Kilimo cha pilipili

ASHA NGEDELE

JF-Expert Member
Jul 5, 2011
784
327
Habarini wakuu,

Nataka kulima Pilipili kibiashara kwa kilimo cha umwagiliaji. Sina taarifa za masoko kwa ukanda wetu wa Pwani esp Dar es Salaam.

Naomba kujua pilipili zipi ambazo zina soko zuri kwa uhitaji wake sokoni na bei kati ya Pilipili Mbuzi, Pilipili Kichaa, Pilipili Hoho na kadharika.

Pia naomba ushauri wa changamoto ambazo ni common kwa kilimo hiki cha pilipili kwa upande wa magonjwa na wadudu shambulizi.

Natanguliza Shukrani.

CC: kilimomaarifa.tajiri Kilimo Faida Upepo wa Pesa @
 
Nina shamba , nimeshaanza kidogo kulima pilipili mbuzi . pilipili mbuzi ni deal sana mwezi wa sita hadi mwezi wa kumi zina pesa balaaa.
Njoo tufanye joint venture.
 
Nina shamba , nimeshaanza kidogo kulima pilipili mbuzi . pilipili mbuzi ni deal sana mwezi wa sita hadi mwezi wa kumi zina pesa balaaa.
Njoo tufanye joint venture.
Unalima wapi ? Ni PM kama uko Dar
 
Pilipili ni zao ambalo soko lake halitabiriki mwaka juzi ilipanda sana hadi 40000 kwa ndoo kubwa mwaka jana hadi sasa bado ndoo ni chini ya 10000 nimelima imenitesa sana kuuza walao mboga hasa mchicha na chinese zinalipa na zina soko
 
Duh hapo unamaanisha pilipili aina zote au specifically ulizolima wewe?? Umelima aina gani ya pilipili?
 
Pilipili ni zao ambalo soko lake halitabiriki mwaka juzi ilipanda sana hadi 40000 kwa ndoo kubwa mwaka jana hadi sasa bado ndoo ni chini ya 10000 nimelima imenitesa sana kuuza walao mboga hasa mchicha na chinese zinalipa na zina soko
Pilipili mbuzi bado ni dili mkuu. Ukiweza kumaintain production miezi hiyo ya June mpaka October unapiga pesa nyingi mkuu
 
Ni kweli kipindi hiki pililipili hasa kwa huku mashambani ni nyingi sana kupindukia
 
Bei ipo chini zaidi , ni pungufu ya 6000 kwa ndoo kubwa.
Lakini kwakuwa sio zao la msimu , ukiweza kumwagilzia unaendelea kuvuna
 
Asante kwa hii taarifa ya masoko.. Je unaongelea pilipili ipi sasa?? Zipo aina tofauti za pilipili
Mimi naongelea pilipili mbuzi. Ukiwanazo nyingi hata zikikosa soko waweza kuuza mbegu zake ambazo nazo zina soko tena zuri mno
 
Kuna pilipili mbuzi naanza kuziona zikikomaa zinakua za njano sio nyekundu kama zile nyingine,na zinaharufu nzuri na ni kali kwel kweli kuna mwenye uzoefu nazo tafadhali anisaidie zinastawi wap zaid
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom