Umslopagas
JF-Expert Member
- Jun 13, 2013
- 214
- 157
Eneo la South China Sea ni eneo muhimu sana ki biashara, asilimia 70-80 ya meli zote kutoka au kwena nchi za Asia na Japan hupitia hapa zikiwa zimeshehena malighafi na bidhaa mbalimbali.
Eneo hili linapakana na nchi nyingi tu na kwa miaka mingi limekuwa international water, miaka ya hivi karibuni China imeweza kujenga visiwa bandia (Man made Islands) kwenye hii bahari na hivyo kugeuza eneo kubwa la hii bahari kama ardhi yao bila kujali kelele kutoka nchi zinazo pakana na hii bahari na ambazo ni washirika wa Marekani.
Marekani imetuma meli na ndege za kivita eneo hili na kuna hari ya sintofahamu, katika hali isiyo ya kawaida Wamarekani wamepeleka hadi Aircraft carrier kitu ambacho si cha kawaida, kwani meli hizi huwa hazipelekwi maeneo yenye migogoro kwani zinakuwa protected sana kutokana na thamani yake.
General mmoja wa China ameishauri nchi yake kuzizamisha hizi manowari za Marekani na anadai hii itawafanya Wamarekani wachomoke mbio kwani hawawezi kustahimili pigo kama hili.