Mk54
JF-Expert Member
- Dec 29, 2016
- 1,997
- 3,933
Miongoni mwa Project zilizoanzishwa kwa muktadha wa Public Private Partnership ni mradi wa mwendokasi.
Kampuni iliyoshinda tenda ya ujenzi wa barabara na miundombinu ni Strabag kutoka Ujerumani kwa mkataba wa EUR 179. 6 Million huku Serikali ikiwa ni muangalizi wa miundombinu.
—Tumeona kwa upande wa Serikali ilivyoshindwa kusimamia miundombinu ya mradi huu. Tumeona jinsi ambavyo barabara zinavyoharibiwa, traffic light zinavyotolewa yaani barabara zinazidi kuharibika siku hadi siku pasipokuwa na action yoyote.
Nchi hii ina Wajumbe,Madiwani , Wakuu wa Wilaya, Wakuu wa Mikoa , Waziri wa Tamisemi na Usalama wa Taifa wote hawa ni Makada wa CCM lakini wameshindwa kujua chanzo cha uharibifu huu na kuwakamata wote wenye kuhusika na uharibifu.
Hivi hii nchi ni nini shida? Maana hizi barabara zinaharibiwa na watu wa mitaani, wanatoa zile nondo na kwenda kuuza, wanavunja vizingiti na kutengeneza njia, hakuna anayefuatilia hili swala.
Haya ndiyo mambo ambayo Makonda unapaswa kuwa na majibu nayo. Mkoa wa Dar unaongoza kwa uchafu, kila kitu ni hovyo halafu unapoteza muda kupambana na Konki Likwidi—Makonda unakwama wapi ? Wewe si ndiyo Rais wa Dar ?
-------------------------------
— kwa upande wa Kampuni iliyopewa dhamana ya uendeshaji wa mabasi wamefeli kwenye kila idara, kuanzia kwenye kutoa Huduma, kukusanya Mapato, kuwalipa Mishahara Wafanyakazi na vifo vya Raia kwa uzembe wa Madereva.
Aidha , Madereva wamekuwa na hasira ya kutolipwa hivyo kwa uzembe na makusudi wamekuwa wakigonga hovyo hovyo, spidi 120 hata sehemu zenye mkusanyiko wa watu, au sehemu zenye mataa.
Sipati picha huko mbagala itakuwaje.
Mwendokasi ulianza kuua kiwete pale Msimbazi, ukaja kuua mtoto pale Gerezani, ukaja kuua Mdada wa Kihindi pale Kisutu, ukaja kuua muendesha Boda Boda pale Manzese, ukaja kuua muendesha gari pale Mapipa Magomeni siku ya Ijumaa 19, Aprili 2019, what is wrong ?
Hawa traffic na wasimamizi wa barabara, wanafanya kazi gani?
Yote haya yamekuwa chini ya kapeti na hatuoni Action yoyote ikichukuliwa, are they above the law? —BS !
Mmeshindwa kusimamia mradi, Na watu wetu pia bado mnatuulia Kwakweli hii nchi inahitaji maombi, tena maombi ya wapagani maana maombi ya watu wa dini yamefeli kwa dhiki na njaa zao za matumbo yao makubwa.
—Zile mbio za Jaffo za kutatua kero za mradi huu ziliishia wapi vile
Hivi ripoti ya CAG Imesemaje kuhusu huu mradi
Tunatambua mchango wa John Magufuli, na jitihada za kuweka nchi sawa. Lakini tunapata
Kigugumizi as in why Rais halitolei ufafanuzi hili swala ikiwa ni pamoja na kumuwajibisha Mkurugenzi mwenye dhamana ya kusimamia huu mradi, na Waziri wake.
Mbona kina Nape, Mwigulu na wengineo walimalizwa on spot bila ya kupoteza muda.
Rais Magufuli wewe ndio unamajibu ya haya maswali na utawapunguzia kero raia wako endapo haya maswali yatajibiwa kwa HERUFI KUBWA.
Katika Utendaji,
MK54, Raia Mwema
Jumamosi 20, Aprili 2019.
-----------------------