Kinachoua lounge na bar nyingi Dar ni huduma mbovu kwa wateja

hata Mwanza kuna Bar kubwa kidogo nilienda nilipofika mtu niliyekuwa naye akaomba tukae nje kwa sababu hataki kelele,akaja muhudumu wa kiume faster nikaagiza robinson yangu kubwa na binti kaagiza maji tu akagoma kula,baada kama ya nusu saa akaja muhudumu yule akaniomba nilipie sababu anamaliza shift,nikampa 27 yake nikaongeza na buku tano ya k vant ndogo na akaleta vizuri akasepa
kimbembe ni nilipotaka kuagiza vinywaji vingine,ilibidi niamke kuwatafuta wahudumu,nilipowapata nikamuagiza mmoja k vant ndogo akaomba pesa nikamwambia nitakupa mezani kwangu,nikamuelekeza na meza,aise nilikaa kama dkk 40 haijaja ikabidi niamke nikamtafute sikumpata,nikamuagiza muhudumu mwingine alileta ila nili mind sana nikawanulia bear wahudumu wote pale na jamaa fulani waliomba pale nje alafu nikaondoka baada ya kuwachana vilivyo
niliona muhudumu kahisi sina pesa wakati nina kilo tatu mfukoni
Na hapo ukatumia sh ngapi?
 
Shida yenu ni misifa nakupenda kutukuzwa kama wafalme...jitu linaona mhudum yuko bize, kabla ya kusema lifuate kinywaji kaunta utalikuta limekazana kuita mhudum kama limefungwa kwenye kiti...nyoko zenu walevi mbwa.
 
sasa hapo umemkomoa nani? cha mno umemnufaisha mwenye biashara na walevi wengine. Nahisi utakuwa na vinasaba vya Kemondo wewe.

By the way ukitak huduma ya haraka nenda kanyewe duka la mangi. Huwa haina kuchelewa huduma.
mkuu sio kuhusu kukomoa,nimeondoka nimewafundisha uwajibikaji, yah kuhusu kwa mangi wana wengi wameshauri hivo
 
Kabisaa... huku mtaani sometimes kuna mambo ya Kishamba sanaa. Mimi sipendi kero so siku nikiamua kuji-spoil huwa naenda kula Gambe viwanja vikubwa. Na uzuri wa hayo maeneo watu mnaheshimiana sana yaani,
mnooo
mi kwakweli siwezi bora waone nna dharau..
Ukienda huko mambele ukishuka tu kwenue lift au lango la kuingilia unawakuta wadada au wakaka wamejipanga na menu zao wanakukaribisha wanakuonyesha pa kukaa popote unapopenda..
wanakupa Menu ukitaka kuagiza unaagiza , wahudumu wote wameweka majina yao kwamba hupati shida unaita tu "Mwanahamisi"
Kama Sea cliff ukikaa nusu saa meneja anakuja kukuuliza una enjoy? unataka nini tukuongezee nk

lakini huku mchangani unaingia mahala unakaa hata nusu saa hakufati mtu
 
Majuzi hapa JF Kuna mdau alipost kuhusu tips lounge kukosa wateja..leo mida ya saa kumi jioni nilienda lounge moja maarufu Sana dar ambayo kwa weekend ukichelewa kidogo unakosa parking au utapata tabu Sana kupata parking.

Nilipofika nilikaa kwenye Kochi huku nikiwa busy na simu lakini hakuna muhudumu aliyekuja baada Kama ya dk 20 Hadi nilipofanya jitihada za kumwita mmoja aliyekuwa anapita..,baada ya kunihudumia second round nikampa fedha hakurudushi chenji zaidi ya saa moja na nusu baadaye nikampata akarejesha. Then nikamwita mwingine nikasema nataka mtu wa chakula naye kapotea moja kwa moja hata hajamwita mtu wa chakula...duuh..nikasema hizo zote scenario tatu zimetokea kwangu, je ni wangapi wamepitia haya nayopitia.?

Je hizi bar na lounge zikiona watu wanajaa usiku wa manane wanadhani wamemaliza kila kitu.?

