Kilumbe Ng'enda: Mbunge Azzan Anahusika na Biashara ya Dawa za Kulevya

Omutwale

JF-Expert Member
Feb 4, 2008
1,429
1,045
Je, wajua kwa nini Idd Azan alisitisha mbembwe za kuunga mkono kampeni "Vua Gamba" kwa aibu na kwa kuomba msamaha?
Posted 24th May 2011 13:08
Kilumbe anaelezwa kwamba alimsema hadharani Mbunge Azzan kuwa anahusika na biashara ya dawa za kulevya katika kikao cha UVCCM wilaya ya Kinondoni, na hivyo kuharibu hali ya hewa.
SOURCE: IPASHE JUMAPILI - http://www.ippmedia.com/frontend/?l=30067

Una fununu ya ugomvi kati ya Madabiba na Azzan?

Soma comment hii ya 21st May 2013

Mfanya biashara mkubwa Nguli wa madawa ya kulevya hata pale Magogoni wanajua!
 
Duhh kumbe haijaanzaa leo!!
Huwa nawashangaa watu. Sijui labda huwa hawasomi au ni uharaka wa kusahau? Idd Azan hakuanza kusemwa leo kwenye hiyo biashara ya madawa ya kulevya na kutakasa pesa kwa kununua mikoko.
Tembelea: Mh. Iddi Azan anafanya biashara gani?
 
Sasa Idd Azzan anapojifaragua leo kuwa vyombo vya dola vifanye uchunguzi na akibainika anajiuzulu ndipo tunapata picha kuwa anajua kuwa yeye ni mhusika. Kama katibu wake wa mkoa alimtuhumu hadharani na hakuna mahali anapoonekana akikanusha, na hata kama angetoa kauli ya kukanusha lakini kauli ya katibu wake wa mkoa ilikuwa thabiti na ndio maana baadae alienguliwa uongozini.

Nadhani Idd Azzan atakuwa na watu wazito zaidi nyuma yake, kama waliweza kumuweka pembeni katibu wa mkoa wa dsm watashindwa nini kumnasua sasahivi na kadhia hii ikiwa bado mkuu wa kitengo cha madawa ya kulevya ni mtuhumiwa Godfrey Nzowa!!?
 
Iwapo Ridhwani alikamatwa na hayo madawa huko China na akaachiwa kwa kuiweka nchi rehani ,je unafikiri vyombo vya dola hii vina moral authority ya kuwakamata wengine wanaohusishwa na biashara hiyo??

...nakusoma sana mkuu, kwa maneno mengine bwana iddi anasema thibitisheni tuhuma zenu kama mtaweza....
 
Kauli alizotoa mbunge kwa mtu makini atagundua kuna walakini.

Uchunguzi wa kweli unahitaji vyombo vya nje, tena hao hao FBI tuliozoea kuwaita kuchunguza mabomu.
 
Kazi kwelikweli. Nafikiria kuhama hii nchi, yaani utadhani ni senema. Kumbe kweli bwana mtu anakuwa mheshimiwa tena m/kiti wa bunge , kumbe zungu la unga,
 
Naikumbuka vizuri sana ile thread ya JoJiPoJi, ya march 2011.Ni dhahiri kama kwa mwaka huo ilikuwa lisemwalo lipo, basi sasa yametimia na afanye haraka kujiuzulu kwa maslahi ya taifa ili uchunguzi huru ufanyike.
 
Last edited by a moderator:
Heshima kwako mkuu Omutwale maana umeniweka sawa kabisa na kwa kweli huyu mzungu wa unga hana pa kuchomokea ni kweli ametajwa na katibu wake wa magamba kunani tena?masisiem ni janga la kitaifa na hii atasafishwa maana hata mwanamfalme alibambwa china..
 
Last edited by a moderator:
haya mambo si kwamba Rais hayajui anafahamu vizuri saana, anawafumbia macho maana ndo wafadhiri wa kampeni zake
Yani he treats us (people who gave him the job) like ------, anaifanya Tz, her people and their children wase..ge. THANK YOU MR.PRESIDENT!
YOU IGNORE THE CRY AND TEARS OF TZ PEOPLE BUT GOD PICKS UP AND REMEMBER EVERY DROP!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…