Kilio cha miradi ya serikali kutelekezwa

Kilio cha miradi ya serikali kutelekezwa

Kulwa Jilala

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2022
Posts
3,889
Reaction score
8,486
Mwaka 2019 ulipoanza ujenzi wa zahanati ya kijiji cha Mwabayanda kata ya Sukuma wilaya ya Maswa ,mkoa wa Simiyu wananchi walifurahi mno na kurukaruka kuwa mwisho wa adha ya kutembea umbali mrefu kufuata huduma za afya umefika mwisho kwenye kijiji chao lakini kumbe haikuwa hivyo!
Baada ya zahanati kukamilika ujenzi wake mwaka 2020 imebaki gofu na haijawahi kufanya kazi yoyote na wananchi wameendelea kutembea zaidi ya kilomita 30 kufuata huduma ya afya kana kwamba hamna zahanati kwenye kijiji chao !

Kisingizio cha viongozi cha kutoifungua zahati hiyo ili wananchi wapate huduma imekuwa ni kwamba hawajapata waraka kutoka wizara ya afya!
Ama hakika Rais Samia unahujumiwa na watendaji wako huku chini.
 
Back
Top Bottom