Kimara yalowa maji, kero ya maji yaisha

Tanzania Nchi Yetu Sote

JF-Expert Member
Mar 12, 2017
505
858
Ni jambo la kufurahisha sana kwa wakazi wa maeneo ya Kimara na viunga vyake kupata maji ya DAWASCO. Kimara ni moja ya maeneo ndani ya jiji la Dar ambako ilikuwa ukimuuliza hata mtoto mdogo kero ya eneo hilo atakwambia maji.

Kukosekana kwa maji eneo la Kimara pamoja na sababu nyingine lakini kulikuwa na mikono ya baadhi ya watu wenye nguvu waliogeuza mradi wa kuuza maji kwa magari kuwa njia yao kuu ya kujipatia mapesa. Hali hiyo ikafanya suala la kupata maji ya bomba kuwa kilio cha miaka nenda rudi.

Shukrani za pekee zimfikie aliyefanikiwa kuvunja genge la wauza maji Kimara.
 
kwa hiyo kero zenu chini ya serikali ya awamu ya tano chini ya rais Magufuli zimepatiwa ufumbuzi?
 
Naunga mkona asilimia 100. Nina miezi zaid ya miwili sijaona maji yakikatika Kimara.
 
Back
Top Bottom