Donatila
JF-Expert Member
- Oct 23, 2014
- 7,563
- 21,665
Mwanamke mmoja aliyetambulika kwa majina ya Yunis Peter mkazi wa jiji la Dar es Salaam ameuwawa kikatili kwa kuchomwa na kitu chenye ncha kali shingoni katika nyumba ya kulala wageni ijulikanayo kwa jina la Sayari Guest House iliyopo mji mdogo wa Ifakara wilayani Kilombero.
Akielezea tukio hilo mhudumu wa nyumba ya wageni Ester Mshimika amesema alistuka baada ya kuona kitendo cha mmoja wa wateja waliokuwa katika chumba kimoja kutoonekana kwa muda hali iliyompa wasiwasi na kuamua kutafuta msaada kwa ngazi zinazohusika.
Mganga wa zamu wa hospitali ya Mtakatifu Fransisco iliyopo mji mdogo wa Ifakara Isaya Msumba ameeleza namna alivyoupokea mwili huo huku Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro Ulrich Matei akithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba jeshi hilo linaendelea kumtafuta mtu aliyehusika na tukio hilo.