Sitataja hiyo lounge coz isije ikaonekana naiharibia biashara .
Tatizo lako ni kujisikia, unajipenda sana, unajibagua unapenda kukaa peke yako mezani, ukifika tu teua mmoja ukaenae mezani na muda si muda wengine watajipitisha na kukuita shem, kila sekunxe meza itafutwa vumbi.
 
we mzee bana umenikumbusha juzi nimeenda sehemu tulikuwa wanaume watatu mezani,tulichangamkiwa mno na wahudumu kila muda wanarudi,walipofika wanawake wetu kila muhudumu akawa busy
 
Anyway!Tusiwalaumu sana.Kuna siku nimekaa sehemu kama nusu saa sijasikilizwa.Nikatumia mbinu ya kumtaniatania muhudumu na kumuita anihudumie.Aliponihudumia,nikaanza kumdadisi kwa nini wanachelewa kuhudumia.Akawa mkweli kwamba;
-huwa wanawasoma wateja kwanza,
-wateja wengine wameenda kupata chakula tu na si vinywaji,
-huwa ni kama wanategeana kujua labda ana muhudumu anayemuhudumia siku zote,
-wanachukua tahadhari kwa sababu wateja wengine wakilewa ni watata kulipa bili,
-kuna wateja wenye visirani na gubu wanawakwepa.
-Na kadhalika na kadhalika...
Sasa yote hayo atayajuaje bila kuja kukusikiliza?!!
 
Sio huduma tuu

Siku za mwanzo wanawaweka wahudumu (pisi kali), wateja wapenda huduma zao watakuja na kujaza bar/lounge...baada ya muda mmiliki akishindwa maintain wahudumu alokuwa nao..wakiondoka na wateja wanaondookaaa
Manager anamtaka muhudumu / bosi anamtaka/ wateja wanamtaka /...etc na akishaanza kuwa close na manager/bosi wahudumu wengi wananza dharau watejaa
 
We limbukeni, kwani kila mtu lazima anywe Hennessy, alafu nyie ndio mmezijulia hizi pombe ukubwani, punguza dharau arif
Duh! Pombe nayotumia ni the dalmore ila nikienda viwanja vya kimaskini ni hennesy au jack daniels nina hela sana mkuu sijisifu ila narudia nina hela sana we arif wa kichaga
 
hata Mwanza kuna Bar kubwa kidogo nilienda nilipofika mtu niliyekuwa naye akaomba tukae nje kwa sababu hataki kelele,akaja muhudumu wa kiume faster nikaagiza robinson yangu kubwa na binti kaagiza maji tu akagoma kula,baada kama ya nusu saa akaja muhudumu yule akaniomba nilipie sababu anamaliza shift,nikampa 27 yake nikaongeza na buku tano ya k vant ndogo na akaleta vizuri akasepa
kimbembe ni nilipotaka kuagiza vinywaji vingine,ilibidi niamke kuwatafuta wahudumu,nilipowapata nikamuagiza mmoja k vant ndogo akaomba pesa nikamwambia nitakupa mezani kwangu,nikamuelekeza na meza,aise nilikaa kama dkk 40 haijaja ikabidi niamke nikamtafute sikumpata,nikamuagiza muhudumu mwingine alileta ila nili mind sana nikawanulia bear wahudumu wote pale na jamaa fulani waliomba pale nje alafu nikaondoka baada ya kuwachana vilivyo
niliona muhudumu kahisi sina pesa wakati nina kilo tatu mfukoni
Kilo tatu nayo ni hela?
 
mnooo
mi kwakweli siwezi bora waone nna dharau..
Ukienda huko mambele ukishuka tu kwenue lift au lango la kuingilia unawakuta wadada au wakaka wamejipanga na menu zao wanakukaribisha wanakuonyesha pa kukaa popote unapopenda..
wanakupa Menu ukitaka kuagiza unaagiza , wahudumu wote wameweka majina yao kwamba hupati shida unaita tu "Mwanahamisi"
Kama Sea cliff ukikaa nusu saa meneja anakuja kukuuliza una enjoy? unataka nini tukuongezee nk

lakini huku mchangani unaingia mahala unakaa hata nusu saa hakufati mtu
Tena sisi wanawake ndio tutafute pesa kwa nguvu zote, tukitaka kunywa na mashost tuende sehemu classic. Hakuna sehemu wanawake tunahudumiwa vibaya kama kwenye ma-Bar.

Kwanza unageuka competition kwa wahudumu wanakuona threat a.k.a kauzibe.
 
Na wanakuona kama umeenda kutega labda
mi Bar siwezi kwenda labda niwe na watu flani flani sio alone mana hamna cha kunivutia
 
Back
Top Bottom