Naandika niko eneo la tukio kata ya Lugarawa wilaya ya Ludewa, mkoani Njombe. Walimu wakuu wametakiwa kukusanya kodi kwa walimu wao na raia wengine.
Iko hivi: katibu TAWALA wa wilaya aliwaita viongozi wa taasisi katika kata hiyo wakiwemo walimu wakuu. Akatoa maelekezo kuwa mtumishi yeyote ni mjasiriamali anatakiwa apewe kitambulisho bila kujali ana biashara au hana.
Hakutaka kupokea maoni zaidi kutoa siku moja vitambulisho hivyo viwe imegawiwa kwa walimu na raia wengine.
Naomba nijue kwingineko Tanzania kukoje? Hali hii ipo? Ni ni kwetu Ludewa tu?