Kilimo ni uhai vs kilimo kwanza

kanta

JF-Expert Member
Jan 24, 2011
343
65
Wakati wa zama za uongozi wa Mwalimu Nyerere kulikuwa na kauli mbiu ya KILIMO NI UHAI ili kuhamasisha wananchi kukifanya kilimo kuwa ni sehemu ya maisha yao. Katika kufanikisha azma hii Ungozi wa Mwalimu uliandaa wataalam wa kilimo pamoja na kuwawezesha wananchi kwa kuwaandalia soko la mazao ikiwa ni pamoja na uanzishwaji wa vyama vya ushirika ambavyo kwa namna moja au nyingine vilikuwa vikimilikiwa na wanachi wenyewe kwa kusaidiwa na serikali.
Lakini katika uongozi wa sasa kuna kauli mbiu mpya ya KILIMO KWANZA ambayo wanasema imelenga kukifanya kilimo kiwe cha kisasa zaidi na hivyo kuongeza uzalishaji maradufu.Kutimiza azma hii, serikali imeagiza power tiller na kusambaza katika maeneo ya kilimo kwa namna ambayo wao wameona ni sahihi kwa ajili ya kutimiza mpango huo wa kilimo.

Swali langu naomba mnisaidie wadu, je ni kauli mbiu ipi imeweza kufanikiwa kati ya hizi mbili. Kati hizo mbili ni ipi ilikuwa imelenga kumkomboa mkulima wa chini na masikini katika nchi hii. Tofautin zake ni zipi kwenye kufanisha mipango hiyo miwili kwa nyakati hizo tofauti?

NAWASILISHA.
 
Back
Top Bottom