Mishahara duni, ukosefu wa makazi, mazingira magumu ya kufanyia kazi kwa walimu, ni kilio cha muda mrefu kwa walimu (walezi wa jamii). Ila kwa masikitiko makubwa serikali imeziba masikio na kutotaka kabisa kuwaboreshea walimu maisha yao na mazingira ya kazi ili wawe na ARI ya kufundisha na kutoa matunda bora....Mwaka jana, walimu wote nchini waligoma kufanya kazi takribani wiki nzima kuishinikiza serikali kuboresha maisha ya walimu ila dola ilikimbilia mahakamani kuzuia mgomo ule...Mahakama baada ya kuzuia mgomo, ilitoa sharti baina ya serikali na walimu kukaa meza moja kutafuta suluhu.CHA KUSHANGAZA,SERIKALI IMEKUWA IKIWAKIMBIA WALIMU KUKAA MEZA MOJA NA HADI LEO HAWAKO TAYARI KUFANYA SULUHU. Kwa manung'uniko walimu walirudi kazini wakiwa hawana ARI ya kufanya kazi, imepelekea MATOKEO YA DARASA LA SABA NA KIDATO CHA NNE 2012 KUWA MABAYA KUPINDUKIA. Kutokana na kelele nyingi na malalamiko ya watanzania juu ya ANGUKO LA ELIMU,waziri mkuu akaunda tume ya kutafuta kiini hasa cha matokeo mabaya.....Cha kushangaza tume kati ya matatizo yaliyo baini eti MASLAHI DUNI, KUKOSEKANA KWA ARI NA UTAYARI WA MWALIMU KUFUNDISHA SI CHANZO CHA MATOKEO MABAYA.....Walimu tumegundua kuwa tume husika haikuundwa kwa dhamira ya kutafuta mzizi wa ANGUKO LA ELIMU, na ndo maana wameelekeza mashambulizi yao yote baraza la mitihani. Watanzania, hv ni kweli kuw anguko la elimu Tanzania linasababishwa BMT?? Haya serikali inalitaka baraza la mitihani litumie huo mfumo wa 2011(50% ya wanafunzi walipata 0) je mwaka huu ndo watoto walifaulu sn?? KIUJUMLA WALIMU TUNAENDELEA NA MANUNG'UNIKO YETU JUU YA UKANDAMIZWAJI WA WALIMU NA UHUJUMU WA ELIMU. MUNGU IBARIKI TANZANIA!!