Kinana , Katibu mwenezi wa CHADEMA ona hapa .

Kinana , Katibu mwenezi wa CHADEMA ona hapa .

Mpaka Kieleweke

JF-Expert Member
Joined
Feb 27, 2007
Posts
4,132
Reaction score
1,582
Ameitaja CHADEMA 16 NA CCM 12 Kwenye taarifa yao hii iliyotoka uhuru na ipo pia kwenye blog yao:

CCM wanavyosaidiakueneza chadema :

Asema viongozi wakewamekubuhu wa ubinafsi
*Wanajali maslahibinafsi ya Chama chao badala ya Watanzania
*Awatakja Watanzaniakuwapuuza
[TABLE="class: MsoNormalTable"]
[TR]
[TD="bgcolor: transparent"]
​
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="bgcolor: transparent"]
Kinana akihutubia mjini Morogoro leo.Picha: Bashir Nkoromo​
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
NA BASHIR NKOROMO,MOROGORO
KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (
CCM), Abdulrahman Kinanaameisasambua Chadema na kusema ni chama ambacho daima kimekuwakikiweka mbele maslahi yake binafsi kuliko ya Watanzania.

Amesema viongozi wa chama hicho wamekubuhu kwa udikteta kiasi cha kujiona waondio wanajua kila jambo kuliko watu wengine hata mwenzao wa chama cha upinzaniikitokea ana mawazo au msimamo wasioutaka au ameipongeza serikali kwaohuonekana ni msaliti na kibaraka wa
CCM.

Akihutubia leo mkutano mkubwa wa hadhara uliofanyika jana mjini hapa,Kinana,alisema kuwa
Chadema ni balaa kwa nchi naa watu kwani viongozi wakewamekuwa ni watu wa kuhubiri machafuko badala ya mshikamano uliozoelekaTanzania.

Alisema kutokana na umangimeza wao sasa
Chadema kimeanza kuigawa nchikwa kutumia sera ya ukanda licha ya kwamba sera hiyoi ni kinyume cha katiba yanchi na watu wake.

"Ninapenda leo niwaelezeni ndugu Watanzania
Chadema ilivyojawa na ubinafsi,wamekuwa wakiwakukusanya Watanzania na kuwagawa kwa sera yao ya majimbo. hilisi mara ya kwanza maana katika kipindi cha siku za hivi karubuni walitangazawazi kuigawa nchi kwa kutaka
kujitenga kanda ya Kaskazini eti ili iwe chini ya utawala wao", alisemaKinana.

Kinana alisema
CCM kama chama kilichoingia mkataba na Watanzaniahaiwezi katu kukaa kimya na kuona hali hii ikitokea, kila mara tumekuwatukihubiri amani na mshakamano lakini Chadema hili limewashinda jamboambalo alisema ni dalili kwamba viongozi wa Chadema wameingia katika siasakwa malengo yao binafsi.

"
CCM itaendelea kusema ukweli kwa kila jambo na walahaitaficha hata likiwa siyo la kufurahisha wanachama wake ili mradi ni lakweli, tofauti na hawa Chadema, lazima Watanzania muwe makini nao kutokana naaina ya siasa na matendo yao wanayojinasibvu nayo" alisema Kinana.

Vurugu za
Chadema
Kinana alisema kuwa
Chadema wamekuwa ni watu wa maajabu na vurugu kubwanchini, na katika hilo alitoa mfano ya mambo ambayo wanayafanya bungeni.

"Chadema kazi yao ni vurugu tu, utadhani wao ndiowamekuwa kambi ya upinzani wa kwanza bungeni katika nchi hii. Walikuwepowapinzani kabla yao lakini kama CUF na Kina Mrema (Augustine Mrema) enzi zaNCCR Mageuzi lakini hamkupara kushuhudia vituko kama

hawa
Chadema ambao wanajiona wao ndio kila kitu. Wanatoavitisho kila siku kwa Serikali hata kumtukana mkuu wa Nchi bila kujali kwambani kiongozi ambaye amefika pele kwa kuchaguliwa na idadi kubwa yaWatanzania", alisema.

