Mbombo Nunu
Member
- Feb 10, 2018
- 92
- 123
Toka 2014 mpaka sasa,inakaribia takribani miaka 5 tangu (WILLIAM FULTON) mmiliki na mkurugenzi wa kituo cha MANGO TREE ,kituo kilichokuwa kikihusika na Msaada Wa kielimu kwa Yatima,Wenye Mahitaji maalumu na waishio katika mazingira magumu ya kimaisha,alipowekewa zuio la kuingia nchini kuja kuangalia,kuendeleza na kusimamia miradi yake ya Ufadhiri aliyokwisha iasisi.
Sababu kubwa ni katika kile ambacho hata Mheshimiwa waziri Wa mambo ya ndani amewahi kukizungumza kuwa,haoni na hakuna ushahidi Wa kosa lolote lililowahi fanya kutolewa kwa zuio juu ya bwana Fulton, hajaliona na hakuliona kwenye ofisi yake na hata alipofika uhamiaji hakuiona wala kupewa sababu ya msingi,na hata waziri Mkuu aliwahi kukaririwa akikiri kuwa anafahamu na anataarifa juu ya uwepo wa kundi la watu wachache waliotengeneza mazingira ya dhurma na kujimilikisha Kituo kiubabe kwa sababu zao binafsi na kwa kutumia nguvu ya nafasi zao kiutawala ,hatimaye wakamtilia ndimu mzee Wa watu na kufanikiwa kwenye mipango yao.
Aibu yao ni kwamba walidhani mzee anafaidi,hivi tunavyozungumza ni habari nyingine tofauti,miradi yote ikawafia mikononi mwao miaka michache tu baada ya kujimilikisha ,watoto waliokuwa wamefaulu elimu za juu wakaanza kulia ukata Wa kutohudumiwa/kutosaidiwa kwa pesa ya kujikimu na ADA,hata wengine kupelekea kufukuzwa toka mashuleni kurudi majumbani,achilia mbali hata kituo chenyewe kushindwa tena kuwapokea watoto walio kwenye mazingira magumu na kuwasaidia kwa mujibu Wa usajiri Wa kituo hata kama walikidhi kuwa sehemu ya wasaidiwa kwa mujibu wa hali zao pia.
Hivi tunavyozungumza ni Habari nyingine kabisaaa,MANGO TREE imekufa kifo cha mende ,watoto wametawavyika hovyo hovyo wengine wamerudi kwenye kuomba Omba ili mradi wajisogeze mahala ,kila mmoja na njia yake,wangine wamerudi kwenye maisha yao ya kimatukio mtaani baada ya kuishia njia Kielimu na kukosa mkono Wa Heri mbadala Wa mzee William Fulton, kwa kipindi chote hicho wahanga wamekuwa WAKISALI NA KULIA KUOMBA MZEE FULTON ARUDI NCHINI kwa kurejea kauli ya waziri Mkuu kuwa hakuona na haoni tatizo lolote linalopelekea KUZUIWA KWA FULTON,lakini sasa MOYO WA UPENDO WA MZEE WILLIAM FULTON HAUJUI UTAWASAIDIA VIPI WALE WATOTO AMBAO ALIWAZOEA NA ALIWALEA KAMA SEMEMU YA FAMILIA YAKE NA KUWASAIDIA KUTIMIZA NDOTO ZAO,ALIKO NAYE ANATOKWA NA MACHOZI HASA PALE ANAPOPIGIWA SIMU NA BAADHI YAO NA KUAMBIWA KUWA mango tree IMEFARIKI kama kituo,na ZAO LAKE AMBALO NI CHUO CHA KPC kilichowafanya waheshimiwa sana kuwekeza huko walau kwa akili na nguvu zao ili wakitendee haki kibiashara zaidi wasijedondoka jumla jumla nacho pia ndio hivyoooo KINAKOSA UELEKEO kwa MITAFARUKU ISIYOISHA YA KIMGONGANO WA MASRAHI.
Chonde chonde waheshimiwa sana ,inawezekana mlitaka kujaribu lakini nia mbaya yenu ndio inayowatafuna nyinyi kwa nyinyi leo hii kwa sababu ya kutokuwa na mikakati thabiti na kutojua namna gani hizi Charity Institutions zinapaswa kusimamiwa na kuendeshwa,miroho yenu mibaya ya kutaka kurefusha matumbo yenu yatokee mbele ndio yanayoishi pamoja nanyi,figisu figisu zinawatokea puani.
Kilichoumiza na kinachoumiza ni kwamba bado mzee Wa watu baada ya kusikia kilio cha jamii ya walezi na watoto wa wana ukanda Wa nyanda za juu kusini ,pamoja na kwamba ana project nyinginezo kama hizo katika baadhi ya nchi barani afrika ,AMESEMA HANA KINYONGO NA JAMII HUSIKA KWA VILE ALIVYOISHI NAO na YUPO TAYARI KUJA KUWAFUTA MACHOZI ENDAPO MAMLAKA HUSIKA ZITAYAKUBALI MADHAIFU YA UPANDE WAKE ULIOJITOKEZA KUFUATIA ZUIO LAKE NA KUAMUA KUTENGUA,naye amesema amejaribu kuomba hivyo Mara kadhaa lakini ugumu huja kwa KUNG'ANG'ANIA kwa wale walioamua kujimilikisha na Kushindwa Kukabiliana na AIBU ya KUTENGUA ZUIO LISILOWAHI KUWA NA SABABU MAALUMU YA KIMAMLAKA zaidi ya misuko.
Swali ni NANI JASIRI WA KUMSEMEA MZEE KUTOKA KWENYE ZUIO LILE AMBALO ANALO HATA SASA AJE KUKIOKOA KIZAZI KILE KILICHOTAPANYWA NA WACHACHE KWA MASLAHI YA TAIFA HILI?
Nyuma ya pazia.......siasa za Kyela.......siasa za Tanzania zilichangia pakubwa kwenye kuirudisha jamii yake yenyewe nyuma.