katibu mkuu wa ccm mwenye ile meli iliyokamatwa na pembe za ndovu mchini China leo amekiri udhaifu na kushindwa kwa chama anachokiongoza.
Akiwa kwenye ziara ya kichama huko Chunya mkoani Mbeya wakati akiwahutubia wananchi alisema "Wananchi mkiona mambo hayaendi vizuri mnailaumu ccm na kuona haifanyi chochote, hiyo ni kweli na mko sahihi".
kauli hii pamoja na ile kauli yake pamoja na Nape kusema kuwa kuna mawaziri mizigo ni sawa na kuwaambia wananchi kuwa hata aliye wachagua na kusimamia baraza la mawaziri naye ni mzigo, kwa maana hiyo hata aliye peperusha ilani yenye ahadi ambazo leo hii hazitekelezeki naye ni mzigo tu maana wananchi wanapo lalamika kuwa serikali haifanyi chochote ni matunda ya kuwa na kingozi legelege ambaye ni mzigo.
mwalimu Nyerere aliwahi kusema "Viongozi legelege huzaa serikali legelege" na ndio tunacho kishuhudi leo na ndio Kinana anacho kikiri mbele ya wana Chunya.
kama Kinana anakiri, watetezi wa CCM wanaoshinda na kutukana mitandaoni wanataka ushuhuda wenye ushahidi gani?