"Wanabeza wapinzani wengine , wakiona mpinzani anapongeza kazi iliyofanywana
CCM wanaanza kumshambulia.Hakuna anayejua zadi ya Chadema .Wanamtukana Rais, wanaushambulia usalama wa Taifa, wanashambuliavyombo vya usalama,"alisema Kinana

"Hawa jamaa ni watu wa ajabu sana, kila kitu wanajua wao wenginehawajui.Wakigombana katika chama chao utasikia kuna mkono wa
CCM. Sijui ni watu wa aina gani , wanafanya mambo ya ajabu sana kiasicha kushangaza,"alisema.

Kinana alitoa ushauri kwa
Chadema kuwa na uwezo wa kutafuta ufumbuzi wa matatizoyao kuliko kutumia muda wao mwingi kila jambo ambalo linakwenda kombo kunyooshavidole kwa CCM.

"CCM tuna changamoto zetu nyingi, lakini tunatatuamatatizo yetu wenyewe hatupotayari.Tuna makundi ndani ya chama lakini hayo ndiomambo ya siasa,"alisisitiza.

Mchakato wa Katiba mpya
Kinana alisema pamoja na kazi nzuri ambayo imefanywa katika mchakato wa Katibampya, kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni ametoa hotuba yake ambayo inaoneshawazi hakuna ambacho kimefanyika katika mchakato huo.

Alisema kuwa kiongozi wa kambi ya upinzani Freeman Mbowe akiwa bunge ametumiamuda wake mwingi kuzungumzia mchakato wa katiba mpya na kubwa katika hotubayake kuwa haufai.

"Simsingizii kiongozi wa Kambi ya upinzani bungeni, ndani ya hotuba yakeameeleza wazi kuwa waliopewa dhamana ya kukusanya maoni ya Katiba mpya hawanaujuzi.Hii si kweli, waliopewa dhamana hiyo ni watu ambao wanaifanya kazi hiyokwa uadilifu,"alisema.

Alisema
Chadema ni watu binafsi ambao wao wametawaliwa na urohomkubwa na wao kazi ni kuangalia maslahi zaidi na ni si maslahi ya nchi.

Ziara yake Morogoro
Kinana alisema kuwa ziara yake amejifunza mamb mengi lakini kubwa na msingiambalo lipo kwa chama hicho kitahakikisha kinatafuta ufumbuzi wa matatizo yawananchi na hasa migogoro ya ardhi, mipaka na huduma za jamii ambazo nazo nichangamoto kubwa kwa maeneo mbalimbali.

"Ziara yangu na viongozi wengine wa chama chetu ambayo tuimefanya katikawilaya zote za Morogoro tumeona changamoto nyingi.Tumetafuta ufumbuzi wamatatizo lakini mengine yanapatiwa ufumbuzi baada ya kukaa na viongozi wa ngazimbalimbali wa chama na kisha kutoa maagizo kwa Serikali kutekeleza,"alisema.

Agizo kwa wabunge
CCM
Katibu Mkuu huyo wa
CCM, alitumia nafasi hiyo kwa kuwataka wabunge wa CCM kutembea kifua mbele kwani chama chao kinafanya kazi kubwa lakinialiwataka wawe makini na Chadema na kuwataka kutowasikiliza kwani sasa imetosha.

Alisema
Chadema wamekuwa wakisikiliza muda mrefu ndani ya Bungena kuna wakati wabunge wa CCM walichukia baada ya Rais Jakaya Kikwetekukubali kukutana nao kujadili mchakato wa Katiba Mpya.
Posted byBashir Nkoromoat9:33 AM0 comments
Email ThisBlogThis!Share to TwitterShare to Facebook
huyu badala ya kuzungumzia chama chake alienda kukijenga chadema , nashauri apewe kazi ya uenezi.......
 
