ASHA NGEDELE
salaamu ndugu, nimekuapta, naomba nichangie kwa mujibu wa uzoefu nilio nao
Je
1. Linakatwa tunda linalozidi na linakatwa wakati gani wa ukuaji wa matunda? i. Ni vyema sana kama endepo matunda yanayoachwa hayo 2-3 yawe katika shina mama, kwa kuwa yatapata chakula direct kutoka shina mama, lakini kwa kuwa shina mama hutengeneza matawi na kuna wakati matawi pia huwa na matunda, ni vyema kuchunguza kwa makini matunda yalipo (Shina mama/tawi) kabla ya kukata. ii. Muda mzuri wa kukata ni mapema tu unapokuwa umejiridhisha kuwa hili ni tunda, coz kuna maua ya dume na jike, tunda ni lile unakuta juu kuna ua na chini kuna kitunda kidogo, hivyo lile lililo ua tu, hilo ni la kiume ni la kutoa
2. Linakatwa shina baada tu ya tunda lako la mwisho na linakatwa vipi na wakati gani ili kutoathiri ukuaji wa mmea?
=Linakatwa mapema tu baada ya tunda kuwa limejitengeneza hata likiwa saizi ya gololi unahesabu matunda matatu kutoka kwa kamba husika, kama unakuta matunda hayo matatu yanakuwa katika shina mama inakuwa vizuri zaidi, kata hizi kamba za pemebeni ili zisitengeneze maua/matunda ili chakula kibaki kutumika katika maina shina. Kisha una vunja kule mbele ili kusiendelee kutambaa zaidi na kutoa matunda, unavunja kama unavyochuma majani ya maboga etc
3. Kama linakatwa shina ili matunda yapate chakula yanakatwa mashina yenye matunda au hata mashina ambayo hayana matunda?=Kikubwa hesabu hayao matunda matatau yanapatikana kwanza?, kisha kata hizo kamba zinazoendelea mbele baada ya matunda na hata kamba za pembeni , coz hizo kamba za pembeni zitakuwa zinakula chakula cha bure, matunda yanayozaliwa pembeni mwa kamba (pembeni mwa shina mama)mara nyingi huwa hayawi makubwa, coz chakula hakiji kingi kwa hayo matawi ya pembeni.
Pia ningependa kujua mmea mmoja wa tikiti unahitaji maji lita ngapi kwa siku,
= Angalau lita 1 kwa siku kwa mche, wastani wa 10,000 lita kwa eka kwa siku
=====