Kimenuka: Wasira amshukia Lissu kwa mambo manne

Rais2020

JF-Expert Member
Jul 14, 2016
3,248
5,537
Rejea Tundu Lissu: Nmenusurika kupigwa na Steven Wassira, ngumi ya kwanza nliikwepa

Wasira ajibu:
Waziri wa zamani katika Serikali ya Awamu ya Nne, Stephen Wasira amemshukia Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu kwa mambo manne.

Moja ya mambo ambayo Wasira amesema ni kwamba mbunge huyo wa Chadema hana heshima kwa viongozi wakuu wa nchi.

Wasira alisema hayo baada ya Lissu kudai kuwa alinusurika kupigwa na kada huyo wa CCM wakati wa vikao vya Bunge mjini Dodoma, habari ambayo ilichapishwa jana na Mwananchi.

Akijibu tuhuma hizo, Wasira (pichani) alisema Lissu anaongea kama vile hayuko sawasawa kwa sababu yote aliyoyasema ni uongo, hajui yalitokea wapi na hajui sababu zake.

Wasira alisema hakuna mtu mwenye akili timamu anayeweza kumtukana Rais wa Awamu ya Kwanza, Mwalimu Julius Nyerere, lakini alimshangaa Lissu alipothubutu kufanya hivyo wakati wa Bunge Maalumu la Katiba.

Alisema Lissu pia alimtuhumu mambo ya uongo Mwalimu Nyerere kwa kudai alighushi saini ya mwasisi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Abeid Amani Karume kwenye hati ya Muungano. “Hata wapinzani wenzake walimshangaa,” alisema Wasira.

“Huyu mtu amethubutu kuwatukana maraisi waliopita, kamtukana (Benjamin) Mkapa, kamtukana (Jakaya) Kikwete ambaye alimkaribisha Ikulu na kunywa juisi huku amejikunyata, sasa anamtukana Rais (John) Magufuli. Mimi si msemaji wa Magufuli, lakini huyu Lissu amekuwa anamtukana,” alisema Wasira huku akisisitiza kuwa Lissu hana heshima na maadili.

Wasira alisema kutokana na vitendo hivyo inaonekana Lissu ana matatizo kwa kuwa mtu aliye kamili hawezi kufanya vituko vya aina hiyo.

Pia, alimshangaa Lissu kuwa mstari wa mbele kumsafisha kwa maelezo mazuri Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, wakati alikuwa wa kwanza kumtuhumu kwa kumuita fisadi kiongozi huyo alipokuwa CCM, akisema huo ni uhalisia wa mtu ambaye mara zote amekuwa hasemi kweli.

“Nashangaa leo ndiye amekuwa mstari wa mbele kumsafisha kwa brashi ya chuma baada ya Lowassa kujiunga nao,” alisema huku akibainisha kwamba hizo ndiyo dalili za mtu asiyesema kweli.

Alisema Lissu kumsafisha Lowassa inaonyesha kabisa kuwa kuna tatizo la ukamilifu kwa mwanasheria huyo mkuu wa Chadema.

“Suala la mwisho Lissu hana maadili…kama atabisha nitatoa ushahidi…” alidai Wasira ambaye amekuwa waziri katika awamu nne za serikali.

Ingawa jana, Lissu hakupatikana, lakini alipozunguma na Mwananchi wiki iliyopita alisema huwa haogopi kusema ukweli.

Chanzo:
Mwananchi

My take: Wasira ana stress za kukosa ubunge katika jimbo lake. Pia ana stress za kukosa teuzi za Magufuli. Pole MZEE Tyson.
 
Source: Mwananchi
KUSEMA UKWELI SIO KUTUKANA! NYERERE ALIKUWA NA MAPUNGUFU KAMA BINADAMU WENGINE. ALIUA, ALIWEKA WATU NDANI, WATU WALIKOSA HUDUMA MBALI MBALI WAKATI WA KUNANA MATUMIZI, HAKUPENDA KUKOSOLEWA, ETC. ALIKUWA NA UDIKITEITA WA AINA FULANI. HAKUWA MKAMILIFU KAMA WASIRA ANAVYOTAKA KUTUAMINISHA, HAKUWA MALAIKA, ALL MEN ARE FALLIBLE NO MAN IS INFALLIBLE
 
Hata sheria hajui, anaanghaika na vikesi ambavyo vinakuwa vimepangwa makusudi kumsumbua alafu anajisifia.Anapambana na kopolo wa polisi alafu watu wanamwona hodari.

Hafakii hata roho ya Lamwai na Marando ukimwacha Dr Tenga, Mkono n.k
Sema haki ya Mungu
 
Wasira ana hasira na Lissu amemgalagaza mbaya kwenye kesi ya Ubunge.......hana hamu naye!! Mzee ya Gombe pumzika tu!!
 
