King'amuzi cha ting hakifai kabisaaa!!

King'amuzi cha ting hakifai kabisaaa!!

Aine

JF-Expert Member
Joined
Nov 1, 2010
Posts
1,603
Reaction score
489
Habari za leo wana JF.
Kwa kweli king'amuzi cha TING sio kizuri na nimekuwa nikikitumia kwa majuto kila siku na leo nimeona niweke wazi ili wahusika aidha wajirekebishe au waeleze kushindwa kwao katika digitali hii.

Ukiweka vocha siku za kazi j3-ijm) katika king'amuzi hiki unaweza kukaa hata masaa 3 kusubiri wa- activate, hivyo kwa muda wote huo tv inakuwa haionyeshi kabisa (ni black)!! na ikiwa umeweka vocha siku za weekend (jmosi-j2) ndio mbaya zaidi, kama ni jumamosi ujue tv utaanza kuangalia kuanzia j3 au j4 kabisa tena ni baada ya kuwapigia sana sana na wanakuambia uwarushie ujumbe uliopokea kwenye simu baada ya kunua vocha ili wa - activate, na zoezi hilo linachukua tena masaa kadhaa, kwa kweli wanaboa sana na binafsi sikipendi king'amuzi hicho kutokana na sababu hizo na nina mpango wa kukifungua na kukiweka stoo!!
 
Pole,hamia digitek..binafsi nimeridhika.
 
ulikuwa hujui?ndo zao c tumekipotezea .....tafuta easy tv o dish!
 
Pole,hamia digitek..binafsi nimeridhika.

Naomba nipe info zaidi kuhusu digitek mkuu, wanasema kuna local channels 10, na za nje pia ni 10, sasa hizo channels ni za aina gani?
 
Hata hao digitek hamna jipya,kwani kwenye hizo chanel za nje hakuna hata moja ambayo ni ya kulipia zote ni free to air,mfano CCTV 9,ARIRANG,FRANCE 24,ALJAZEERA,hakuna hata moja,ya maana!kwa mtazamo wangu,startimes wana package nzuri kulinganisha na ting,na digitec,sema tatizo lao ni picha kusimama simama,na hata wao unapolipia malipo ni dk 5,tu wanafungua.
 
Digitek ipo poa tu kwa tunaotaka local channels zote zinapatikana. Mambo ya kugeuza antenna kisarawe hayapo kabisa channel 24 zinatutosha hakuna cha vocha wala nini.
 
Naomba nipe info zaidi kuhusu digitek mkuu, wanasema kuna local channels 10, na za nje pia ni 10, sasa hizo channels ni za aina gani?
sidhani kama zinafika 20 kaka,na si mpenzi sana wa TV hivyo ni ngumu kukumbuka zote ATN,ITV,EATV,CAPITAL TV,TBC,CH 10,START TV,CLOUDS,AFRICAN SWAHILI(ISLAMIC), nje ni CCTV9,ALJAZEERA,EMANUEL TV,NHK JAPAN,AIRANG**,SETANTA
 
Digitek ipo poa tu kwa tunaotaka local channels zote zinapatikana. Mambo ya kugeuza antenna kisarawe hayapo kabisa channel 24 zinatutosha hakuna cha vocha wala nini.

Ni kweli mkuu,ule mpango wa " usisahau kunirekodia kile kipindi kikianza bado niko mbali ntachelewa kurudi" unahusika sana.
 
Hivi digtech ni king'amuzi au receiver tu ya kawaida?
 
hata hao digitek hamna jipya,kwani kwenye hizo chanel za nje hakuna hata moja ambayo ni ya kulipia zote ni free to air,mfano cctv 9,arirang,france 24,aljazeera,hakuna hata moja,ya maana!kwa mtazamo wangu,startimes wana package nzuri kulinganisha na ting,na digitec,sema tatizo lao ni picha kusimama simama,na hata wao unapolipia malipo ni dk 5,tu wanafungua.
startimes ki - kweli wanajitahidi, ila nao picha inastuck sana kiasi kwamba inapoteza mvuto wa kuangalia
 
Digitek ipo poa tu kwa tunaotaka local channels zote zinapatikana. Mambo ya kugeuza antenna kisarawe hayapo kabisa channel 24 zinatutosha hakuna cha vocha wala nini.
ngoja niitafute
 
nilichokigundua ni kwamba, Tz tulikuwa hatujajipanga kuingia ktk mfumo huu mgeni kwetu wa digitali, ndio maana kila king'amuzi kina kasoro fulani, labda hicho cha digitek ambacho sikijui
 
Startimes imetulia sasa full bata
 
mkuu digtek ina channel ngapi?

sidhani kama zinafika 20 kaka,na si mpenzi sana wa TV hivyo ni ngumu kukumbuka zote ATN,ITV,EATV,CAPITAL TV,TBC,CH 10,START TV,CLOUDS,AFRICAN SWAHILI(ISLAMIC), nje ni CCTV9,ALJAZEERA,EMANUEL TV,NHK JAPAN,AIRANG**,SETANTA

Ninazozikumbuka ni hizo mkuu.
 
Mimi nina decoder ya TING. Hayo matatizo yanayowakumba sisi hauyajui. Tunapata channels vizuri.
 
Back
Top Bottom