Kinana apongeza ziara ya Rais Samia Marekani

SautiYaMnyonge

JF-Expert Member
May 13, 2018
439
742
Na Mwandishi Wetu,
Moshi, Kilimanjaro.

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Tanzania Bara, Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana, amepongeza ziara ya Rais Samia Suluhu Hassan nchini Marekani kwa kusema kuwa italeta faida kubwa kwa nchi.

Amesema ziara hiyo imemkutanisha na viongozi wakubwa akiwemo Makamu wa Rais wa Marekani Kamala Harris ambaye nchi yake Ina ushawishi mkubwa duniani.

Kinana ameyasema hayo katika mkutano wa ndani wa chama hicho mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro akiwa katika ziara ya kikazi kukagua uhai wa chama na kujitambulisha baada ya kuchaguliwa kushika nafasi hiyo hivi karibuni.

"Sasa hivi anafanya ziara nje huko, kwa kukutana na wawekezaji, wafanyabishara, wafadhili na watoa mikopo ili tuweze kupata fedha nyingi zaidi kwa maendeleo ya taifa letu na kukuza uchumi kupitia biashara na uwekezaji." Amesema Kinana

Kinana aliendelea kusema "Rais yuko Marekani, ameonana na Makamu wa Rais wa Marekani. Marekani ni nchi kubwa, Marekani Ina kauli duniani, Marekani ni mshiriki wetu wa maendeleo katika sekta mbalimbali zinazowagusa wananchi,"

Amesema Rais Samia pia amekutana na viongozi wa Benki ya Dunia na Shirika la Fedha duniani (IMF), Taasisi ambazo ni washirika muhimu wa maendeleo na uchumi wa Tanzania, hivyo anastahili pongezi.

IMG-20220426-WA0047.jpg
IMG-20220426-WA0049.jpg
IMG-20220426-WA0066.jpg
IMG-20220426-WA0059.jpg
IMG-20220426-WA0055.jpg
IMG-20220426-WA0064.jpg
IMG-20220426-WA0039.jpg
 
Unafikiri utasema maneno gani zaidi ya kumpongeza kwani Nani hajui kuwa amekupa ulaji ulionao Sasa hivi ,kwa hiyo hatushangai wala
 
Kinana tuambiwe kama nchi ,tumetumia shilingi ngapi kuandaa huo mradi,tutapata shilingi ngapi.

lakini kusema Tu tutapata faida haieleweki maana miaka iliyopita tuliambiwa tutembee kifua mbele tunafedha nyingi hivyo hatuna wasiwasi na maisha.

Leo CAG amekuja na uozo wa matumizi na wizi wa kutisha hivyo kinana tuambiwe ukweli wako
 
Mzee naona yupo active...yaonekana kaletwa rasmi kuhakikisha wale wahuni wa chatial wananyamaza na kutii mamlaka.

Amesema wazi kabisa kwamba nchi iliharibiwa vibaya na wahuni wachache.
 
Back
Top Bottom