Lissu ni mkweli siyo mnafiki ndiyo maana kila anayeboronga anamlipua.

Kuhusu Lowassa ile ilikuwa siasa. Mtu anaona una mke mzuri mumetulia mnaishi vizuri anamtamani. Anaamua kuanzisha fitina kwamba mkeo ana shida fulani. Ukiingia king unamuacha jamaa anabeba.

Kifupi waliozusha ufisadi wa Lowassa ni chadema na wanaomsafisha ni chadema na ccm. Na ni ukweli usiopingika kuwa Lowassa siyo fisadi. Ndiyo maana hata mahakama ya mafisadi haimgusi. Zile zilikuwa siasa.

Tyson achana na Lissu atakuumbua. Lissu ni mjuvi wa sheria na haogopi kima yeyote. Hata ungekuwa na mapembe.
 
Rejea Tundu Lissu: Nmenusurika kupigwa na Steven Wassira, ngumi ya kwanza nliikwepa
Wasira ajibu:
Waziri wa zamani katika Serikali ya Awamu ya Nne, Stephen Wasira amemshukia Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu kwa mambo manne.

Moja ya mambo ambayo Wasira amesema ni kwamba mbunge huyo wa Chadema hana heshima kwa viongozi wakuu wa nchi.

Wasira alisema hayo baada ya Lissu kudai kuwa alinusurika kupigwa na kada huyo wa CCM wakati wa vikao vya Bunge mjini Dodoma, habari ambayo ilichapishwa jana na Mwananchi.

Akijibu tuhuma hizo, Wasira (pichani) alisema Lissu anaongea kama vile hayuko sawasawa kwa sababu yote aliyoyasema ni uongo, hajui yalitokea wapi na hajui sababu zake.

Wasira alisema hakuna mtu mwenye akili timamu anayeweza kumtukana Rais wa Awamu ya Kwanza, Mwalimu Julius Nyerere, lakini alimshangaa Lissu alipothubutu kufanya hivyo wakati wa Bunge Maalumu la Katiba.

Alisema Lissu pia alimtuhumu mambo ya uongo Mwalimu Nyerere kwa kudai alighushi saini ya mwasisi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Abeid Amani Karume kwenye hati ya Muungano. “Hata wapinzani wenzake walimshangaa,” alisema Wasira.

“Huyu mtu amethubutu kuwatukana maraisi waliopita, kamtukana (Benjamin) Mkapa, kamtukana (Jakaya) Kikwete ambaye alimkaribisha Ikulu na kunywa juisi huku amejikunyata, sasa anamtukana Rais (John) Magufuli. Mimi si msemaji wa Magufuli, lakini huyu Lissu amekuwa anamtukana,” alisema Wasira huku akisisitiza kuwa Lissu hana heshima na maadili.

Wasira alisema kutokana na vitendo hivyo inaonekana Lissu ana matatizo kwa kuwa mtu aliye kamili hawezi kufanya vituko vya aina hiyo.

Pia, alimshangaa Lissu kuwa mstari wa mbele kumsafisha kwa maelezo mazuri Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, wakati alikuwa wa kwanza kumtuhumu kwa kumuita fisadi kiongozi huyo alipokuwa CCM, akisema huo ni uhalisia wa mtu ambaye mara zote amekuwa hasemi kweli.

“Nashangaa leo ndiye amekuwa mstari wa mbele kumsafisha kwa brashi ya chuma baada ya Lowassa kujiunga nao,” alisema huku akibainisha kwamba hizo ndiyo dalili za mtu asiyesema kweli.

Alisema Lissu kumsafisha Lowassa inaonyesha kabisa kuwa kuna tatizo la ukamilifu kwa mwanasheria huyo mkuu wa Chadema.

“Suala la mwisho Lissu hana maadili…kama atabisha nitatoa ushahidi…” alidai Wasira ambaye amekuwa waziri katika awamu nne za serikali.

Ingawa jana, Lissu hakupatikana, lakini alipozunguma na Mwananchi wiki iliyopita alisema huwa haogopi kusema ukweli.
Source: Mwananchi
My take: Wasira ana stress za kukosa ubunge katika jimbo lake.
Kwa hiyo huyu mzee anataka kutuaminisha huyo mungu nyerere alikuwa kweli Mungu!. Tunajua walikuwa na undugu. Baba wa Umaskini Tanzania ni Nyerere na alijaa gubu kwa waliokuwa nacho.
 
Sijaona alipokanusha kurusha ngumi, zaidi amejikita katika tabia za kisiasa za Lissu!
Naona amepiga 180 degrees. Kaanzisha uzi mwingine lakini hoja kweli hajaikanusha. Gazeti nao hawajambana ipasavyo.
 
Back
Top Bottom