Kimwaga Ajutia Kutua Simba

Amavubi

JF-Expert Member
Dec 9, 2010
30,156
13,249

KIMWAGA (KATIKATI)
Sraika wa Simba, Joseph Kimwaga ametamka kuwa kati ya vitu ambavyo anajutia kwenye maisha yake ya soka, basi ni kutua kuichezea timu hiyo.
Mshambuliaji huyo alitua kuichezea Simba kwenye usajili wa dirisha dogo akitokea Azam FC kwa mkopo, ambapo amekuwa haonekani Simba kwa muda wa mwezi mmoja na nusu kutokana na kutokea sintofahamu kati yake na uongozi.
Kimwaga alisema alitarajia kufanya mengi makubwa akiwa na Simba, lakini ndoto zake zilikatishwa baada ya kutopewa nafasi ya kucheza.
Amesema Simba ndiyo waliyoifuata Azam kumuomba kwa mkopo na moja ya makubaliano ni kupata nafasi ya kucheza ili akuze zaidi kiwango chake, lakini baada ya kutua mambo yakabadilika.
“Sikutarajia kuyaona haya ninayoyaona hivi sasa Simba, kiukweli siamini, hivyo nimeona ni bora nikae nje ya timu ili nitulize akili yangu kuliko niwe ndani ya timu bila faida.
“Ninajuta kukubali kuja kuichezea Simba, inafikia kipindi ninafikiria vitu vingi sana kwa timu iliyokufuata wenyewe kukuomba kwa mkopo ukakubali halafu baadaye wanafanya vitu sivyo kabisa.
“Nimeona niwaachie timu yao na mimi nifanye mambo yangu mengine huku nikisubiria mkataba wangu miezi mitano na Azam kumalizika, kwa sababu nilifanya kila ninaloliweza ili nipate namba lakini nikashindwa,” alisema Kimwaga.
SOURCE: CHAMPIONI
 
Kwani kuchukuliwa kwa mkopo, ndio uhakika wa kucheza, hata kama kiwango kimeshuka...?
 
Kwani kuchukuliwa kwa mkopo, ndio uhakika wa kucheza, hata kama kiwango kimeshuka...?
halafu wanacheza 11 tu alipewa nafasi zenji akawa anajipasia na kuangalia chini....ukiligema unalinywa
 
Hayo maandishi inaonekana ni uswahili tu! Kama mchezaji anapata stahili zake zote, inakuwaje ajiweka pembeni.. Labda kama alikuwa halipwi mshahara, kucheza sio ishu.. Hizo ni story za kijiweni
huyu alipoifunga Yanga akajiona mchezaji mkubwa sana kama ilivyokua kwa Bahanuzin wa Kagame
 
Inategemea na ushindani ulioukuta. Huwezi kupangwa tu eti kisa umechukuliwa kwa mkopo, afanye jambo la ziada kumshawishi kocha. Mbona Simba imemtoa kwa mkopo Miraji Adam na anafanya vyema Coastal Union?
 
safi sana na hata akina Mbaraka, Kipalamoto, Seseme na EDWARD na wengineo wanacheza
Inategemea na ushindani ulioukuta. Huwezi kupangwa tu eti kisa umechukuliwa kwa mkopo, afanye jambo la ziada kumshawishi kocha. Mbona Simba imemtoa kwa mkopo Miraji Adam na anafanya vyema Coastal Union?
 
KIMWAGA (KATIKATI)
Sraika wa Simba, Joseph Kimwaga ametamka kuwa kati ya vitu ambavyo anajutia kwenye maisha yake ya soka, basi ni kutua kuichezea timu hiyo.
Mshambuliaji huyo alitua kuichezea Simba kwenye usajili wa dirisha dogo akitokea Azam FC kwa mkopo, ambapo amekuwa haonekani Simba kwa muda wa mwezi mmoja na nusu kutokana na kutokea sintofahamu kati yake na uongozi.
Kimwaga alisema alitarajia kufanya mengi makubwa akiwa na Simba, lakini ndoto zake zilikatishwa baada ya kutopewa nafasi ya kucheza.
Amesema Simba ndiyo waliyoifuata Azam kumuomba kwa mkopo na moja ya makubaliano ni kupata nafasi ya kucheza ili akuze zaidi kiwango chake, lakini baada ya kutua mambo yakabadilika.
“Sikutarajia kuyaona haya ninayoyaona hivi sasa Simba, kiukweli siamini, hivyo nimeona ni bora nikae nje ya timu ili nitulize akili yangu kuliko niwe ndani ya timu bila faida.
“Ninajuta kukubali kuja kuichezea Simba, inafikia kipindi ninafikiria vitu vingi sana kwa timu iliyokufuata wenyewe kukuomba kwa mkopo ukakubali halafu baadaye wanafanya vitu sivyo kabisa.
“Nimeona niwaachie timu yao na mimi nifanye mambo yangu mengine huku nikisubiria mkataba wangu miezi mitano na Azam kumalizika, kwa sababu nilifanya kila ninaloliweza ili nipate namba lakini nikashindwa,” alisema Kimwaga.
SOURCE: CHAMPIONI

Hivi vitoto vipuuzi kweli. Vinaacha kujibidiisha na mazoezi ili vimshawishi Kocha vyenyewe kutwa ni kupiga tu majungu. Kwanza hata kutua kwake Simba pia ni bahati lakini pia hata sisi wana Simba Sports Club tumejuta kumchukua mchezaji wa aina yake ambaye hajui mpira. Halafu mwambieni aache tabia ya kupenda kuwaroga wenzie! Sasa uone kuwa huyu dogo ana nuksi ya kutukuka yaani anaroga lakini na kwenyewe pia anashindwa kupata namba kikosini. Na nyie Viongozi wa Simba Sports Club yangu siku nyingine msituletee " utumbo " wa aina hii tafadhali.
 
Angetumia mguu kuongea badala ya mdomo ingeweza kusaidia zaidi.

Kijana huyu bado ni mdogo na ana uwezo mzuri tu, anapaswa kuongeza juhudi na kuwa mvumilivu.
Kuna watu wengi walikuwa wanakaa benchi pale Simba kama akina Novati Lufunga lkn leo ni wanavuna matunda ya uvumilivu.
 
WACHEZAJI WATANZANIA WANA MATATIZO SANA. ANAWEKWA BENCHI HALAFU ANALALAMIKA BADALA YA KUFANYA MAZOEZI KWA NGUVU. HAPO HAPO SIMBA KUNA MFANO MDOGO TU WA NOVATI LUFUNGA, MWINYI KAZIMOTO NA JONAS MKUDE WAKATI WA KERR WALIKUWA BENCHI HAWACHEZI MARA KWA MARA LAKINI WALIFANYA MAZOEZI KWA NGUVU NA SASA WANACHEZA. PIA HUYO DOGO UKIANGALIA SANA AKIPANGWA ANATAKA AFUNGE YEYE MWENYEWE HATA KAMA YUPO KATIKATI YA UWANJA ANASAHAU KUWA YUPO NA WENZAKE 10 UWANJANI. HANA USHIRIKIANO NA WENZAKE UWANJANI ANANG'NG'ANIA MPIRA HATA SEHEMU ISIYOSTAHILI BADALA ATOE PASI. AKIPUNGUZA HIZO DOSARI NDOGO NDOGO NA AKIJITAMBUA ATAKUWA MCHEZAJI MZURI KWANI UMRI BADO UNAMRUHUSU.
 
Back
Top Bottom