Kinana anaongopa

kasimba123

JF-Expert Member
Apr 18, 2010
1,753
811
Kinana ajibu mapigo

lC.gif
Mwandishi Wetu​
Septemba 22, 2010
rC.jpg

KINYUME cha utamaduni wake wa muda mrefu wakati wa kampeni, Chama Cha Mapinduzi (CCM) sasa kinajibu kila hoja anayotoa mgombea Urais kwa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Wilbroad Slaa, Raia Mwema imethibitisha.
Kwa muda mrefu sasa CCM kimekuwa chama chenye uhafidhina katika baadhi ya taratibu ambazo zimegeuzwa utamaduni, lakini sasa kinapata kazi ya ziada kujibu hoja za Dk. Slaa ambaye dhahiri anakisumbua.
Huko nyuma CCM imekuwa ikijibu hoja za wagombea urais wa Upinzani kupitia kwa wapiga debe wake lakini safari hii, imekuwa ikitumia viongozi wake rasmi kwa kazi hiyo, akiwamo Mwenyekiti wa Kampeni wa chama hicho, Kanali mstaafu Abdulrahman Kinana na Katibu Mkuu, Yusuf Makamba.
Hoja za karibuni ambazo CCM imezijibu rasmi ni pamoja na ile ambayo Dk. Slaa anasema ni kutaka kupunguza mishahara ya wabunge na mshahara wa Rais; kutangaza mpango wa kujenga reli kutoka Mwanza hadi Dar es Salaam.
Katika kujibu hoja hizo, Kinana ameliambia Raia Mwema katika mahojiano na gazeti hili kuwa hoja ya kukata mishahara wabunge na Rais, haitawezesha kupata fungu kubwa la kutatua matatizo ya wananchi.
Katika mahojiano hayo yaliyochapishwa kwenye gazeti hili, Kinana anasema kama wabunge watakatwa asilimia 15 ya mishahara yao kwa idadi yao



zitapatikana Sh milioni 225 ambazo hazitasaidia sana malengo ya kuinua huduma za wafanyakazi kama Dk.Slaa anavyodai.
“Sh 750,000 mara watu 300 ni unapata Sh. milioni 200 na zaidi, ni fedha ndogo sana, sijui unawezaje kuboresha mishahara ya wafanyakazi au mazingira yao kwa fedha hizo. Kwa hiyo, ni kuchukua vitu vidogo vidogo ambavyo masikio mwa wananchi vinaleta raha lakini havina tija.
“Amesema nakata mshahara wa Rais kwa asilimia 20, mimi nilifikiri anaondoa kabisa mshahara wa Rais labda angeeleweka vizuri zaidi. Rais yeyote duniani, hasa Rais wa Tanzania hana mshahara, Rais anaishi kwa marupurupu zaidi kuliko mshahara.


“ Sasa anasema ataondoa asilimia 20 ya mshahara wa Rais, tuchukue kwa mfano, Rais analipwa Sh milioni 10 ina maana ataondoa Sh milioni mbili tu kwa mwezi, kwa mwaka ni Sh milioni 24. Huu ni udanganyifu,” alisema.
Katika hatua nyingine, Kinana alimkingia kifua Spika wa Bunge, Samuel Sitta, ambaye naye alishambuliwa na Dk. Slaa kwamba ana matumizi ya anasa.
“Anasema Spika wa Bunge anajilipa marupurupu makubwa pamoja na kujenga ofisi yake kama Mbunge wa Urambo.
“Jambo moja ambalo Watanzania hawajui na ningependa walijue ni kwamba mara baada ya haya yote yanayofanyika bungeni, mishahara anayosema mikubwa, kujenga ofisi za wabunge na kuanzisha Mfuko wa Jimbo haya ni mapendekezo ambayo yameletwa na kukubaliwa na Dk. Slaa mwenyewe.
“Kwa nini? Spika wa Bunge aliunda Tume ya watu saba kuangalia uendeshaji wa Bunge pamoja na maslahi ya wabunge, Dk. Slaa alikuwamo.
“Hiyo kamati ilikuwa na watu saba, CCM watano na wawili kutoka Kambi ya Upinzani Bungeni, ambaye ni Dk. Slaa na Hamadi Rashid Mohamed. Wamezunguka nchi mbalimbali duniani kuangalia wabunge wana maslahi gani, wana uwezo kiasi gani, wanahuduma kiasi gani na marupurupu kiasi gani.
“Sasa Dk. Slaa na wenzake ndio waliopitisha mapendekezo haya ambayo analalamikia. Alikuwamo kwenye mapendekezo hayo yaliyopitishwa bungeni kwa ushawishi wake.
“Haiwezekani akubali hayo mapendekezo halafu arudi kwa wananchi kuwaambia kwamba hiki kinacholipwa kwa wabunge ni kibaya,” alisema Kinana na kuongeza:
“Na alikuwa anapokea mshahara na hata siku moja sijasikia akikataa mshahara au kuchukua na kupeleka kwenye NGO fulani inayosaidia watu masikini. Sasa huko ni kuhadaa watu.”
Akizungumzia ahadi ya Dk. Slaa kujenga reli na kununua treni yenye kasi, alisema haiwezekani kujenga na kupata treni yenye uwezo wa kutembea kwa saa tatu kati ya Mwanza na Dare es Salaam.
“Kuna treni inaitwa bullet train ya Japan ambayo kwa mwendo huu anaosema Dk. Slaa itachukua karibu saa 10.
“Kuna treni ya Kifaransa inaitwa TGV, yaani treni inayokwenda kasi sana kuliko nchi yoyote za Ulaya na kwa hesabu nilizopiga (kutoka Dar-Mwanza) inachukua zaidi ya saa sita lakini yeye amesema saa tatu. Huku ni kuhadaa watu, unajua unapokaa majukwaani si vizuri kudanganya watu na ndiyo maana nasema Kikwete (Jakaya, mgombea Urais kwa CCM) atapa kura nyingi,” alisema.
Kwa upande mwingine, Kinana amedai kuwa CHADEMA ni chama chenye Katiba inayolinda siasa za kimwinyi na kibepari, na si siasa za ujamaa kama ambavyo Dk. Slaa amekuwa akiitumia kutoa ahadi zake jukwaani.
“CHADEMA kinaamini katika mrengo wa kulia, chama kinachoamini siasa na sera za kibepari na utakumbuka wakati kinaanzishwa CHADEMA na waasisi wake walikuwa wakipinga sera za siasa za ujamaa, wakitetea sera za ubepari.
“Walikuwa wakipinga serikali kumiliki mashirika ya umma au kampuni, wakisema si sawa, ni vizuri kuyaweka kwenye mikono ya watu binafsi, kutoa huduma za afya na elimu bure serikali isifanye hivyo.
“Hata ukiangalia Katiba yao ndivyo inavyosema. Inazungumza juu ya siasa za kuendeleza watu binafsi na si wananchi kwa ujumla. Sasa kauli anazotoa Dk. Slaa hadharani hazifanani na maudhui ya kimsingi yaliyoko kwenye Katiba ya CHADEMA.
“Wako karibu zaidi na vyama vya Republican (Marekani), Conservative (Uingereza) na vyama vya kimwinyi vya Uholanzi, Ujerumani na Australia, kwa hiyo wasidanganye wananchi,” alisema.


Raiamwema




Hapa hakuna utafiti kabisaaa alioufanya kinana kwenye hii hoja


millioni 225 kwa mwezi ni ndogo! unaweza kuchimba visima vingapi au kununua madawati mangapi?


Kwa sasa duniani Treni inayoenda kasi sana iko China na sio ufaransa na haiwezi kuchukua saa 6 kama anavyosema
 
Back
Top Bottom