Kina Dada acheni tamaa. Ukipendwa pendeka. Soma kisa cha huyu Dada

Bubolwa Chura

JF-Expert Member
Dec 12, 2019
300
560
Naandika si kwamba nahitaji ushauri, ila nataka ujifunze kama unatabia hizi na unahisi mpenzi wako hakujui.

Nilianza mahusiano na huyu dada miaka miwili iliyopita kule Moshi. Kwasasa naishi Mbeya.

Sifa za huyu Dada ni mpole, mchangamfu, mkarimu na ukimuona utajua huyu ni mcha Mungu namba moja. Asili yake ni kule walikoongoza matokeo ya la saba hadi form four, bila shaka ulanzi unawasiaidia kuperform darasani.

Baada ya kuanza mahusiano naye na kukubaliana kwamba sasa ni wapenzi rasmi, nilianza kuona tabia ambazo zilinishangaza hasa kwa mdada anayejielewa.

Mfano, anaweza asikutafte siku nzima usipomtafta wewe. Hata kukubeep ili kama hana salio umpigie hawezi, hata kutuma sms hawezi. Kwahiyo kama siku hiyo uko busy ujue itapita bila bila. Niliongea naye kwa taaabu sana akajirekebisha kidogo, nilifanya hivo kwasababu mapenzi ni ya wawili si ya upande mmoja.

Tabia ya pili, baada ya kuwa naiba simu yake akiwa amelala niligundua anamawasiliano na wanaume kadhaa ambao kwa mazungumzo ni mpenzi wao. Nilimkanya akakubali kwa tabu sana na kuahidi atajirekebisha lakini kiuhalisia hajaacha, anachokifanya ni kufuta tu kila aina ya ushahidi kwenye simu yake, ingawa mimi huwa nikishika simu yake narudisha kumbukumbu zote kwahiyo naona.

Tatu, niligundua nimuongo muongo sana, anaweza akapigiwa simu na mtu mkiwa wote, akiulizwa yuko wapi atajibu niko nyumbani au nimesafiri niko mwanza. Katika uchunguzi wangu nikafuma sms akimdanganya mwanaume kuwa sipo nyumbani nipo Mbeya nimesafiri kikazi ila nikirudi nitakujulisha, wakati huo alikuwa amelala kwangu kwa siku kadhaa. Unaweza kumuuliza kitu kwa kumtega tu, atakudanganya mpaka utashangaa wakati huo ukweli unakuwa unaufahamu. Ukimuuliza uko wapi au leo ulienda wapi, utadanganywa dunia yote.

Nne, nikagundua hatosheki na alichonacho. Anatumiwa pesa na wanaume tofauti tofauti wengi sana ikiwemo watu niliowahi kuhisi ni wapenzi wake,nilipomuuliza, alikataa kuwa si wapenzi wake na wala hajapokea pesa yeyote. Niliwahi kumuuliza kwanini unapokea pesa za mtu flani au mnabiashara gani?, hakunipa jibu la kueleweka ingawa huyo mtu nilitumia kama mfano tu kati ya wanaume wengi anaopokea pesa na vitu mbalimbali kutoka kwao. Tabia hii iliniathiri sana kisaikolojia kwasababu, mwanzo nilikuwa na moyo wa kujitoa sana kwake kwa hali na mali, baada ya kugundua hii tabia, nikaacha kabisa.

Tano: Wakati naanza naye mahusiano niliwahi kusikia anamtu ingawa sikuwa na uhakika, nikamuukiza akasema huyo mtu sina mmahusiano naye wala simpendi. Ila katika uchunguzi wangu huyo mtu wanawasialiana na akisafiri analeta zawadi kama kawaida na huyu anapokea.

Sita: kuna tabia nyingi za ajabu ambazo kwakweli si sawa kuzitaja hapa, but in summary ni hizi.

Huyu mdada nilimpenda sana lakini kwa tabia hizi naona sio ridhiki. Nadhani nitakuwa sina hatia kwa hatua yeyote nitakayoichukua.

Siwezi nikaanzisha uhusiano halafu kila siku roho iwe juu juu tu. Lengo la uhusiano ni kuwa na mtu ili upate pumziko la moyo na kuridhisha mwili pindi unapohitaji kufanya hivo.

Nawasilisha: kumbuka sijaomba ushauri hapa, ni ushuhuda.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mmmh sasa apo ujui alikiweka kwene list kuna baadhi ya vitu ungesaidia kwene hilo kundi alilonalo? Yeye alikwambia anahitaji mpenzi?
 
Na bora ulivyosema huhitaji ushauri maana kutokana na ujumbe wako unaonekana wewe ndio una matatizo makubwa kuliko huyo mpenzi wako.
 
Kuwa serious na mahusiano pale utakapoona Yes, wote wawili mmeridhika na kila mmoja kweli ana nia na anaona umuhimu na uhitaji wa mwenzie.

Sasa hapo wewe ndio ulikuwa unataka mahusiano ila mwenzio hakuna
 
Pole sana!
Sababu zooooote hizo pamoja na ambazo hujazitaja bado tu upo nae??
Mimi mbili tu zingetosha kumzima
 
daah kaka sio peke yako!! hapa nilipo nimetoka kwenye break up na binti mwenye tabia kama ulizozianisha hapo. almost 90% zimefanana. ila mimi namshukuru mungu nakuaga mwepesi ku move on!! anaweza akakaa kimya siku nzima halafu utakapomtafuta hata hakwambii shida ilikua nini. nikaona kama napoteza muda hivi japo nilikua na sex nae kama kawaida. na mimi nikaanza kukaa kimya. cha ajabu hakunitafuta na yeye mpaka siku nne zikapita. kaja kunitafuta jana akiwa ana lalamika balaa na sms nyingi saana na ananigeuzia kibao kwa rafiki zangu ati mimi ndio kikwazo.kiukweli nimeshindwa kuishi nao hawa wanawake kama bible vile inasema

Sent using Jamii Forums mobile app
 
daah kaka sio peke yako!! hapa nilipo nimetoka kwenye break up na binti mwenye tabia kama ulizozianisha hapo. almost 90% zimefanana. ila mimi namshukuru mungu nakuaga mwepesi ku move on!! anaweza akakaa kimya siku nzima halafu utakapomtafuta hata hakwambii shida ilikua nini. nikaona kama napoteza muda hivi japo nilikua na sex nae kama kawaida. na mimi nikaanza kukaa kimya. cha ajabu hakunitafuta na yeye mpaka siku nne zikapita. kaja kunitafuta jana akiwa ana lalamika balaa na sms nyingi saana na ananigeuzia kibao kwa rafiki zangu ati mimi ndio kikwazo.kiukweli nimeshindwa kuishi nao hawa wanawake kama bible vile inasema

Sent using Jamii Forums mobile app
Polen sana wanaume
 
Kumtongoza mtu na akakubali haimaanishi kuwa ndyo mtakuwa pamoja wengine ni wa kupitia na kutembea kwa inavyoonekana wewe ndyo ulishindwa kung'amua upo kwenye mahusiano gani mwenzako alikuwa kwenye chapa ilale wewe ukaweka kibanda ukiona mtu awezi kukutafuta hadi umtafute iyo ni sababu moja wapo kubwa ya kumpitia na kumuacha maana yupo anayethaminiwa zaidi yako kwaiyo utajiumiza mwenyewe ukiendelea kujiweka kwake

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom