Bunge la 11, mkutano wa 3, kikao cha 18
Maswali na majibu
Maswali na majibu
Zitto Kabwe: Anaeongea kwa sasa ni mbunge wa Kigoma mjini, Zitto Kabwe na anaelezea kuhitaji reforms kwenye sekta ya afya, amesema ruhusa ya kuajiri imetolewa lakini wizara haijaajiri. Pia amesema wafanyakazi wasichangie mifuko mingi na badala yake pesa wanazochangia kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii sehemu yake ziende kwenye bima ya afya.
Maria Kangoye: Anampongeza waziri na naibu kwa hotuba nzuri na kazi nzuri, ameona ujenzi na ukarabati wa hospitali. Pamoja na pongezi anaikumbusha serikali kuwa haijafikia lengo la Abuja kwa kutenga asilimia 15 kwa ajili ya sekta ya afya, ameongelea upungufu wa dawa katika hospitali za wilaya na anatolea mfano wilaya ya Magu mkoani Mwanza.
=====
Swali: Serikali ina mpango gani wa kujenga madaraja yalioyopo katika barabara ya Chamwino kuelekea kaskazini?
Majibu: Serikali kupitia wakala wa barabara TANROADS itaendelea kufayafanyia matengenezo madaraja haya ili yaweze kupitika wakati wote.
Swali: Shirika la ndege la ATCL ni la Tanganyika na Zanzibar? Na je Zanzibar ina hisa kiasi gani? Ni lini serikali italipa deni la kutua kwa ndege ya ATC kiwanja cha ndege cha Zanzibar?
Majibu: ATCL Inamilikiwa na Jamhuri ya muungano wa Tanzania kwa asilimia 100. Hakuna kiasi kilichoonesha kumilikiwa na Tanganyika wala Zanzibar.
Aidha deni la Ndege za ATC litalipwa punde tu baada ya kuhakikiwa, serikali pia ina mpango wa kulipa gharama zote za ndege za ATCL kutua Zanzibar.
Serikali ina mpango wa kufufua shirika la ATCL kwa kuanza kununua ndege mbili za Q400 ili kupunguza gharama za usafiri wa anga.
Serikali ina mpango wa kubadili uongozi wa shirika la ndege wa ATCL ili kuleta ufanisi zaidi.
Swali: Ni lini serikali italeta mapendekezo ya kubadili kifungu cha 20 cha sheria ya NECTA?
Majibu: Sheria haina kifungu hicho namba 20. Na sheria ya NECTA inampa waziri wa elimu kufanya maamuzi kwa niaba ya serikali. Aidha serikali haina mpango wa kubadili sheria hiyo.
Kuhusu suala la kubadili mfumo wa divisheni kwenda GPA, serikali ilishirikisha wadau.
Serikali italifanyiakazi suala la wanafunzi waliozuiliwa matokeo yao ya kidato cha nne kutokana na kushindwa kulipa fedha za mtihani huo.
Swali: Serikali ina mpango gani wa kuanzisha benki ya wafanyabiashara wakubwa na wadogo?
Majibu: Serikali haina mpango wa kuanzisha benki mpya ya wafanyabiashara wakubwa na wadogo. Serikali itajikita kuimarisha benki zilizopo ikiwemo benki ya kilimo na benki ya posta ambayo imeenea nchi nzima.
Serikali inaandaa sera ya taifa ya huduma za fedha kwa ajili ya kushughulikia kampuni zinazotoza riba kubwa, ifahamike kuwa serikali imejitoa katika uendeshaji wa shughuli za kifedha toka mwaka 1991