kutokana na utajiri mkubwa alionao wa fedha na mali nyingi, yakiwemo majumba ya kifahali wakati umri wake na muda wake wa utumishi wa umma, havifanani na utajiri wake huo.

Zipo pia taarifa kuwa ni kingunge aliyewakumbushawajumbe kuwa ccm ni chama cha wakulima na wafanyakazi wanyonge, hivyo hakiwezi kuongozwa na kada wake mwenye utajiri usiokuwa na maelezo ni wapi ameupata mali hizo na kwa njia gani!

Baada ya maelezo hayo ndipo mwalimu nyerere akapigilia msumari kuwa lowassa hana sifa za kuliongoza taifa hili. Kuna wakati marafiki zake lowassa walipopata taarifa hizi walimjulisha lowassa kuwa aliyepigilia msumari jina lake kukatwa alikuwa kingunge ngombale mwiru.

Lowassa baada ya kupata taarifa hizo alimtolea uvivu mzee kingunge na kumwendea, kabla ya kumtamkia kuwa "wewe mzee ni mtu mbaya sana siwezi kuongea na wewe tena katika maisha yangu." lakini baadaye nyerere aliwapatanisha baada ya kingunge kulalamika na kushitaki kwake.

Cha kushangaza sasa katika hotuba yake kingunge aliyoitoa kwa niaba ya wazee wa ccm katika safari ya matumaini hiyo ya lowassa siku ile ya jumamosi ya mei 30, mwaka huu, katika uwanja wa sheikh amani abeid, imewashangaza wengi na kumuonyesha kuwa kingunge hana nia nzuri kwa chama chake cha ccm na tanzania kwa ujumla wake.

Kifupi kabisa niseme mapema hapa; kwamba kama kingunge alidhani hotuba yake ile imemjenga mtu wake lowassa, atakuwa amejidanganya mwenyewe. Kwa maoni yangu, hotuba ile imerahisisha sana jukumu la vyama vya siasa nchini vinavyounda umoja wa katiba ya wananchi (ukawa) kuing'oa ccm katika uchanguzi mkuu wa oktoba 25 mwaka huu!

Tuendelee kuona mengi na kuyafahamu.

umekuraaaamaharageee ya wapiiii weweee sikuheshimuui tenaaaa weeweee kafemarimaooo weweee hunakadihata ya ccm weseee
 
Mpwaaa hata wewee unatakakuniziboiaaa matumaini ya unclezakoo jamanii loh


cc.chaki
 
Back
Top Bottom