Hawajui kama ndo CDM inazidi kuimalika. Wacha wahangaike kwa sasa wakidhani ndo wanabomoa CDM KUMBE NDO WANASAIDIA KUJENGA CHAMA BILA MALIPO YOYOTE. NAPENDEKEZA VIONGOZI WA CDM WAWAPELEKEE MAGAMBA ZAWADI YA VITENGE NA CHUMVI KWA KAZI KUBWA WANAYOIFANYA KUKIJENGA CHADEMA.
 
alikuwa anatambulisha CHADEMA kwa wanachama wake ambao ni wazee na mara zote hawashiriki mikutano ya CHADEMA , jana aliwapa kiu wakisikia kuna mkutano wa chadema wataenda ili kuona hao wakoje mbona walitangazwa sana ? anahitaji zawadi kwa kazi kubwa ya kutangazia taifa juu ya chadema tena livu , na hapa gazeti lao na blog yao pia inaendelezaz matangazo kwa wanachama wao ......

Hawajui kama ndo CDM inazidi kuimalika. Wacha wahangaike kwa sasa wakidhani ndo wanabomoa CDM KUMBE NDO WANASAIDIA KUJENGA CHAMA BILA MALIPO YOYOTE. NAPENDEKEZA VIONGOZI WA CDM WAWAPELEKEE MAGAMBA ZAWADI YA VITENGE NA CHUMVI KWA KAZI KUBWA WANAYOIFANYA KUKIJENGA CHADEMA.
 
blog yao inatembelewa na watu 154,414 , hivyo leo ameitangaza CHADEMA mara 16 kwa waliotembelea blog hiyo leo ,
 
Mwizi wa nyara za taifa apewe uenezi wa CDM? Hapo sikubaliani na wewe.
Hawa hawana la kuongea, angekuwa na sera angetupatia na angeongelea mambo ya Chama Chake kwa sababu wao ndiyo walioshika dola lolote likitokea wataulizwa wao au alitaka kutuambia wizi wa Pembe za ndovu tukamuulize Dr. Slaa?
 
historia yake Kinana:

"KAMPUNI ya uwakala iliyosafirisha kontena lililokuwa na meno ya tembo ambayo yalikamatwa nchini Vietnam, inamilikiwa na Mjumbe wa Kamati Kuu (CC) ya CCM, Abdulrahman Kinana, imefahamika.

Taarifa zinaonyesha kuwa Kinana anamiliki hisa 7,500 kati ya 10,000 za kampuni hiyo inayoitwa Sharaf Shipping Company iliyosajiliwa Dar es Salaam.

Mshirika mwenzake katika kampuni hiyo, Rahma Hussen anamiliki hisa 2,500 zenye thamani ya shilingi 1,000 kila moja.
Kwamujibu wa taarifa za usajili, wamiliki wote wawili, Kinana na Rahma wanapatikana kwa S.L.P 10910, Kiwanja Na. 403 Mtaa wa Tosamaganga, Msasani Peninsular, Dar es Salaam.

Nyaraka zilizopo katika ofisi ya Wakala wa Usajili wa Makampuni na Biashara (BRELA), zinaonyesha kuwa kampuni ya Kinana ilisajiliwa Oktoba 2003 na kupewa hati Na. 47221.
 
Hii hotuba haijaongelea matatizo hasa ya watanzania na watu wa Morogoro hivi ni kweli hotuba hii ni yake katibu mkuu wa chama DUME
 
kitu kizuri huzungumzwa mara nyingi na ndiyo maana hata ccm sasa wamegungua CHADEMA ni chama makini wasipokiongelea sana wazomewa na watanzania big up kinana. wewe piga piga tu bora ushike mshiko wako na kampuni zako zinaedelea na magendo bila kukamatwa
 
Hauwezi kwenda kwenye ibada halafu jina la shetani lisitajwe.
 
Tunashukuru wanaipa promo CHADEMA bila kujijua.
 
Back
Top Bottom