Kina Ndiyo Mzee wengi serikalini - Rutabanzibwa

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,790
288,007
Kina Ndiyo Mzee wengi serikalini - Rutabanzibwa

Mwandishi Wetu Februari 27, 2008
Raia Mwema

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Maji, ambaye pia aliwahi kuwa Katibu wa Wizara ya Nishati na Madini, Patrick Rutabanzibwa, amesema kuna uoga mkubwa katika kutoa ushauri miongoni mwa watalaamu serikalini.

Amesema wakati mwingine wataalamu wanafikia mahali wanasema “basi bwana” akisisitiza kuwa, hicho ni chanzo cha kasoro katika mikataba ya baadhi ya miradi nchini.

Maelezo hayo ya Rutabanzibwa aliyatoa na kunukuliwa katika taarifa rasmi za Kamati Teule ya Bunge iliyochunguza mchakato wa zabuni kwa kampuni ya kuzalisha umeme wa dharura ya Richmond .

Kampuni hiyo ndiyo chanzo cha kuvunjwa kwa Baraza la Mawaziri la kwanza la Rais Jakaya Kikwete pamoja na kuteuliwa baraza jipya na Waziri Mkuu mpya.

“Siwezi nikasema matatizo yote ya TANESCO (Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania ) ni Serikali, lakini kwa mikataba hii mingine (hakuitaja) kama mtaalamu wa sekta ya nishati naweza nikasema kwamba kwa upande mmoja kunakuwa na labda uoga wa kushauri.

“Kwa upande wa wanaojua kama TANESCO kwa wakati mwingine wanafika mahali wanasema basi bwana. Hicho ni chanzo cha matatizo na huko kwetu wakati huko kwenye mgao kuna mashinikizo ya kila aina, wafanyabiashara wanapita pita huku na huku na wao wanatembeza maslahi.

“Hiyo ndiyo imekuwa kawaida ya miradi hasa mikubwa kwenye sekta na ninaweza nikasema wote tunawajibika kwa matatizo yanayotokana na hayo,” alisema Rutabanzibwa.

Kwa mujibu wa Rutabanzibwa, kama akichambua mkataba mmoja mmoja (ya Nishati), anaweza kusema wote tunaweza wanabeba lawama kwa maana ya Serikali na shirika lenyewe.
 
Back
Top Bottom